Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Serikali ya Uingereza imeanzisha mpango unaolenga kufuta kodi ya bidhaa mbalimbali zinazoingia nchini humo kutoka nchi maskini 65 duniani. viatu, nguo na baadhi ya matunda yasiyo zalishwa nchini humo ni miongoni mwa bidhaa zitakazo nufaika na mpango huo.
Mpango huu unaotarajiwa kuanza rasmi January, 2023 utaongeza idadi ya bidhaa zinazo ruhusiwa kuingizwa nchini humo pasipo kudaiwa tozo na utahusisha asilimia 99 ya bidhaa zote kutoka Afrika.
Kitengo kinachohusika na biashara ya ndani nchini humo kimeelezea hatua hii kama sehemu ya kuongeza mshikamano, kuondoa umaskini na kupunguza utegemezi wa misada kwenye nchi za Afrika.
Aidha, mpango huu utakuwa na nguvu ya kuondoa ushiriki wa nchi wanufaika ikiwa zitajiingiza kwenye mambo yanayovunja haki za binadamu pamoja na kushindwa kutimiza matakwa yatakayowekwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.
Mfano wa matunda yatakayo ingia nchini humo pasipo kutozwa kodi ni matango ambayo huadimika sana wakati wa majira ya baridi.
Chanzo: BBC