Kwa utaratibu wa DECH (Dar es Salaam Electronic Clearing House) kitengo cha BoT kinachosimamia ubadilishanaji na malipo ya cheki kwa mabenki sheria na utaratibu uko hivi:-
1 - kama cheue yako ni ya benki ya Dar itachukua siku nne za kazi (ondoa wekeend na sikuu)
2 - Kama cheki yako ni ya benki ambayo haiko Dar, itachukua siku saba
3 - Benki nyingi zinatoa siku moja kwa cheki za benki hiyo hiyo ambazo haziendi DECH
4 - Kuna kesi ambayo kama hiyo ni cheki ya benki ambayo haipo Dar na haiwakilishwi DECH huchukua muda mrefu zaidi.
Mfano, kama uko Mwanza na umelipwa cheki ya Citibank ambao hawako Clearing House ya Mwanza, itabidi cheki yako
iletwe DECH ambako Citibank inafanya clearance ya cheki zake. (hizi ndio huchukua muda mrefu kidogo) kitu kama 14 days.
Wakikamilisha mfumo wa cheque truncation, hapatakua na usumbufu wote huo kwa sababu vivuli vya cheki ndio vitakuwa vinatumwa clearing na cheki zenyewe kufuatia baadae, clearing itakua centralized Dar, za mikoani zitakufa.
Kisheria, kama cheki yako ikichukua zaidi ya siku hizo, hapo unahaki ya kulalamika na kutaka maelezo kwa benki husika.