Ujasiri wa Rais Magufuli juu ya janga la korona katika ulimwengu wa roho

Hivi anachofanya ni ujasiri au uoga wa kuujua ukweli?
 
Watanzania walichagua kiongozi wa nchi atakaewaongoza,sio kiongozi wa dini.Kuleta assesment za ki dini wakati umepewa ridhaa ya kuongoza watu mchanganyiko wakiwamo wasoamini Mungu ni usaliti. Serikali haina dini,ivo masuala ya dini yabaki kwa mtu binafsi.
Ugonjwa wa Corona ni tatizo linalohitaji kupewa ufumbuzi wa kitaalamu na waliobobea kwenye taaluma za magonjwa. Corona ipo na inaua na itaendele kutumaliza kama mkiendelea na hizi hadithi zenu.
 
Hapa uko sahihi kabisa ndugu yangu
Unajua nini? Mimi nilichokiona kwenye ulimwengu wa roho ni kwamba Mungu aliamua kumrudia JPM akitaka kuhakikisha kama JPM bado yuko kama alivyokuwa mwanzo kipindi Corona inaingia, na ambayo alimponya nayo, au ameshabadilika baada ya kupata uponyaji. Ni kwamba kulikuwa na kipigo cha mbwa kingeshuka kama angekuwa amebadilika. Sasa hivi ni ushindi tu, hakuna baya lolote litakalotokea, haya mengine yanayoendelea muda huu ni upepo tu unaovuma kwa muda mfupi, utapita!
 
Akili yako ndivyo inavyoona.
Ushuzi n'tupu

Naam.
 
Mungu hana dini wewe.
Kumtanguliza Mungu ni tofauti sana na kutanguliza dini.
 
Ujinga Mtupu
Naomba nikujibu hivi hatuoni kilichopo nje yetu ila kilichopo ndani yetu .
Kama ulimwengu wako wa ndani unaonesha ujinga basi kusema unaona ujinga hukosei kabisa kwa sababu ndicho uonacho.
 
Kwa hiyo wataalamu hawapaswi kumtanguliza Mungu?..
 
Hivi anachofanya ni ujasiri au uoga wa kuujua ukweli?
Mkuu ukweli ni kuamini ipo nguvu kuliko nguvu za kimwili na nguvu hiyo ni nguvu ya kiroho.
Kumtanguliza Mungu ni kujua ukweli kama ulivyo.
 
Mkuu hakuna kinachofanyika katika ulimwengu wa vitu ambacho hakuna asili katika ulimwengu wa roho.
Jaribu kuvuka mipaka ya ulimwengu wa vitu ili uone vizuri. Ulimwengu wa roho upo,unafanya kazi, ni sahihi, haubahatishi na ndiyo asili ya wanadamu wote.
Kila kitu kilianzia kwenye ulimwengu wa roho kuja kwenye umbile linalodhihirika katika ulimwengu wa vitu.
Vuka mipaka ya milango mitano ya fahamu utanielewa vizuri mno.
Karibu sana.
 
Soma uelewe ndo hujibu,nilichosema ni 'assessment' yake ni ya ki dini.wataalamu wanatumia taaluma zao na hekima za dini sio vice versa.
Mkuu hivi kumtanguliza Mungu ni assessment ya Dini ipi?...Mungu ana Dini kweli?..
Kuna masuala kuyaelewa yanahitaji zaidi ya kufikiri.
 
Mkuu hivi kumtanguliza Mungu ni assessment ya Dini ipi?...Mungu ana Dini kweli?..
Kuna masuala kuyaelewa yanahitaji zaidi ya kufikiri.
Duh,we mbona mgumu kuelewa! Ok let's try again.kafanya assessment ya ugonjwa kwa kutumia dini,yeye kama kiongozi naona haijakaa sawa.ukienda kwa mwanasheria kama una tatizo unategemea kusikia sheria zinasemaje sababu ndo zinazotumika kuendeshea maisha,pia ukienda kwa daktari kama unaumwa malaria unatarajia akupime na akwambie dawa gani utumie,kwa sababu ndo mipangilio yetu ya kimaisha ilivyo na wakati unatumia dawa unaomba Mungu akusaidie upone.Lakin iwapo utaambiwa omba Mungu,wakati unataka msaada wa kitabibu,utakuwa umepewa assessment za ki dini sio kitaalamu.
 
Mkuu nakuelewa vizuri kabisa lakini ni katika mipaka...majibu ya hoja yako yanadhibitiwa na mipaka mingi mno kiasi kwamba yanakuwa kama gereza lisiloruhusu kuvuka nje ya mstari wa mahali na muda.
Huenda thread hii haijaeleweka vizuri kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…