JF kwa double standards,
Angekua Magufuli amefanya the same, kungekua na nderemo za kumsifia na pengine watu kumtaka agombee urais.
Lakini kwa vile ni mwanamama, na halafu hajjat, watu wanashindwa kukubali kilicho dhahiri.
Huyu mama nakubali ni kero kwa watendaji wa Halmashauri. Tena ni kero kubwa sana!... Sababu kuu ni kuwa yeye kila anapoenda anaziba mianya ya utafunaji hela za wananchi kwa visingizio visvyo na tija. Ziara za watendaji za "mazoea" zisizo na results anabana, tena anabana haswa.
Amekua mkali kwenye utoaji wa zabuni mbalimbali kwa kutaka uwazi zaidi, na ushiriki mpana zaidi wa wakandarasi ili kuongeza ushindani. Maana watendaji huwa wamegawana wakandarasi utandhani ofisi za umma ni vioski vyao binafsi, na wakandarasi huwa wanajirudia haohao hata wakiharibu kazi watatafutiwa excuses za kuharibu.
Kuthibitisha, miezi miwili nyuma chama cha wakandarasi wa mkoa wa Iringa(alipokuwepo kabla ya kuja Pwani) walimtunukia nishani ya uongozi bora kwa kufanikiwa kupunguza rushwa kwa kiwango cha juu kwenye utoaji wa kandarasi za miradi ya barabara za mkoani. Tukio hili lilitokea kwenye TV station zote kubwa.
Sasa kama mama anakubaliwa na wananchi na vyama huru vya wafanya biashara kwa uongozi bora, unategemea watendaji wetu hawa tuliowazoea maserikalini watampenda au kumsifia kwa lolote???....Tia akili.