Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Kwa siku kadhaa nimekuwa nikisoma Kitabu cha Ujamaa cha Julius Nyerere, na ni mengi ninajifunza tena na kubaini kuwa Mwalimu aliandika vision ya kutujenga kama Taifa hata kabla ya Azimio la Arusha.
Ni rahisi sana kwa wasiopenda kusoma na kutafakari kuamini kuwa Ujamaa(mfumo wa wzalishaji) ndio uliangusha Uchumi wa Tanzania na kuulundika kwenye fungu moja la Ujamaa (mfumo wa maisha) ambaondio chimbuko la Nyerere kuandika kitabu chake nakuwa muumini wa Ujamaa wa kiafrika ili kujenga mfumo na uchumi wa ujamaa na kujitegemea.
Kilichonisisimua zaidi ni sehemu ya Elimu ya Kujitegemea http://hakielimu.org/files/publications/document169Elimu_Kujitegemea.pdf
Nyerere alipoandika hili mwaka 1967, alidhamiria kuwepo kwa mfumo wa elimu ambao ulikuwa una manufaa kwa kila Mtanzania.
Nikipima hali halisi ya Ujinga na Umasikini wa leo Tanzania, najikuta najiuliza ilikuwaje tulishindwa kujenga mfumo wa elimu na ufahamu ulio madhubuti kuleta maendeleo na kujizatiti kama Taifa linalojitegemea?
Mapungufu makubwa tunayoyaona leo katika soko la ajira, ubwanyenye na unyapara wa waajiriwa, kuongezeka wa uduni na ujima katika uzalishaji unaniambia wazi kuwa kuna mahali tulipotea na kuachana na vision ya taifa iliyoandikwa na Rais wetu.
Ningependa sana kwa kila mmoja wetu kuchukua muda na kutumia fursa ya kusoma Elimu ya Kujitegemea na kisha tuje tujadiliane tulikotoka, tulipo na tunapoenda.
Kuna mengi sana ya kujifunza na hata kuunda mitaala kuanzia shule za chekechea mpaka vyuoni kuhakikisha mfumo wetu wa elimu unadhamiria kujenga watu wenye ufahamu na dhamira za kujitegemea na kuwa wenye umahiri wa uzalishaji mali.
Maendeleo yetu hayatatokana na idadi ya wahitimu vyuoni pekee, bali kuuelewa mfumo wa Elimu na Ufahamu ambao unaendana na mazingira yetu.