Ujasiriamali: Usindikaji wa Yoghurt na Mtindi

Ujasiriamali: Usindikaji wa Yoghurt na Mtindi

2. JINSI YA KUTENGENEZA YOGHURT

Yoghurt ni moja ya zao la maziwa ambayo yamegandishwa (fermented) na aina hii ya bacteria " Lactobacillus bulgaricus na Streptococcus thermophillus".

Kwa hapa Tanzania mazao ya maziwa ambayo yamegandisha ambayo yapo sokoni ni Yoghurt na Mtindi(Cultured milk/ Maziwa mala)

Hivyo naomba tuende katika mtiririko huu ili tuweze kulielewa somo letu.
i. Kwanini Maziwa yanaganda

ii. Utofauti kati ya Yoghurt, Mtindi na Mtindi wa kienyeji

iii. Ubora wa maziwa kwa ajili ya kutengeneza Yoghurt

iv. Utengenezaji wa Yoghurt

v. Changamoto za Ugandishaji wa Yoghurt

vi. Faida za Yoghurt.

i. KWANINI MAZIWA YANAGANDA (FERMENTING)

Bacteria waliopo kwenye maziwa hushambulia sukari ya maziwa (lactose) na kuibadilisha kuwa chachu -Lactic acid. Mtakumbuka kinachofanyoka hapa ni Anaerobic respiration kwa wale mnao ijua biology.

Anaerobic respiration ni aina yabuzalishaji nishati katika kiumbe hai pasipo kutumia hewa ya oxygen.
Hivyo bacteria wengi waliopo kwenye maziwa ni Anaerobs(hawahitaji oxygen kuzalisha energy/nishati). Hivyo matokeo yake baada ya kuitumia sukari ya maziwa kama chanzo cha nishati hutengeneza Lactic acid na hewa ya carbondiozide.

Asidi hii ya Lactic ikipambana (react) na protin iliyopo kwenye maziwa yanaganda. Hivyo asidi hii ya Lactic ndiyo husababisha maziwa kuganda.

Maziwa mabichi yatokapo kwenye Ng'ombe tu tayari yana bacteria. Yasipo chemshwa au kuwekwa kwenye Freezer yanachechuka/ ganda na kutoa mtindi wa kienyeji.

Bacteria hawa wa asili wapatikanao kwenye maziwa ( Streptococus lactis) hufanya kazi kuanzia nyuzi joto 20-40 centigrade.
Mtindi huu wa kienyeji ambao huchachushwa na bacteria hawa unakuna na sifa zifuatazo.
1. Kujitenga kwa Mtindi na maji, hivyo kulazimika kumwaga maji ili kupata mtindi.
2. Kuwa machachu sana.
3. Kutoa harufu mbaya
4. Kuwa na ladha isiyk nzuri
5.Kuwa unpredictable
6. Kuwa unconsistence( haya fanani kila ukigandisha).

Nimeona nieleze jinsi mtindi wa kienyeji ulivyo ili muweze kuutofautisha na Yoghurt na Mtindi wa kisasa ambao pia nitaueleza baada ya kueleza Yoghurt.

iii. UBORA WA MAZIWA KWA AJILI YA KUTENGENEZA YOGHURT.
Kuna vitu vya kuzingatia kwenye maziwa ili kuweza kupata Yoghut bora na salama( Safe and Quality).

Hizi ni baadhi ya vitu vya kuzingatia
* Maziwa yawe ni wholesome(original) au yapunguzwe mafuta kidogo

* Yawe masafi na yaliyochujwa na kitambaa

* Yasitoke kwa Ng'ombe mgonjwa au aliye kwenye dozi au Chanjo hivi karibuni.

* Yasiwe yamechachuka

* Yasitoke kwenye vyombo vilivyonoshwa kwa sabuni ya unga

*Yasitiwe maji

iv. UTENGENEZAJI WA YOGHURT
Nitarudi.
 
Mkuu naona hujazungumzia zile mamlaka za serikali zatakazo kuwa zinasimamia ubora wa bidhaa zako, mfano TFDA, TBS n.k
Nadhani kwenye gharama za kuanzia ilitakiwa na hiyo iwemo, plus kodi za majengo ili tupate gharama halisi ya kuinzia.

Lakini umetoa mwanga mzuri sana kwa wenye nia na hii kitu.
Binafsi nimeipenda sana. Tuwasiliane tuone tunafanhaje, mi mtaji ninao
 
Mkuu naona hujazungumzia zile mamlaka za serikali zatakazo kuwa zinasimamia ubora wa bidhaa zako, mfano TFDA, TBS n.k
Nadhani kwenye gharama za kuanzia ilitakiwa na hiyo iwemo, plus kodi za majengo ili tupate gharama halisi ya kuinzia.

Lakini umetoa mwanga mzuri sana kwa wenye nia na hii kitu.
Binafsi nimeipenda sana. Tuwasiliane tuone tunafanhaje, mi mtaji ninao
mkuu unawazo kama langu mkuu,kwa sasa niko shule mwez wa nane narudi kazini, cha kwanza ni kufanya research ya upatikanaji wa maziwa na soko, nikijirizisha tu naingi NMB, 5mil mfukon naanza mambo,uzuri usafiri upo, labda kukodi jengo tu. pia naomba msaada uni-pastie nondo hizi kwenye email yangu, sim yangu imegoma ku hilight,

demafa88@gmail.com
 
Back
Top Bottom