Uingereza: Idadi ya watu wasioamini uwepo wa Mungu yazidi Wanaoamini, Utafiti Wabaini

Uingereza: Idadi ya watu wasioamini uwepo wa Mungu yazidi Wanaoamini, Utafiti Wabaini

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Queen’s, Belfast, umebaini kuwa nchini Uingereza, idadi ya watu wasioamini uwepo wa Mungu imezidi wale wanaoamini.

Matokeo haya yanatokana na utafiti wa miaka mitatu unaofanywa kimataifa ili kuchunguza sababu za kuongezeka kwa ukosefu wa imani. Karibu watu 25,000 kutoka Uingereza, Marekani, Brazil, China, Denmark na Japani walihojiwa, huku data pia zikikusanywa kutoka kwenye tafiti za British Social Attitudes Survey na World Values Survey.
1728630458902.png
Matokeo ya utafiti huo yamevunja dhana ya zamani kwamba watu wasioamini Mungu huishi maisha yasiyo na maana, maadili au malengo. Utafiti unaonyesha kuwa malezi ya wazazi ni mojawapo ya sababu kuu zinazochangia imani au ukosefu wa imani.

Chine McDonald, Mkurugenzi wa kituo cha kufikiri kuhusu dini, Theos, alieleza kuwa hali hii inaakisi miaka 50 ya kushamiri kwa maisha yasiyo ya kidini katika jamii, vyombo vya habari, na utamaduni.

McDonald pia alibainisha kuwa idadi kubwa ya wahamiaji wanaoingia Uingereza ni Wakristo, jambo linaloweza kuleta mabadiliko katika siku zijazo. Kwa mujibu wa utafiti huo, malezi ya wazazi yana nafasi kubwa katika kuunda imani za watoto. Hivyo, iwapo wazazi wengi katika siku zijazo wataendelea kumfundisha Mungu watoto wao, kutakuwa na ongezeko la watu wanaoamini Mungu nchini Uingereza.

===============

The UK now has more atheists than people who believe in God, according to new research by Queen’s University Belfast.

It has published the interim results of a three-year global project looking at why atheism has grown.

Nearly 25,000 people from across the UK, United States, Brazil, China, Denmark and Japan were questioned for the survey which also collated results from the British Social Attitudes Survey and World Values Survey.

The findings challenge the stereotype that atheists lead lives devoid of meaning, morality or purpose. It also suggests parental upbringing is a major factor influencing a belief in God.

Chine McDonald, director of religious think tank Theos, told Premier the findings reflect 50 years of widespread non-religion in society.

She said: "What this collation of the data is showing, is the consequence of around 50 years of a pervasive non-religion in our society, in our media and our culture; this idea that actually to believe in God is a weird thing.

“But I am interested in what the future holds because I think we'll see some changes in that. Recent research has found that over 50 per cent of immigrants to the UK are Christian and less than 20 per cent are Muslim. That is a significant proportion of people coming to this country who do believe in God.”

McDonald said this is significant because - according to the university's study - the biggest predictor of both atheism and theism is parental upbringing and parental attitudes towards God and belief.

She further noted: "So it would follow then that if you've got a significant proportion of society in the future believing in God and bringing up their children in their faith, then it's going to be a significant number of people who will believe in God."

“Christianity has good things to offer," she continued. "But I think what this new research shows is there is a significant number of people who just don't know or who don't have any kind of strong feelings. There are lots of people who just aren't religious because they have never encountered religion in the household that they grew up in.”

Professor Jonathan Lanman from Queen’s University Belfast said: “Our large cross-cultural surveys reveal that while many factors may influence one’s beliefs in small ways, the key factor is the extent to which one is socialised to be a theist.

“Many other popular theories, such as intelligence, emotional stoicism, broken homes, and rebelliousness, do not stand up to empirical scrutiny.”
 
Kwani hao wasioamini uwepo wa mungu wenyewe wanasemaje?
 
Kuna hadithi moja ya zamani kidogo kuna maneno ya malaika mtoa roho nayakumbuka mpaka leo. Alimwambia dada mmoja alipoenda kuchukua roho yake wakati wa mauti yake.

Dada aliuliza, nini kinafata? Akajibiwa "Unaenda kule ulipoamini, kama uliamini hakuna chochote basi utaenda kusipo na chochote"

Kwa mujibu wa simulizi hii kila mtu yupo sahihi kwa anachoamini, ile nafsi yako inachotengeneza ndicho kinachokuja kuwa, huyu aliamini hakuna chochote na ndicho kilichomsubiri baada ya mauti, wale walioamini kuna hukumu kweli walienda mbele ya hukumu, wale wa mabikira hivyo hivyo N.K.

EVERYONE IS RIGHT. KILA MTU NA MSALABA WAKE.
 
Shidai ipo hapa afrika, Mungu tunaowaamini waliletwa , Je Mungu wa waafrika aliyekuwo kabla ya wageni yaani wazungu na waarabu yuko wapi?
 
Shidai ipo hapa afrika, Mungu tunaowaamini waliletwa , Je Mungu wa waafrika aliyekuwo kabla ya wageni yaani wazungu na waarabu yuko wapi?
Waafrika kiasili hawajawahi kuwa na Mungu bali miungu; countless number of gods.
 
Back
Top Bottom