Uingereza na Tanzania hakuna tofauti

mavumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
596
Reaction score
328
Ni taratibu zinazofanana na kutofautiana kwa mazingira tu. Tofauti ni pale kwa wenzetu, kiongozi anapokubali kuyashindwa majukumu anajiuzulu. Wakati huku kwetu suala la kushindwa majukumu sio kigezo cha kujiuzulu.

Lakini utaratibu ndio huo, Uingereza Chama kinamshukia kiongozi hadi anajiuzulu maana kuwepo kwake kama kiongozi ni kwa ridhaa ya Chama chake.

Sasa huku kwetu Tz, Spika wa Bunge aliyechaguliwa na Wabunge anabinywa na Chama hadi anajiuzulu - ingawa ni wabunge ndio waliomchagua.

Na Kimsingi watu wachache ndio wanaoweka mbinyo huo kote kote, ndio maana lawama kwa Uingereza ni kuitisha uchaguzi mkuu.

Tunajifunza mengi ipo siku Jaji Mkuu Tanzania atajiuzulu kwa kushukiwa na Chama!
 
Sasa mbona unaonesha tofauti halafu title unasema hakuna tofauti?
 
Nimekosa Mimi,
Nisamehe Sana
Nisamehe Mimi,
Nimekosa jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…