Uijaribu kupeleka cheque CRDB

Maega

Senior Member
Joined
Jul 10, 2010
Posts
156
Reaction score
30
Nilikuwa nimezoea kupeleka cheque (ya Barclays) Exim ilikuwa inachukua siku 4 au 5, NBC likuwa inachukua siku 5 basi kwa vile pia nina akaunt CRDB nikasema niipeleke huko tangu tarehe 4/03/2013 hadi leo tarehe 14/03/2013 haijaiva. Nimewafuata benki wananiambia hakuna tatizo zitaingia tu ndani ya siku chache zijazo. Kibaya zaidi kipindi napeleka cheque waliniambia itakuwa tayari ndani ya siku 4. Najuta kuifaham CRDB, katu kwenye suala la cheque usishirikiane na CRDB utajuta
 
Naomba uni PM mkuu au piga huduma kwa wateja namba:
Please call +255(22)2 19 77 00, 0714 19 77 00, 0755 19 77 00, 0789 197700 or email customer-hotline@crdbbank.com
Ha ha ha ha ha!
Ebu tuaminishe mkuu,hivi ki kawaida itatakiwa cheque ikae muda gani iwe imeiva?maana nnampango wa kufungua account ya cheque hapo kwenu ili niweze kufanya biashara zangu vzr!
Please advise asap!
 
Mdau haujasema kama hyo cheque ni ya Crdb wenyewe au ni ya benki nyingine
Kama ni ya wao wenyewe crdb kuna tatizo hapo kwan hzo local cheque huwa same day zinaingia katika account.Kama ni za benki nyingine yaan mfano labda ya Nbc ukabank Crdb hizo zina span yake kuingia katika account na kawaida cku kumi ukitoa weekend dayz.
Kama una haraka kuna ktu kinaitwa special clearance hyo cku moja au mbili tayar ishaingia ktk akaunti na unatakiwa ulipie amt flan kwa ajil ya hyo special clearance
Hapo nadhan ni kule wahudumu kulack maelezo kwako na ww kutowaambia kama wataka hzo hela fast,
So tuambie hyo cheque ni ya aina gan then tutacomment
 
Ha ha ha ha ha!
Ebu tuaminishe mkuu,hivi ki kawaida itatakiwa cheque ikae muda gani iwe imeiva?maana nnampango wa kufungua account ya cheque hapo kwenu ili niweze kufanya biashara zangu vzr!
Please advise asap!

Kwa utaratibu wa DECH (Dar es Salaam Electronic Clearing House) kitengo cha BoT kinachosimamia ubadilishanaji na malipo ya cheki kwa mabenki sheria na utaratibu uko hivi:-

1 - kama cheue yako ni ya benki ya Dar itachukua siku nne za kazi (ondoa wekeend na sikuu)
2 - Kama cheki yako ni ya benki ambayo haiko Dar, itachukua siku saba
3 - Benki nyingi zinatoa siku moja kwa cheki za benki hiyo hiyo ambazo haziendi DECH
4 - Kuna kesi ambayo kama hiyo ni cheki ya benki ambayo haipo Dar na haiwakilishwi DECH huchukua muda mrefu zaidi.
Mfano, kama uko Mwanza na umelipwa cheki ya Citibank ambao hawako Clearing House ya Mwanza, itabidi cheki yako
iletwe DECH ambako Citibank inafanya clearance ya cheki zake. (hizi ndio huchukua muda mrefu kidogo) kitu kama 14 days.

Wakikamilisha mfumo wa cheque truncation, hapatakua na usumbufu wote huo kwa sababu vivuli vya cheki ndio vitakuwa vinatumwa clearing na cheki zenyewe kufuatia baadae, clearing itakua centralized Dar, za mikoani zitakufa.

Kisheria, kama cheki yako ikichukua zaidi ya siku hizo, hapo unahaki ya kulalamika na kutaka maelezo kwa benki husika.
 
Nimesema ni ya Barclays (in bracket) but kama ni siku 10 why siku zote hizo?????? mbona benk nyingine siku 4 tu! kama ndo utaratibu wao crdb cheque ya bank nyingine wajipange katika hili na hata hivyo kama yule niliyempa cheque angeniambia siku 10 badala ya siku 4 alivyonidanganya ningeipeleka kwa banker mwingine
 
Thank you kwa maelezo yako na kuniongezea uelewa wa haya mambo. Cheque yangu ni ya benk ya Morogoro japo hizo siku 7 zimekwishapita ukitoa weekend. Lakini nimekuwa nikifanya utaratibu wa cheque za benki hiyo hiyo ya Morogoro kwa kupitishia benki nyingine Exim na NBC na cheque zilikuwa zinachukua siku 4 hadi 5. Nafkiri crdb wajipange
 

Karibu mkuu, hapo kuna uzembe na nnadhani uzembe wenyewe uko hapa, wakishaipokea hiyo cheki hawaipost kwenye account yako moja kwa moja (Cheque sent for collection) wanairekodi kwenye register yao kisha wanaipeleka clearing wakisubiri ilipwe au irudi kwa sababu ya aina yeyote ile. Sasa kinachotokea ikishalipwa inabidi account yako iwe credited. sasa hapo inategemea umakini wa kukumbuka na mfumo uliopo wa kufuatilia cheki ambazo zimelipwa na zinatakiwa ziwekwe kwa wateja.

Na kama niko sahihi, huwezi kuiona hiyo entry kwenye statement yako siku unapodeposit hiyo cheki tofauti na cheki zilizolipwa na benki ambazo zipo Dar, unaiona hela ila inakuwa kwenye float.

Be blessed
 
Nimekuwa na experience mbaya mno na Crdb kwa kweli. Sishangai cheki kuchelewa kwani so far hakuna huduma Yao niliyowahi kuhitaji ikafanyika on time.
 
Nimekuwa na experience mbaya mno na Crdb kwa kweli. Sishangai cheki kuchelewa kwani so far hakuna huduma Yao niliyowahi kuhitaji ikafanyika on time.
Kwa hali hii nafikiria hata kuifunga tu hii akaunti yangu ya CRDB
 
mimi nilipeleka crdb tarehe 7/3/2013 nikaambiwa siku tatu za kazi lakini nilivyoenda tarehe 11/3/2013 nikaambiwa hela imeshaingia lakini hatuwezi kuitoa mpaka tarehe 14/3/2013 hapo ndio sikuelewa .....
 
Inaonekana kuna tatizo kubwa CRDB. Mimi nawadai hela yangu ambayo nilitaka kutoa kwenye ATM haikutoka nikajaza form na sasa zimepita siku 45 sijasikia chochote.
 
Nilishafunga account za CRDB, cause hawako makini na hata uwajibikaji kwao ni zero. Nilifika Dodoma nikadraw kwa ATM 200,000 hazikutoka nikangia ndani kwa benki wakaniambia niandike barua nilipofungulia account na nikafuata taratibu zao zote walizonielekeza, lakini leo huu ni mwaka wa nne sijawahi kuzipata hizo fedha na nikafunga rasmi account zote na kuhamishia EXIM. That guys are not serious!
 
mi nashangaawatu wanavyoteseka kwenye mabank makubwa,hizi benk hazina muda na wafanyabiashara wadogo,nawashauri mwende FNB-first national bank,ni benk mpya yenye huduma bora,jaribu kuwatembelea upate info zaid,matawi yapo posta opp serena;peninsula masaki na quality centre
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…