Ujanja mpya umeibuka wa kutapeli wanawake hela kwa kutumia dating page za Instagram

Bora hiyo, ipo hii ya wazungu, wachina kuwaibia wadada wanaofanya kazi bank taarifa za siri za kibenki, yaani anakuja bank na kutoa/kuweka hela na unakuta ana mpunga mrefu bank, mara ya kwanza ya pili etc, baada ya hapo mdada anajiona kapata, then siku ya siku mzungu anamuomba wakutane wakalane hotel, unakuta ni muda wa kazi akitoka waonane (kinacholengwa hapo ni laptop/simu zenye taarifa za bank anayofanyia kazi), basi wanaenda hotel nzuri tu nyota tano. Wakifika mzungu hatoi kitambulisho na mdada kwa sababu anajiona kapata mzungu nasi anasema mume wangu hahahah, wanaenda chumbani baada mida kama saa tano au sita au midnight Mzungu anatoka anasema kapata dharula mke wake kampigia au kisingizio chochote anatoka hotelini na credentials za mdada zoteeee, asubuhi hana kila kitu, hii imepelekea bank nyingi kuibiwa hela mno mno, sasa sijui bank wanaujua huu utapeli. Kwa hiyo unakuta mwizi siyo mfanyakazi wa bank ila particular zake zimetumina. Hata kwa vijana the same. Wadada wamelizwa sana tena sana. Dating ni social, kutana na watu utapta mke/mume.
 
Wadada hao hao njiani wana ringa afu kwa keyboard wana tafuta mchumba
 
Mimi sina maana nimepewa story tu.

Ukitaka namba nenda katembelee page za wachumba instagram utapewa namba. Ila ujiandae kulipishwa hela.
Dah basi itabidi hao wadada waje huku jamiiforum maana huduma za kuunganishwa ni Bure Sina insta mkuu ila Waite waje huku
 
Desperation ya wanawake wanaotaka kuolewa ndiyo inawaweka mjini hawa watu
 
Hivi kwanini Elimu isifutwe?
Huwa naumia sana ninapoona mtu mwenye elimu angalau kuanzia kidato cha nne anatapeliwa mtandaoni
 
Wanawake wanaamini watu haraka sana hapo ndo ilipo shida yao kubwa, miaka miwili iliopita nilizoeana na dada mmoja yuko huko nchi za Gulf nilijuana nae kupitia instagram akaanza kujichangaya bila hata kumset ni basi tu sometimes imani ya Mungu inatuweka mbali na dhulma kwa kuhofia.
Ila nilimueleza kuwa usiamini watu haraka
 
Ukiwa muongeaji na uko active mtandaoni, akikucheki ushajibu kila siku unamcheki, hawazi kua huyu kijana ni jobless ndo maana ana muda wa kuchezea ila anachowaza ni kua wewe umefall kwake na unampenda kwelikweli.
 
"Nimelijua hilo baada ya kupewa story na boda boda mmoja Ambae ni mmojawapo ya hao wanaume wanaotumika kuwachatisha wanawake"


Ha ha ha hii kiboko usikute na bida wangu nae ni miongoni Kwa vijana wa huko😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…