Mimi nimaswali, Hivi kwauzoefu wako mzee wetu unaona kunatofauti gani ktk mapenzi ya faragha ya sasa na ya enzi zenu...
Pia unaona kwasasa ni jinsia gani kwenye mapenzi imepoteza mbinu/ushirikiano ilikunogesha mgegedo..
Ahsante
Sent using
Jamii Forums mobile app
Mapenzi ya enzi zetu ni tofauti sana na mapenzi ya siku hizi.
>Vigezo vya kumfanya mwanaume ampende mwanamke sikuhizi vingi vimebadilika vivyo hivyo vigezo vya mwanamke kumpenda mwanaume baada ya kutongozwa (ama bila ya kutongozwa) pia vingi vimebadilika.
Mfano:-
(a) Uzuri / Haiba
Ingawaje kila mtu hutafsiri kwa namna yake kuhusu uzuri / haiba ya anayempenda, lakini siku hizi watu wengi hupenda uzuri / haiba isiyo halisi kama vile nywele bandia, kope bandia, kucha bandia, ngozi iliyochubuliwa, makalio ya kujionhezea kwa madawa ama madogoro nk. Ilimradi unakuta mtu anavutiwa na haiba isiyo halisi.
Zamani watu walipendana kwa uzuri ama haiba halisia ingawaje mapambo pia yaliongezea lakini bila kubadili uhalisia.
#Haiba fake 'hukata stim' in time!
Hence mapenzi / Mahaba hupungua, michepuko huanza ama kuendelea...
(b) Umri
Zamani ilikuwa na mara chache sana watu kupendana (kimahaba) wakiwa na tofauti kubwa ya umri, siku hizi siyo ajabu tena kijana wa kiume mwenye miaka 20 hivi akampenda kimahaba mwanamke sawa na mama yake! Kauli maarufu "umri siyo kitu, ni namba tu'; vivyo hivyo siyo ajabu tena kwa mama wa miaka zaidi ya 50 kumpenda (kumtaka kimahaba) kijana wa miaka 20 hivi.
Sugar Dadies na Sugar Mamies walikuwepo tangia zamani, lakini kwa uchache sana, siku hizi ni kawaida.
#Tofauti kubwa ya umri huleta mgongano wa kimslahi kuhusiana na mapendeleo, kijana wa 20's atapenda kwenda night clubs mara kwa mara tofauti na wa 50's atakayependa kutulia na kujenga maisha, na mifano mingine mingi...
Hivyo, tofauti kubwa ya umri 'hukata stim' in time! Hususani kama kile kinachoshikilia uhusiano / mahaba hayo kuondoka (eg. Pesa)
(c) Tabia
Pamoja na kwamba kila mmoja hutafsiri anavyotaka kuhusu tabia za mwenza, lakini kuna tabia za msingi hubaki vilevile, mfano, heshima, ukarimu, uchapakazi nk.
Siku hizi watu wanaweza kupendana kwa kupenda tabia ya mwenza ambayo siyo ya msingi hata kidogo, mfano unaweza kukuta kijana anampenda msichana kwa tabia ya kujiweka mitandaoni akiwa katika mionekano na sehemu na matukio mbalimbali.
#Tabia ambazo siyo za msingi 'hukata stim' in time! Hususani mwenza akigundua tabia za msingi zako zilivyo.
(d) Ukwasi
Enzi za zamani watu WENGI walipendana bila kujali ukwasi wa mwenza, waliamini watajijenga pamoja, lakini sikuhizi wengi HULENGA kwenye ukwasi (japo si vibaya) ila isiwe sababu ya msingi kwa kuwa ukwasi huo ukiondoka 'hukata stim' in time!
NA KADHALIKA.
>Namna za utongozaji zimebadilika. Siku hivi ukipata namba ya simu tu, mtu hujihakikishia asilimia kadhaa (say 50%) amefanikiwa kukubaliwa. Na mara nyingi ina prove positive. Enzi zetu hadi kumpata mwenza ilikuwa ni mchakato, unasotea haswa, hadi mwenza anajiridhisha ni kweli unampenda naye anakuwa ameanza kukupa nafasi 'moyoni' mwake hivyo mnaanza kupendana. Mara nyingi walio oana kwa kutafutana kwa njia hii hudumu sana katika ndoa.
Siku hizi, siyo ajabu watu wakatongozana leo na leo leo ama in few days wakagegedana, wakawa wapenzi na hatimaye wakaoana.
>Namna za "uchakataji na ugegedaji" nayo siku hizi zimebadilika sana. Ingawaje kila mtu yuko huru 'kuchakata na kugegeda' atakavyo, lakini siku hivi watu wamepetuka mipaka. Watu wanapiga deki 'mitaro 071' na kuzamishaMO dushe, ingawaje tangia zamani watu walizama 'uvinza' ila hii ya kudeki 071 hata Gomora hawakufanya ( I bet)
Siku hivi wanaume wengi hugegeda juu juu, wanawake wengi hawafikishwi, na siyo kwamba wanaume hao hawana nguvu za kiume la hasha, bali ujuzi wa kumfikisha mwenza umepungua na wengi hawapendi kujifunza ama hujifunza kwa wasio na weledi wa fani husika.
Wengine 'wameharibiwa' (brain washed) na filamu za ngono hadi kudhani hawana nguvu za kugegedana, hivyo kujipendelea yeye mwenyewe bila kumjali mwenza (mke) na wana msemo wao maarufu siku hizi eti "atakojoa njiani wakati anaenda kwao" Kha! Sasa kama ni mkeo je! Tarajia kusaidiwa.
>Aidha, jinsia zote sikuhizi zinachangia kuzorotesha mahaba kwa kila jinsia na sehemu yake, kwa mfao kwa wanaume ni udhaifu wa 'uchakataji na ugegedaji' na kwa wanawake "kubana" mahaba hadi aone hela au 'anuse harufu' yake na uvivu wa kuwatia moyo (ikibidi kupiga hata jeki) wanaume wanaodhani hawana nguvu wakati wa ugegedaji.
Nakadhalika.
###Nitaandaa uzi kwa ajili ya kuelimisha namna ya kumfikisha mwanamke kunako###
Nawatakia Jumapili njema.
James Jason