Ujasiri huu wa Watanzania kwa wazungu umepotelea wapi?

Ujasiri huu wa Watanzania kwa wazungu umepotelea wapi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Henry Kissinger, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kaja Tanzania kupatana na Rais Nyerere kuhusu jambo. Alikutana na mabango mengi. Leo hii leo hii leo hii mzungu kutoka Marekani mwenye cheo hiki akija tena Tanzania ole wake atakaenyanyua bago, ujasiri wetu umeenda wapi?

Ujasiri umeyeyushwa na misaada ya mabilioni ya fedha za miradi zinazoishia kwa wachache.

kiongozi jukumu lake ni uwajibikaji, akishaelemea kwenye maslahi kazi inakuwa ni kujinufaisha yeye.
 
Kama mnakataza hata wanavyuo wasijadili mambo ya nchi mkisema hiyo ni siasa. Unategemea huo ujasiri wa kuhoji utaupata wapi?
 
Kama mnakataza hata wanavyuo wasijadili mambo ya nchi mkisema hiyo ni siasa. Unategemea huo ujasiri wa kuhoji utaupata wapi?
hao wanavyuo nao ni mazuzu na walimu wao, haki ni haki tu ilimradi huvunji sheria, ichukue kwa nguvu kama una uhakika 100% kuwa ni haki yako..
 
hao wanavyuo nao ni mazuzu na walimu wao, haki ni haki tu ilimradi huvunji sheria, ichukue kwa nguvu kama una uhakika 100% kuwa ni haki yako..
Unazungumzia haki ipi ikiwa wanaostahili kupata mikopo hawapati ?? Haki ipi unayoimba hapa ikiwa wanaomaliza vyuo hawapati kazi? Watu wanaporwa pesa kwa sheria mbovu na kisha wanateuliwa kwa nafasi za juu zaidi???
 
baada ya kuona hivyo wewe umefanya nini? unaingia uvunguni mwa kitanda chako na kuanza kulia na kunung'unika? Siku hizi Mwanafunzi wa chuo kikuu anawaza na kufanya kama mwanafunzi wa kidato cha nne wa miaka ile. Wakati ule hata shule za sekondari haki zilikuwa zinadaiwa na zinapatikana. Ajira!!! anza kwa kujitolea (volunteering) bila malipo ili uchote ujuzi na uzoefu kisha tafuta ajira au jiajili mwenyewe. Unapofanyakazi kwa kujitolea fanyakazi kwa usahihi wa hali ya juu, juhudi na maarifa ili kumshawishi mwajili.
 
Back
Top Bottom