Ujasiri wa Rais Magufuli juu ya janga la korona katika ulimwengu wa roho

Mkuu naomba kwa lugha rahisi kabisa elezea ni kwa namna gani ugonjwa wa Corona ni vita ya kiuchumi kwa Tanzania wakati huo ugonjwa upo Duniani kote?
Akielezea na mm unitag mkuu, hii sentesi sijawai ielewa"
 
Toa upuuzi wako hapa. Anaposema matambara ya kuziba pua hayatusaidii anamaanisha nini kama si kuziponda barakoa?
Barakoa za kutoka nje si salama uchunguzi ulifanywa lini na nani? Na zinatoka nchi gani ambayo inatuletea Watanzania barakoa ambazo si salama ili tufe?
Acha kusambaza ujuha wako ambao unaweza kabisa kuongeza kusambaa kwa maambukizi.

 
Naam ndivyo unavyoona wewe!..
Naomba nikuulize na wewe....hivi barakoa za hapa Nchini zinazozaliswa na MSD unazichukulia kama nini?...
Jaribu kuangalia nyuma ya kila kitu Mkuu utaona kila kitu kwa sababu alishauri za kujishonea napo alitoa sababu.....
Usijenge hoja ukiwa umeizima akili yako upande mmoja na kuwasha upande mwingine.
 
Mkuu naomba kwa lugha rahisi kabisa elezea ni kwa namna gani ugonjwa wa Corona ni vita ya kiuchumi kwa Tanzania wakati huo ugonjwa upo Duniani kote?
Ni ugonjwa pekee unaowafanya watu wengi usijishughulishe na uzalishaji mali kwa wakati mmoja.
Tafiti zinaonesha uchumi wa Nchi nyingi Duniani umeyumba kutokana na ugonjwa huu ndani ya muda MFUPI ukilinganisha na magonjwa mengine.(nieleweke kuwa ninaafiki kuwa magonjwa mengi hudhohofisha uchumi lakini kasi hutofautiana kasi ya COVID-19 kudhohofisha uchumi ni kubwa ukilinganisha na maradhi mengine.)
Gharama za matibabu na vifaa tiba, idadi ya wagonjwa na msambao wake ni tishio la uchumi.
Inaendelea.
 
Sawa kabisa, maana Mungu naye ni Roho na anaabudiwa rohoni, si mahali fulani panapoonekana kwa macho. Ukiwa macho rohoni na kumtegemea Mungu, vitu vya mwilini au vinavyoonekana havina nguvu kabisa, kwa kuwa Mungu aliye ndani yetu (rohoni), ana mamlaka na nguvu zote kuliko yeyote, awe rohoni au nje ya roho! Kongole kwa kufunuliwa hiyo siri kubwa na ya kweli!
 

Akielezea na mm unitag mkuu, hii sentesi sijawai ielewa"
Nimeshaeleza na ninaendelea Mkuu fuatilia thread ila tambua wewe ni kiumbe wa kiroho anayeishi ndani ya mwili.
Usikubali mipaka ya muda na mahali inayoudhibiti mwili ikudhibiti na wewe.
 
Yaani bongo kuna wajuaji balaa,Leo corona umekua ugonjwa wa kiroho Mara brah brah nyiiiiingi,nyie ndo mlikua watetezi wa babu wa loliondo enzi zile et ukinywa kikombe uwe na imani ndo utapona,upuuzi tu kwendraaa zenu,watu kama nyie ndo mfano wa yule nabii aliechoma watu kanisani kwake Uganda kwa kuaminisha watu ujinga
Et mwaka 2000 ni mwisho wa dunia kiimani wakati kisayansi ni New millennium haaaahaaaahaaa!
 
Unataka kukataa uhalisia wako Mkuu.
Je wewe siyo kiumbe wa kiroho?....
 
Mlaki umeeleza vizuri lakini umekosa muunganisho kati ya mwili na roho. Roho ni formless na timeless lakini Kuna kanuni zinazoongoza mwili (physical body )magonjwa ya kuambukiza yanahitaji tiba. Ndio hivyo hamna ubishi, usifungwe na mtazamo binafsi na kuelezea Ulimwengu mwingine in order to justify what you believe with your mind which also part of your physical dimension .
 
Naam nakuunga mkono ila kumbuka kinachouongoza mwili ni kitu kisichoonekana " formless and timeless" na baadhi ya wanafalsafa wanakipa sifa ya eternity(umilele) na omnipresent (uwepo kila mahali).
Ulimwengu wa roho unatawala ulimwengu wa mwili kwa maana hiyo mwili ni receptive tool tu ya masuala yanyotokea kwenye ulimwengu wa roho.
Taratibu tu itaeleweka vizuri.
 
Roho (spirit) ndiye mtu halisi (real human being), imevaa nafsi (soul) na mwili (flesh). Uwepo wako wa ndani kabisa ndiyo roho yako. Nafsi ina utashi ambako kuna akili, hisia na maamuzi

1 Wathesalonike 5:23
 
Jibu swali acha kuruka kuruka! Barakoa zisizo salama zimetoka nchi gani na ni nani na lini aliyegundua si salama? Nchi nyingi za Afrika zinapata barakoa toka nje mbona hatujasikia hata moja ya nchi za Africa ikilalama kuhusu huu upuuzi wa barakoa zisizo salama?
 
Mkuu umeeleza generally jinsi ugonjwa wa corona unavyoathiri uchumi wa nchi zote which I agree with you. Naomba sasa unieleweshe ni kwa namna gani ugonjwa wa corona ni vita ya Kiuchumi kwa Tanzania. Tunapigana wa watu gani ikiwa nchi zote zina tatizo la Corona?
 
Roho (spirit) ndiye mtu halisi (real human being), imevaa nafsi (soul) na mwili (flesh). Uwepo wako wa ndani kabisa ndiyo roho yako. Nafsi ina utashi ambako kuna akili, hisia na maamuzi

1 Wathesalonike 5:23
Naam...nakubaliana na maelezo haya bila shaka kabisa.
Kinachokufanya wengi tukwame kilishawahi kuelezwa kuwa "Kuna vita kati ya mwili na roho" ....roho inaweza kuwa tayari kwa lolote lakini mwili ukakataa.
Kwa jinsi ya mwili ni vigumu sana kuelekea hapa ila kutafakari kwa kina umbali siyo vikwazo tunaona, tunawasiliana na tunaelewana.
Hakuna mpaka wala muda katika ulimwengu wa roho.
Katika ulimwengu wa roho ndipo ulipo uumbaji wote na ugunduzi wote uliuowahikufanyika ambao hakijafanyika na utakaofanyika.
Ulimwengu wa roho una sifa ya kutokuwa na ukomo na pia umilele.
.......nothing to fear.....
 
Naam!
 
Mkuu siyo lazima kile anachofanya jirani yako na wewe ufanye...kumbuka kila mmoja ameumbiwa kusudi lake na anapaswa kulitekeleza.
Halikadhalika mataifa yote unayoyaona Duniani yana kusudi la uwepo wake hayapo hivihivi tu..." there must be a purpose"..
Tanzania ina kusudi la uwepo wake hakuna kinachofanyika kwa bahati mbaya katika ulimwengu wa roho...ni suala la kuwa tayari kusikiliza sauti ya ndani.
 
Tunapigana na watu wenye nia ovu dhidi ya uchumi wa Dunia ikiwemo Tanzania katika ulimwengu wa roho.
 
Mkuu unanishangaza sana kukataa ukweli unapoishi kila uchao.
"Everything owe its origin from formless to form"...hata Serikali unazozitaja mwanzo wake ni katika ulimwengu wa roho.
Elewa usipaparike Kaka...Ulimwengu wa roho siyo Dini au imani fulani ila ni mwanzo halisi wa kila kitu unachokifahamu na usichokifahamu.
Usipinge jambo kwa sababu tu milango mitano ya fahamu hailielewi ....mwanadamu ana uwezo wa kuvuka mipaka ya milango ya fahamu na kuelewa vitu ambavyo ni vigumu kuelezea kwa kutumia milango hiyo.
........usiogope.....
Wewe ni kiumbe wa kiroho ndani ya mwili usitawaliwe sana na mipaka ya mwili wako.
 
Vipi Kuhusu Ule ulinzi wake Wa Mitutu ya Bunduki na Hellicopter, kwenye ulimwengu wa Kiroho mnaitaje aina hiyo ya Ulinzi.?
Mungu asipoulinda mji waulindao wafanya kazi bure.
"Ulinzi unaanza na ule wa kiroho huo tunaouona wa mitutu na bunduki ni taswira tu ya ulinzi halisi".
Kwa kifupi tunalindwa na sana katika ulimwengu wa roho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…