Stiv
Member
- Jul 17, 2021
- 6
- 3
Karibu katika makala hii:
UHUSISHWAJI WA AFYA YA AKILI KATIKA UTOAJI A HUDUMA YA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI.
Uzingatiwaji wa afya ya akili katika jamii ya Tanzania uko katika kiwango kidogo, Athari zake huathiri walio na kasoro ya kiakili na wasio nazo, hivyo watoto na watu wazima wako katika hatari ya kuathiliwa kwa namna ya utendaji pia athari kubwa hutokea kwa watu wenye kasoro hizo kwa namna jamii inavyo wachukulia na kutokulinda haki zao.
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kipengele cha afya ya akili kiliingizwa katika mpango wa maboresho ya afya ya 2001
(1).Licha ya hivyo Katika ripoti ya shirika la afya duniani (WHO) ya mwaka 2017 hakukuwepo na data juu ya mpango au mkakati kwaajili ya afya ya akili ya mtoto, pia ripoti hio ilionyesha ukubwa wa tatizo la afya ya akili ni watu 2,727.86 katika mkusanyiko wa watu laki moja (100,000)
(2) Shida ya akili kwa watoto (Mental disorders in children) ni mabadiliko mahususi ya tabia, hisia (namna ya kudhibiti mhemko) na namna mtoto anajifunza, mabadikiko haya huweza kuleta msongo na kuathili utendaji na ukuaji wake.Shida hizi huweza kua sababu ya kuzaliwa au kutokana na mazingira yanayo mzunguka.
Shida ya akili kwa mtoto hujumuisha wasiwasi uliopitiliza pamoja na hofu (anxiety), sonona (depression), msongo baada ya kupata tukio lililo athiri akili (posttraumatic stress disorders), kasoro ya kitabia (conduct disorders), kasoro ya kiakili inayopelekea tabia ya kutotoa ushirikiano na kupinga (opposition defient disorder), obsessive compulsive disorder, kasoro ya akili inayopelekea kukosa utulivu (attention deficit hyperactivity disorder), usonji (autism spectrum disorders), kushindwa kujifunza (learning disability) na shida ya mawasiliano (communication disorders)
(3) . Hizi kasoro huweza kuonesha tabia tofauti tofauti uwepo wa maarifa kwa walimu wazazi na jamii huleta matokeo chanya hususan katika ufanisi wa mtoto. Licha ya uwepo wa kasoro hizo. Pia mabadiliko ya kiakili na mitazamo huweza kutokea kwa mtoto ambae awali alikua kawaida. Mabadiliko hayo huchangiwa na mwingiliano wa mazingira ya jamii na mitazamo ya nje.
Watoto wadogo wa shule hutumia muda mwingi kwa siku katika shule, na miaka mingi wakiwa mashuleni. Katika kuhakikisha hawa watoto kufikia kiwango stahiki cha uwezo wao ni muhimu kuhusisha msaada madhubuti katika afya yao ya akili. Ukizingatia kuwa katika darasa moja ndani ya shule nyingi nchini Tanzania huwa na wanafunzi wengi wakiwa na uwezo tofauti hivyo basi ni muhimu sana kuwa na mpango wa jumla na mpango wa mtoto mmoja mmoja. Shule huchangia katika ukuaji wa mtoto, sio tu kwenye mwingiliano na watu bali pia katika kielimu, upambanuzi wa changamoto, kutawala hisia, maendeleo mema na tabia na maadili mema
(4) Uwezeshwaji mashuleni unahusisha kuwepo kwa sera maalum ya afya ya akili ya mtoto mashuleni, maarifa na taarifa juu ya mahitaji maalumu jumuishi kwa wanafunzi wote na ya mmoja mmoja, na shughuli mbalimbali zitakazo imarisha afya ya akili ya watoto. Uhusishwaji wa afya ya akili mashule utasaidia mtoto dhidi ya uonevu kutoka kwa wazazi, wanafunzi wenzake na walimu na jamii nzima, pia itaongeza kujiamii kwa mtoto hivyo kuongeza ufanisi wake kwa ujumla(5,6).
Uboreshaji wa afya ya mtoto unahusisha sekta mbalimbali, katika shule utatekelezwaji wake utakuwa katika namna mbili; ya kwanza ni kuwa na walimu walio wezeshwa, na kuwa na uwezo wa kuwajengea uwezo watoto na kutekelezwa kwa shughuli kama vile uhusishwaji wa mtoto katika jamaii, kujenga uwezo wa usuluhishaji madhubuti wa tatizo, kuwa raia muwajibikaji, kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuelewa na kutawala hisia mbalimbali binafsi na kutoka katika mazingira, kuepuka na kutawala msongo, namna ya kufanya mawasiliano ( effective communication), uboreshwaji wa mahusiano kati ya mwalimu na mwanafunzi yasiyo katika mtazamo wa woga bali heshima, pamoja na shughuli zote za kishule, michezo, burudani, na Sanaa mbalimbali zenye kuleta tija katika afya ya akili ya mtoto . Shughuli hizi hufanywa katika ujumla zitahusu kujenga jamii ya shule yenye heshima na uwezo wa kila mtoto katika kujiamini. (4)
Pili ni uwepo wa wanasaikolojia walio wezeshwa mashuleni (kwa maana ya kisela, nyenzo na maarifa). Kutokana na uhaba wa rasilimali watu na fedha Tanzania, uwepo wa kada wa afya ya akili (psychiatrist), mwanasaikolojia (psychologist), mnasihi (counsellor), mtu wa jamii (social worker), tiba ya kurudisha utendaji kazi (occupational therapy), mmoja katika eneo lenye ukubwa Fulani ( mfano; mtaa ) ambae ata hudumia shule kadhaa hivyo kupunguza gharama, Kwanza kabisa mtaalamu huyu atapima watoto kawa skeli maalum (screening scale), na kutambua uwezo wao na mapungufu yao, kisha kwakutumia maarifa ya kisaikolojia kuendeleza uwezo wa mtoto na kujaribu kusahihisha mapungufu yaliyo onekana
Kuhitimisha , rejea katika tafsiri ya shirika la afya duniani afya njema ni hali ya ukamilifu wa kimwili, kiakili na ustawi kijamii wala sio tu kutokuwepo kwa ugonjwa au udhaifu.
KUMBUKUMBU
1. Services P. Development of a Mental Health Policy and System in Tanzania : An Integrated Approach to Achieve Equity. 2010;61(10):10–3.
2. Mental Health ATLAS 2017 Member State Profile Tanzania , United Republic of. 2018;2016:2018.
3. Zhang M. M a s tering. 2014.
4. Fazel M. HHS Public Access. 2015;1(5):377–87.
5. Brown R. Mental health and wellbeing provision in schools October 2018. 2018;(October).
6. December HM. No Title. 2017.
6. December HM. Transforming Children and Young People’s Mental Health provision: a Green Paper. 2017.
ZINGATIA; maneno ya kiingereza yametumika kutokana na ugumu wa kuyatohoa nlio upata
MWISHO NA ASANTE

Upvote
6