Kivyako-vyako, ah ah, kivyako-vyako, ah ah, kivyako-vyako
Ras Pompidou
Ajue Kiingereza, asijue, as long as hajanigongea hodi kunitwisha mzigo wake, na mie sijamgongea, ni poa tu.
Sasa kama mtu akikwambia hayo ndiyo maisha aliyochagua, na labda kipaji cha lugha hana, utamwambia nini?
After all lugha ni janga la taifa na Kiingereza chenyewe ni lugha fyongo kwa mtu aliyezoea lugha nadhifu kama Kiswahili (take it from George Bernard Shaw)
Sitetei u-Maimuna, nakataa kukubali hii "lording it over them" kama a genuine concern.
Kuna watu wanapenda kuwakoga wenzao tu, kwamba wamekaa Uingereza miaka yote lakini hawajui Kiingereza. Lakini katika kuwakoga hivyo wanataka tuamini kwamba wanasema hilo kwa noble reasons kama kukemea ujinga na kuwa genuinely concerned. Mbona hamtuambii mmewasaidiaje hawa "ndugu zetu" wasiojua Kiingereza?
Mie mtu anayekaa miaka yote hiyo Uingereza bila kujua Kiingereza nampa heko maana inaonekana ana skills fulani zinazo transcend lugha, ama sivyo angesha fungasha.
Halafu ananipa afueni sipati competition zaidi katika ubebaji makasha.