Ujasiri wa Hajjat Amina Said?

Ujasiri wa Hajjat Amina Said?

hata hu ujasiri hana maana alifungia vituo vya mafuta wakagoma na hawakufunga wakanedelea kufanya kazi kama kawa na akawa mpole...hamna lolote ni kubebana tuu

Ochu,
Huyo avatar wako anakunywa nini?mbona hamalizi....
 
Amehamishwa sana huyu kwa miaka hii minne. Au ndio utendaji uliotukuka anahitajika kila mahali?
 
Amehamishwa sana huyu kwa miaka hii minne. Au ndio utendaji uliotukuka anahitajika kila mahali?

Alikuwa karani wa statistical library,akachaguliwa kuwa DC Bukoba,wakati watu wanajiandaa kumfanyia party ya kumkaribisha akateuliwa kuwa RC Iringa..imagine that..a promotion in under a month
 
kimsingi kama ndivyo alivyo; hafai kuwa Mbunge wa kawaida. Anatakiwa kuwa mbuneg wa kuteuliwa halafu anapewa uwaziri wa kusimamia matokeo.. we need results oriented leadership..

Huyu mama namjua vizuri, kabla ya pwani alikuwa Iringa, hafai kabisa kuwa waziri, maamuzi yake ni ya mlipuko with no thinking. alitusumbua sana alivyohama tulishangilia.
 
Huyu mama namjua vizuri, kabla ya pwani alikuwa Iringa, hafai kabisa kuwa waziri, maamuzi yake ni ya mlipuko with no thinking. alitusumbua sana alivyohama tulishangilia.

aliwasumbua vipi mkuu Remmy ... hebu nyanyambua kidogo tafadhali!
 
Alikuwa karani wa statistical library,akachaguliwa kuwa DC Bukoba,wakati watu wanajiandaa kumfanyia party ya kumkaribisha akateuliwa kuwa RC Iringa..imagine that..a promotion in under a month

ndo maana tunataka ku-connect dots ... why all these guts just a sudden??
 
anajiamini...ni shangazi yake mkulu

waweza thibisha hili mkuu ... possibly ni name coincidence ... sababu humu humu watu walimuhusisha Hawa Ghasia na Mama Salma ... ikapingwa vikali sana!
 
Huyu mama namjua vizuri, kabla ya pwani alikuwa Iringa, hafai kabisa kuwa waziri, maamuzi yake ni ya mlipuko with no thinking. alitusumbua sana alivyohama tulishangilia.
utawajua tu watendaji wetu!!
 
napat kigugumizi kumsifia huyu Mama kwani alikuwapo Iringa na madudu mengi yalifanyika mbele ya macho yake likiwa la ukarabati feki wa Barabara za Mji wa Iringa wakati wa uongozi wake; sasa sijui hii ni kujifagilia kuelekea ubunge?
 
JF kwa double standards,

Angekua Magufuli amefanya the same, kungekua na nderemo za kumsifia na pengine watu kumtaka agombee urais.

Lakini kwa vile ni mwanamama, na halafu hajjat, watu wanashindwa kukubali kilicho dhahiri.

Huyu mama nakubali ni kero kwa watendaji wa Halmashauri. Tena ni kero kubwa sana!... Sababu kuu ni kuwa yeye kila anapoenda anaziba mianya ya utafunaji hela za wananchi kwa visingizio visvyo na tija. Ziara za watendaji za "mazoea" zisizo na results anabana, tena anabana haswa.

Amekua mkali kwenye utoaji wa zabuni mbalimbali kwa kutaka uwazi zaidi, na ushiriki mpana zaidi wa wakandarasi ili kuongeza ushindani. Maana watendaji huwa wamegawana wakandarasi utandhani ofisi za umma ni vioski vyao binafsi, na wakandarasi huwa wanajirudia haohao hata wakiharibu kazi watatafutiwa excuses za kuharibu.

Kuthibitisha, miezi miwili nyuma chama cha wakandarasi wa mkoa wa Iringa(alipokuwepo kabla ya kuja Pwani) walimtunukia nishani ya uongozi bora kwa kufanikiwa kupunguza rushwa kwa kiwango cha juu kwenye utoaji wa kandarasi za miradi ya barabara za mkoani. Tukio hili lilitokea kwenye TV station zote kubwa.

Sasa kama mama anakubaliwa na wananchi na vyama huru vya wafanya biashara kwa uongozi bora, unategemea watendaji wetu hawa tuliowazoea maserikalini watampenda au kumsifia kwa lolote???....Tia akili.
 
JF kwa double standards,

Angekua Magufuli amefanya the same, kungekua na nderemo za kumsifia na pengine watu kumtaka agombee urais.

Lakini kwa vile ni mwanamama, na halafu hajjat, watu wanashindwa kukubali kilicho dhahiri.

.

Hivi JF ni nani? Wewe haumo?

Na hizo conspiracy theory za u-hajjat sijui mwanamke, mdini mkubwa wewe. Kila kitu unakichukulia ktk muonekano wa kidini. Very hopeless.

Hivi ni sheria gani hiyo ya kukata mshahara watu? Yaani unataka tumpongeze kwa kuleta kauli tata ambazo hazina mashiko ya kisheria?
 
anajiamini...ni shangazi yake mkulu

Sio kweli ,lakini inawezekana ana ukaribu na mkewe Mkulu ; alipokuwa mkuu wa mkoa wa Iringa hukufikia utendaji wa yule mama aliyemtangulia as a result wakati wa ziara ya Mkulu hapo Iringa , mama wa watu akapata pressure ikabidi alazwe hospitali wakati wote Mkulu alipokuwa ziarani!! Matokeo yake Salma akaenda Iringa na muda si muda akahamishiwa Pwani ambako ndiko anakofanya hivyo vityuko sasa.Talk about nepotism, there it is in action.
 
Ma RC na DC Lini walipokonywa nguvu za kuwaweka ndani raia wa TZ anaposikia mbona kumbu zangu hafifu seuze kukata mshahara ambao ni kiduchu hata YENU BAR haukeshi ???
 
Tunapozungumzia ujasiri wa watu au utendaji wao mbaya au mwema si vema tukahusianisha mambo haya na dini au kabila zao kwani kama ni ufisadi hauna dini wala ukabila. Sasa haya mambo ya kusema kwa kuwa ni hajjat au nani yanatoka wapi? yule mama ni mtendaji kweli kama baadhi wanavyosema hapa, na pia kwa kuwa kila mtu ana upande wa pili wa shilingi basi nao si jambo baya wanapotutanabaisha. Tuendelee na mjadala
 
Kukata mtu mshahara sio kinyume cha sheria?

nanai aliyekuambia watakatwa mshahara??............... hakuna atakayekatwa hapo, hata JK hawezi kuthubutu kukata mshaara wa mtu............... zile ni kauli za kisiasa tu, zilikuwa za kufurahisha hadhiza............... na ni za kupuuuzwa......................
 
Anae mpongeza huyu mama ana matatizo pia.Mama huyu (Mkuu wa mkoa) amevunja taratibu, kanuni na sheria za kazi. Tukumbuke Lowasa akiwa waziri mkuu aliwahi kumfukuza kazi mkurugenzi mmoja wa wilaya kwa kuchelewa kutumia fedha (sababu sawa na za huyu tu) lakini yule mama alikuwa na sababu za kisheria (Zabuni ni lazima itimize siku 28 kwenye serikali za mitaa). Hatujui kwa nini kisarawe walikaa na hizo fedha lakini masuala ya ujenzi yana mchakato mrefu sana kuanzia kuandaa mchoro wa majengo, bill of quantities n.k hivyo kumwadhibu mtumishi kuwa mzembe wakati hujui kazi yake inatumia muda gani kukamilika ni kosa. Sijampa sifa wala kuona utendaji katika hilo. Nawatetea watumishi wa Kisarawe na hasa mhandisi wa ujenzi.
 
kama kuna Machache ya Kuwasimamia Watendaji wa Chini yanafanyiwa kazi ni kazi ya Kupongezwa na kuhimizwa kwani ndivyo vitu wadau tunahitaji...!!!

Kazi za DC/RC nafikiri si pekee za kuamuru kamata huyu au yule..au kuleta FFU!!!ni kazi ambazo hata Mkuu wa Polisi wa Wilaya/Mkoa anaweza zifanya.

kama itakuwa DC/RC hana Power ya Kuwasimamia watendaji basi hakuna maana ya uwepo wa DC/RC...

the so called Hazina...ni wapitisha mishahara...waajiri ni Utumishi...!!! ni Mgawanyo wa Kazi...

Otherwise Wadau mtuletee amevunja vipengele gani vya Sheria....!!!
na Pia mtuwekee Boundaries za Utendaji kazi wake....!!! kuna statement DC/RC anasimama nafasi ya Rais ktk Wilaya/Mkoa husika...!!!...

Tunapenda double standard....!!! Wengi humu ndani tulipenda au tunapenda Rais awachukulie hatua Mafisadi...tena bila kupitia Mahakama or any procedural zilizopo...!!! Leo hii viduchu vya kuwashtua watendaji wetu Waamke....basi DC/RC amekosea....!!! Kweli tunakazi ndefu....!!!
 
Back
Top Bottom