Uingereza yakosolewa mpango wa kuhamishia wakimbizi Rwanda

Uingereza yakosolewa mpango wa kuhamishia wakimbizi Rwanda

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kagame.JPG
Serikali ya Uingereza imekosolewa maamuzi yake ya kutaka kuwahamisha wakimbizi kutoka nchini humo na kuwapelekea Rwanda ikioneana ni kama inafanya biashara ya kuuza watu.

Uingereza imeingia makubaliano na Rwanda kuhusu maamuzi hayo ambapo safari hiyo ya kilometa 6,000km itawahusu wote wanaoingia Uingereza kinyume cha sheria

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson yeyote ambaye aliingia nchini humo kinyume cha sheria kuanzia Januari mwaka huu anaweza kujumuisha katika safari hiyo.

Makundi ya Haki za Binadamu na Taasisi za wakimbizi wameita maambuzi hayo kuwa ni katili na siyo ubinadamu na ni kama ukoloni mambo leo.

“Inashangaza na sio ubinadamu,” anasema Steve Valdez-Symonds, Mkurugenzi wa Kambi ya Wakimbizi ya Amnesty International UK, anaongeza:

“Mpango huo hautapunguza idadi ya wakimbizi. Itasababisha kiasi kikubwa cha ukatili na kuchochea njia hatari zaidi za wakimbizi kuanzishwa.

Source: Aljazeera
 
Rwanda inahitaji wanasayansi sisi tumelala.
Marekani na Russia walichukua wanazi na wayahudi wakaendeleza sayansi ndo maana hawagusiki
 
Rwanda inataka kutanua nchi na huyu jamaa msipo shtuka mtaniambia
 
issue sio kuchukua Wakimbizi wala wahamiaji bali wana sifa zipi?

mbona sie tulibeba sana Warundi, wa Congo na Wanyarwanda kwa miaka mingi ?
Rwanda inahitaji wanasayansi sisi tumelala.
Marekani na Russia walichukua wanazi na wayahudi wakaendeleza sayansi ndo maana hawagusiki
 
Mimi nadhani itasaidia sana kupunguza kasi ya wakimbizi kwenye nchi za uchumi mkubwa. Yaani mtu akifikiria kuwa akikimbilia UK atapelekwa Africa(Rwanda)
 
Mimi nadhani itasaidia sana kupunguza kasi ya wakimbizi kwenye nchi za uchumi mkubwa. Yaani mtu akifikiria kuwa akikimbilia UK atapelekwa Africa(Rwanda)
Rwanda analipwa kwa kichwa akipata watu wengi na pesa inakua nyingi so ILI- MRADI UWE ENDELEVU unafanyaje?
 
kwa kuwa rwanda in raia wachache acha tu waongezewe watu ili wachangamane waachane na ukabila huu ni mpango mahususi sababu hawa jamaa wana ukabila sana sasa wakichangamana na watu wengine ukabila utaondoka pole pole good aidear
 
Rwanda inataka kutanua nchi na huyu jamaa msipo shtuka mtaniambia
Mie nimemshtukia toka kitambo alipotaka kugusa sharubu za Mzee wa Msoga Na Mzee wa Chato haka kajamaa akili zake hazina muelekeo Mkakati huo
 
Back
Top Bottom