Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameomba radhi kwa kushiriki katika sherehe ya kunywa pombe iliyofanyika katika bustani ya ofisi yake wakati nchi hiyo ilipokuwa chini ya vizuizi vikali vya watu kujumuika.
Hata hivyo, kiongozi huyo amepuuza miito ya upinzani ya kumtaka ajiuzulu, iliyomtaja kama mtu asiyeona aibu.
Johnson amesema aliuchukulia mkusanyiko huo wa watumishi wa ofisi yake kuwa wa kikazi, na kuongeza kuwa hivi sasa anajutia tukio hilo.
Johnson alikuwa akijibu maswali ya wabunge mchana wa leo mjini London, baada ya kusalia kimya kufuatia ufichuzi wa sherehe hiyo inayouweka mashakani uongozi wake.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour Keir Starmer amepuuza hatua hiyo ya Johnson ya kuomba msamaha, akisema imechelewa na haina maana, baada ya miezi ya udanganyifu na ulaghai.