Serikali ya Uingereza imekosolewa maamuzi yake ya kutaka kuwahamisha wakimbizi kutoka nchini humo na kuwapelekea Rwanda ikioneana ni kama inafanya biashara ya kuuza watu.
Uingereza imeingia makubaliano na Rwanda kuhusu maamuzi hayo ambapo safari hiyo ya kilometa 6,000km itawahusu wote wanaoingia Uingereza kinyume cha sheria
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson yeyote ambaye aliingia nchini humo kinyume cha sheria kuanzia Januari mwaka huu anaweza kujumuisha katika safari hiyo.
Makundi ya Haki za Binadamu na Taasisi za wakimbizi wameita maambuzi hayo kuwa ni katili na siyo ubinadamu na ni kama ukoloni mambo leo.
“Inashangaza na sio ubinadamu,” anasema Steve Valdez-Symonds, Mkurugenzi wa Kambi ya Wakimbizi ya Amnesty International UK, anaongeza:
“Mpango huo hautapunguza idadi ya wakimbizi. Itasababisha kiasi kikubwa cha ukatili na kuchochea njia hatari zaidi za wakimbizi kuanzishwa.
Source: Aljazeera