Habari wadau.
Ukweli wabongo ni Watu wanaojua sana kucheza na fursa.
Wamegundua wanawake wengi sana wanatafuta wachumba wa kuwaoa. Hivyo wajanja wameanzisha page instagram za kuunganishiwa mwenza kwa malipo kiasi kazaa. Na page hizo zinakiwa zinatoa ushauri wa mambo ya mahusiano ili kuvutia followers wajae.
Mbinu wanayofanya.
Kwanza Kwenye page zao wanapost details za mwanaume mwenye kazi nzuri akijifanya anatafuta mchumba wa kike wa kuoa.
Huyo mwanaume anakuwa ni fictional character tu hayupo kiuhalisia. Ila kunakuwa na wanaume kazaa wanaojuana na mwenye dating page kwa ajili ya kujifanya wao ndio huyo mwanaume hewa aliyepostiwa.
Wadada wengi walio single wakiona sifa za huyo mwanaume anaetafuta mchumba wanaenda inbox wakiomba wanganishwe nae. Huko inbox wanaambiwa kuunganishwa ni lazima watoe hela 20,000 ama 30,000 kuonesha wapo serious.
Wakishalipa hizo hela wadada hao wanapewa namba ya mwanaume ambaye ameshapangwa tayari na mwenye dating page. Kwamba wazuge zuge hawa wadada kwa kuwachatisha tu. Na kuwatumia picha hata za uongo. Ili wadada waone hela waliyolipia imefanya kazi. Ila baada ya siku kazaa jamaa akate mawasiliano ama anajifanya amesafiri.
Hivyo wanakuwa wanapiga hela za wadada wanaotafuta wachumba kila siku.
Unakuta per day wenye hizo page wanatengeneza hadi laki 5 kwa urahisi tu.
Nimelijua hilo baada ya kupewa story na boda boda mmoja Ambae ni mmojawapo ya hao wanaume wanaotumika kuwachatisha wanawake waliolipishwa fedha huko instagram kwenye page za kuunganishiwa wachumba.
Unakuta mdada meneja wa bank ana masters ila anachatishwa na muhuni tu dalali wa vyumba anaejua kiingereza. Dada anajiona amepata mume anasubiria kuonana nae. Huku kashaliwa elfu 30 yake na mwenye page