Ujasusi Macho Manne

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UJASUSI MACHO MANNE!

Anaandika, Robert Heriel.

Nilianza kuvutiwa na Ujasusi nikiwa Kidato cha pili huko Makanya, Kwa mara ya Kwanza Neno Ujasusi nililipata miaka hiyo nikisoma Biblia, kisa cha Kwanza cha Ujasusi kilichowazi nilikipata kwenye Kisa cha Yusufu alivyowaambia Ndugu zake wamekuja Misri kuipeleleza nchi(alikuwa akiwazingua) visa vingine vya Ujasusi Kwa wakati huo ningali mdogo ni kisa cha Joshua na Kalebu walivyoagizwa kuipeleleza nchi, Kisa kingine Kisa cha Hadasa ambaye alikuwa Jasusi pandikizi aliyepandikizwa na Mjomba wake aitwaye Mordekai, Hadasa akapewa jina Bandia lenye asili ya Kiashuru Akiitwa Esta ikiwa na maana ya jina lake la awali "Hadasa"
Kisa cha Malkia Esta kwenye Biblia ni muendelezo wa visa vya Kijasusi ndani ya Biblia.

Kisa cha Jasusi Delila, aliyemuangusha Samson baada ya kumchokocha na kuijua Siri ya Asili ya nguvu zake. Niliwahi andika Jambo hili pia.

Ujasusi nyakati nikiwa shuleni ulinisaidia mambo kadhaa Yafuatayo;

1. Kuepuka adhabu za kuchapwa hovyo hovyo, au matukio ya kushtukiza ya misako ya simu nilipokuwa Advance
Ujasusi unahitaji ukusanye Taarifa Kwa kadiri uwezavyo ambazo utazitumia katika kujilinda na mambo yako mengine.
Ujasusi utakuhitaji uchimbe mifereji kutoka kwenye vyanzo vinavyokupa taarifa ili uweze kujihami ikiwa tatizo lolote litatokea.

2. Kufaulu mitihani bila kutumia nguvu kubwa
Kwa waliosoma na Mimi watakuwa mashahidi kuwa Taikon Hakuwa msongokaji, sikuwa John kisomo Mimi, nilikuwa nasoma Kwa akili sio Kwa bidii, bidii kubwa niliiweka kwenye Akili ya ku-mastet mazingira na kujua waalimu wanaonifundisha wanahitaji nini, kusoma Saikolojia zao, na nini wanahitaji kutoka Kwa wanafunzi.
Kwa waliosoma na Mimi watakuwa mashahidi sikuwa mtu wa kuandika Notes, Kwa kweli nilikuwa mvivu Sana,
Unajua nini Kufaulu inahitaji akili, sio tuu ya darasani Bali hata ya mtaani.

3. Kujipatia Warembo
Kama Vijana wengine, nyakati za Balehe Vijana tunavutiwa na wasichana. Ujasusi utakusaidia kujipatia warembo kirahisi tuu pasipo kutumia nguvu, Kivipi? Mimi nikiwa O'Level sikuwa na pesa ukizingatia nimetokea familia yenye kipato cha chini, uvaaji wangu haukuwa wa kuvutia Sana licha ya kujitahidi kuwa msafi. Lakini kitu pekee nilichokiweza Kwa umri ule wa miaka tuu 15 nilidodosa ni vitu gani wasichana wanapenda Kwa wavulana. Nikapata majibu haya; Wasichana wa umri wa sekondari wanapenda Vijana HB, wenye vipaji, wacheshi na wenye kujua kuzungumza Kwa kujiamini, pesa ilikuwa sifa mojawapo lakini haikuwa kwenye listi za juu.

Kwa kweli Kwa ucheshi hilo nililimudu ingawaje sikuwa mtu wa mchezo Kwa watu wasionijua, yaani ukiniona Kwa mara ya Kwanza ungedhani sio muongeaji, mpole, Mstaarabu na nisiyependa mazoea lakini kadiri tukiwa karibu utagundua sipo hivyo.

Vipaji vya uimbaji na kucheza nako sikuwa nyuma ingawaje sikuwa mzuri Sana lakini niligangamala, nilifanikiwa.

Nyakati nasoma kitu nilichofeli Kwa kweli na ambacho nilitamani kuwa nacho ni Kuwa mbabe, nikitamani niwe mkorofi na mwenye kupiga watu, Hilo sikufanikiwa Kwa sababu nilikuwa muoga ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€. Niliogopa kutoka manundu au kutolewa Damu piano๐Ÿ˜Š

4. Kupata Material ya kujifunzia
Ujasusi ulinipa Mianya ya kujipatia vitabu na materials ya kujifunzia nikiwa mwenyewe. Mimi ni Wale wanafunzi ambao shuleni tulikuwa wapiga kelele lakini usiku tunasoma. Hivyo nilifanya jitihada za kuunda urafiki na Waalimu WA Maktaba, kisha Yale masomo ambayo yalikuwa na uhaba wa material niliunda urafiki na waalimu WA masomo hayo.

Pia niliweka marafiki katika muundo wa kimkakati, wapo marafiki majizi yaliyokuwa yanaiba Vitabu vya waalimu na Wanafunzi, nilijitahidi kuwa nao karibu, hivyo nilipata vitabu na kujifunzia kupitia wizi wao. Unajua Maktaba huwezi chukua vitabu vingi, na pia hata ukichukua vingi pia unaweza ukapoteza, hivyo Kwa kujihami ilinipasa nitafute Alternative ambayo ndio hiyo.

Kuna rafiki yangu Ghetto lake lilijaa vitabu vya kila Aina, ungedhani ni Maktaba. Na wezi wengine nilihakikisha nawafahamu ingawaje sikutaka wajue ninawafahamu isipokuwa Kwa marafiki zangu. Kuna Wale waandika Notes hao nao niliweka urafiki nao hasa Wale waliokuwa wanaufaulu unaoniridhisha, nisingeweza kuchukua Notes za watu wanaofeli Hilo kwangu nisingekubali.

Jambo moja la kukukumbusha ni kuwa Mtu yeyote asiyeandika Notes Darasani alafu akawa anafaulu ni aidha awe mwizi wa madaktari ya wenzake au vitabu, au kanunuliwa vitabu na wazazi wake.
Au atumie mbinu Kama yangu,

5. Kula chakula kizuri cha waalimu ambacho tulikuwa tunakiiba
Ujasusi ulitusaidia kuiba vyakula vya waalimu wakati tunasoma, usije ukadhani ujasusi unatumika kwenye ishu chanya tuu utakuwa unajidanganya, pia unajihusisha na ishu Hasi Kama za wizi. Chakula cha shule kilituchosha jamani, tulipofika Kidato cha tatu tukiwa tume-master shule na kuijua in and out tukaanzisha Wizi wa vyakula vya waalimu.

Kwa vile Mimi nipo Polite na ukiniona Nina Sura Innocent lakini pia nilikuwa najulikana Staff na waalimu hivyo wenzangu walikuwa wakinitumia Mimi kwenda Staff kupeleleza mazingira yamekaaje, hakuna yeyote ambaye angenishuku, hata hivyo Kwa wale waalimu ambao wanatabia ya kujifanya wanashtukia niliwaweza Kwa mdomo wangu na ucheshi, Hilo nilikuwa mahiri. Jiko lilikuwa karibu na Staff ya waalimu hivyo ili ufike jikoni itakupasa aliyeko Staff akuone ndio maana Mimi ilinipasa nitangulie Staff.

Kama ningekuwa waalimu basi ningerudi kurejesha ujumbe kuwa kuna waalimu, huku moja ya Wale waalimu nikimuambia kuna kazi namleta anisaidie. Hivyo wakati nimewapanga wenzangu kuwa waanze kusogea Mimi nikiwa-keep Busy waalimu Kwa maneno yangu mengi huku nikielekezwa maswali Fulani. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Ingawaje kuna siku tulikamatwa tukiwa Kidato cha nne, tulipigwa bakora mbele ya shule๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ lakini ilikuwa Too late shule imeshaisha.

6. Kuepuka Kufukuzwa Shule
Nikiwa na rafiki yangu aitwaye Issa tukiwa tumetoka kuiba chakula cha waalimu, tuliratibu maandamano ya shule kugoma Kula Makande Kwa sababu walizirusha zaidi ya wiki mbili siku za wali. Jambo la uhakika ni kuwa nyakati zingine wakati wizi unatokea wapo Waalimu wanaojua wezi halisi sema kutokana na ukaribu wao na wanafunzi hao wanajikuta wanakaa kimya.

Tulimchochea Headboy, na kiranja WA chakula wawagomeshe wanafunzi Kula, tulihakikisha tunamjaza Headboy naye Kwa Kupenda sifa akajaa. Mzizi wa Jambo hili ulikuwa Rafiki yangu kugombea Demu na Headboy hivyo tuliamini Kama maandamano yatafanyika Sisi tukiwa nyuma kabisa Headboy atafukuzwa shule na kupewa Suspension. Rafiki yangu alikuwa akilalamika Sana kuhusiana na Jinsi Headboy anavyotumia Cheo chake kumchukua Demu ampendaye, ndio tukafikia uamuzi huo.

Tulichofanya ni kwenda kuomba ruhusu kuwa rafiki yangu anaumwa hivyo nitampeleka Hospitali, kisha baada ya kupewa ruhusa muda ya saa Saba hiyo zikiwa zimesalia dakika chache Kengele ya Lunch igongwe, baada yakuchukua ruhusa ndio tukamchochea Kwa nguvu Headboy na kiranja wa chakula tukamsaidia kupita Darasa moja mpaka jingine kuwaambia wanafunzi Kengele ya chakula ikigongwa waende Assemble tuandamane. Tulitembelea madarasa yote.

Kengele ilipogongwa tukaona wanafunzi wakienda assemble huku wakiimba wakiongozwa na Headboy, tukaona tumefanikiwa, tukaondoka zetu kwenda Hospitali. Headboy alifukuzwa kwenye Cheo chake, kisha wakati akiwa hayupo Kwa adhabu ya suspension tukautumia muda huo kumnyang'anya Demu wake. Hiyo ilikuwa rahisi Sana.

Jambo moja la kuweka kichwani ni kuwa sio kila ushauri unaopewa unatakiwa uufuate hasa kwenye mambo ya utawala.

7. Kuepuka kuonewa na Kuibiwa
Shuleni kuonewa Kwa miaka ya kipindi kile ilikuwa kitu cha kawaida Sana. Ujasusi unaweza kukufanya usionewe. Mbinu nilizokuwa nazitumia hasa nikiwa Mgeni ni kuwahi siku moja kabla shule hazijafunguliwa, mbinu hiyo ilinisaidia nikiwa fomu One, Kidato cha tano, na Chuo kikuu mwaka wa Kwanza. Unapowahi shule au Chuo unaepuka kuwekwa mtu Kati, kuingizwa mjini na ndevu.
Unafika mapema unasoma mazingira, na wewe ndio unaona wenzako wakija, unajua Nani ni Nani, ukiwa tayari ushaizoea shule au Chuo. Ushapata uhalisia wa baadhi ya mambo ya shule au Chuo na watu wake.

Wanafunzi wezi na matapeli ni rahisi kuwajua ukiwahi kuliko ukichelewa.

8. Kushirikiana na Jamii! Na kupata Favour za jamii husika
Ujasusi ni muhimu ukiwa mwanafunzi kwani itakusaidia katika kuchangamana na jamii yako au jamii ngeni. Mbinu kubwa hapa ni kushiriki katika shughuli za kijamii kwa kupitia Vyama vya Kidini vilivyopo shuleni Kwa Mfano ASSA Kwa Wasabato, KIMSIYA Kwa waislam, TYSS Kwa Wakatoliki, UKWATA Kwa Walutheri Na CASFETA(sijui hawa ni dhehebu gani) Hii itakusaidia kupata mialiko wakati WA wikiendi kwenda Kula au kupoteza muda baada ya kuchoshwa na shule Kwa wiki nzima, upata vizawadi kutoka kwenye jamii inayozunguka shule. Mfano nilipokuwa Mbeya Matema Beach nilikuwa naletewa maziwa Fresh karibu kila jioni, maparachichi, Dagaa wa ziwa Nyasa, Wale wote tuliokuwa Social shule ilikuwa sehemu ya Burudani, wala chakula cha shule tulikuwa hatukiwazii maana tulishaweka mafungamano na wanajamii.

Hii pia itasaidia siku ukikamatika na makosa kwenye jamii hasa makosa ya ujana Kama kukutwa na Binti wa mtu n.k.

9. Kuepuka Migogoro na Waalimu au viongozi wakubwa katika jamii husika
Ujasusi utakusaidia kupata taarifa za watu na tabia zao na shughuli wazifanyazo. Hii itakusaidia kutoingia kwenye migogoro isiyo ya maana uwapo katika Mazingira yoyote. Ni ngumu Sana Baraza la shule au jamii kukuzingua Kama upo makini katika Ujasusi, utakuwa mtu Mwema Kwa waliowema, utakuwa mtu mbaya Kwa waliowabaya Ila hawatakuwa na time na wewe.

10. Ni rahisi kumshambulia Adui Kwa njia isiyo ya moja Kwa moja
Ujasusi shuleni unaweza kukusaidia kumdhuru adui yako aliyekuzingua Kwa namna isiyo ya moja Kwa moja. Mathalani, mshindani wako wa darasani unaweza kumtengenezea zengwe akashindwa na kupoteza Pambano Lenu Kwa kumpa shughuli zitakazompotezea muda asi-focus na masomo Bali a-focus na mambo mengine mfano. Rafiki yangu alikuwa katika Battle la kimasomo na Mwanafunzi mwingine tuliyekuwa tunasoma naye, wakawekeana pesa Kwa mitihani ya Mock.

Akaniomba ushauri, nikamwambia Kwa vile Mshindani wake anapenda sifa za kijinga basi tuwatumie wanawake kumpotezea muda, akasema kivipi, nikamwambia tutawapanga wasichana kadhaa WA Darasa letu alafu tutawashauri awe anawaelekeza somo la Mathematics, hivyo kila mwalimu anapotoka wawe wanaenda kuelekezwa na mshikaji. Wazo hilo likawa Bora.
Basi kila tukiwa na Free hasa baada ya lunch wake Wadada Tuliowaandaa walikuwa kazi hiyo wakiifanya, wanamfuata mshikaji wanamuomba awaelekeze.

Tulikuwa Yafuatayo;

1. Mshikaji ataona anaonekana anaakili na Wale warembo, ndio maana ataichukulia nafasi hiyo kama utukufu kwake na kujitamba mbele ya Rafiki yangu.

2. Mshikaji ataona Ile ndio nafasi ya kujipatia mrembo Kati ya Wale wasichana maana tulichagua wazuri, walikuwa watatu.

Muda mwingi aliutumia kuwaelekeza wale wasichana katika somo moja tuu huku akiyaacha masomo mengine nane.
Nilimuambia rafiki yangu kuwa atafaulu Kwa kiwango cha juu kumshinda katika somo Hilo tuu hata mengine Atashindwa.
Mtihani ulifika tukafanya ikawa Kama tulivyopanga. Huo ni mfano tuu WA namna ya kukabiliana na adui indirect way.

Kwenye mapambano sio lazima utumie Direct way kwani mara nyingi inamadhara kuliko indirect way. Indirect way itahitaji tuu akili nyingi na mikakati kabambe

Huo ni muhtasari wa Ujasusi katika Mazingira ya shule Kwa ngazi ya Vijana wadogo wenye umri kuanzia miaka 10-23.
Hata hivyo mambo hayo huweza kutumika hata katika Kwa watu wazima, kwenye familia, biashara, makampuni, Serikali n.k

Kwa leo tunaishia hapa, siku nyingine tutaendelea Ujasusi macho manne katika watu wenye umri kuanzia miaka 24-45.

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Moshi!
 
Hapo pa miaka 24-45 naomba usisahau kunitag mkuu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ