Ujasiri wa Rais Magufuli juu ya janga la korona katika ulimwengu wa roho

Tunaongea sayansi hapa acha kuleta mifano yako isiyo na kichwa wala miguu. Sayansi ya kupambana na Covid-19 Marekani ndiyo hiyo hiyo ya kupambana na COVID Tanzania au nchi nyingine yoyote ile.

Ulimwengu wako wa roho kaa nao mwenyewe hausaidii chochote kwenye kupunguza maambukizi au vifo vinavyosababishwa na corona.
 
 
 
Iyo vita ya kiuchumi tupigwa sisi tu?
 
Hatuwezi kuiona roho kwa macho kwa kuwa si mwili. Je, tumewahi kuuona upepo kwa macho? Hata kama hatujawahi kuuona lakini sauti yake, nguvu yake na matokeo au madhara yake, tunayasikia na kuyaona kwa hakika.

Kwahiyo, uwepo wa kitu fulani si lazima tukione kwa macho. Hata sauti hatujawahi kuziona lakini tunazitoa na kuzisikia kwa hakika! Umeme upo, tunauzalisha na kutoa nishati tunayoitumia sana, lakini umeme hauonekani kwa macho!

Vivyo hivyo roho yako ndiyo wewe mwenyewe. Mwili ni koti tu lililoivaa roho kama waya unavyokuwa na umeme. Waya bila umeme hauna nguvu yoyote, kama ambavyo mwili bila roho ni bure kabisa. Nguvu halisi iko rohoni.

Roho ikitoka tunakuwa tumekufa. Na mwili ukiharibika, roho hutoka pia. Aidha, kila mtu ana sehemu tatu kwa pamoja: mwili (flesh), nafsi (soul) ambayo hujumuisha akili (mind), hisia (emotions) na maamuzi (decisions), na kisha roho (spirit or heart). Nafsi hubeba utashi (conscience) ambao wanao watu tu, si wanyama.

Tunafanya jambo lolote kwa utashi wetu, kwa maamuzi yetu na mitazamo au mapenzi yetu. Tunu hiyo haipo kwa wanyama. Hata mnyama anapokunya hafikirii chochote - kunya kunamtokea tu "puuh" popote alipo!

Je, umewahi kutokewa ambapo unabishana na wewe mwenyewe? Akili yako inaamua kwenda mahali fulani, lakini ndani yako unasikia sauti ya chini inakukataza usiende! Ukiamua kwenda bila kuitii hiyo sauti ndani yako halafu ukapata shida huko uendako, utaanza kusema roho yangu ilinikataza! Roho yangu ilisita! Roho iligoma kwenda! Ahaah, roho yako ni wewe halisi, mwili ni koti tu.

Hata Yesu alithibitisha haya kwa waliodhani ni Roho baada ya kufufuka. Tusome Luka 24:37-39 na turudie 1 Thesalonike 5:23
 
Kabisa!
 
Asante.
 
Ndiyo maana nimetoka tujitambue kuwa sisi sote na wewe ikiwemo ni viumbe wa kiroho tunaoishi katika mwili.
Lengo ni kutaka kuliweka suala la kiroho nje ya mipaka tuliyoizoea
Hio mimi naita indoctrination..., na mwisho wa siku sababu ni Imani (kila mtu yupo entitled kuamini anachokiamini) pale tukitaka wote tuamini jambo moja ni mwanzo wa kushindwa kuvumiliana, hususan kwenye jamii zenye imani tofauti hence kama uwezekano upo kwenye mambo ya afya za watu imani iwe additional strategy na sio the only strategy.

Kama wanavyosema Imani yako itakuponya; huenda wewe imekuponya) sasa wasio na Imani ya kuweza kuhamisha milima hatuna budi kuwapa treatment kama inavyoshauriwa na daktari....
 
Mkuu unataka kukataa asili ya kila kitu?...sijaongekea dino hapa au imani yoyote ile ila nimeongea ulimwengu unaotawaka ulimwengu mwingine.
Elewa taratibu Kaka.
 
Shut up!!!! usituletee habari za Kibwetere hapa!! yaani watu wetu wana malizizika sababu eti habari za kiroho!! amabazo hamzijui mbona mnakuwa wajinga hivi? mnamjaribu jaribu Mungu na mambo ya kijinga jinga kabisa tu!!!

Huyo mungu wenu wa kilokole huyooo!!! hakawiagi kuwa geuka nyie fanyeni upuuzi huo tu na mizaa isiyokoma!!! na mungu wa Jiwe ni mzungu yuko anaiishi hapo Vaticani palee ukivuka Tunisia tu!!!

Tangu zamani mungu mzungu hawapendi waafrica!! na hata kaa awapende hata mtambike uchi!!! anawaangalia tu mlivyo ving'ang' anizi lkn mpaka leo wewe na mkemia wako huyo mnamwamini tu hamtaki kujifunza nani Mungu wa kweli????
 
Umeshauri vema kabisa na kwa uungwana. Safi!
 
Hakuna ujasiri wowote wa kiroho anakimbia majuku yake kwa kutumia mwamvuli wa imani. Mbona kwenye malaria hawaambii muache kutumia neti zinazotoka mabeberu. Au mungu wenu ni wa Corona tu?
 
Nimeshaeleza na ninaendelea Mkuu fuatilia thread ila tambua wewe ni kiumbe wa kiroho anayeishi ndani ya mwili.
Usikubali mipaka ya muda na mahali inayoudhibiti mwili ikudhibiti na wewe.
Huezi eleweka! Roho na dunia wapi na wapi ww!?

Mathalani umeambukizwa korona, unapambanaje kiroho roho?
Na kipindupindu je?

Halafu ni lini kama nchi tulipambana kiroho?

Tupambane kuondoa ujinga, umasikini na maradhi, hayA ni mambo ya kiroho!?

Zipo taasisi za kidini zinazohusika na mambo ya kiroho na zinafahamika.

Serekali inayotoza watu kodi, inashtaki watu, kufilisi, kuwafunga na hata kunyonga watu. Wapi na wapi mkuu?

Acheni kutetea wanaokwepa majukumu kwa visingizio hewa.
 
Labda umekula ugoro mbichi,meko ni mentalcase hakuna mtawala anaaacha waliomchagua wanakufa ovyo bila yeye kutoa ujumbe wa kujikinga....ushetani na ujinga ndio unamsumbua,leo anasema barakoa za nje hazifai,wakti mwaka jana kazivaa sana na kukimbilia kwao kujificha
 
Tatizo ni kuchanganya waganga na maombi

Giza na Nuru havikai pamoja, tushike moja, kama ni waganga au Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…