UJASUSI; Usiwaambie watu Ndoto/malengo yako. Future ni Siri na ndoto inapaswa kuwa Siri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UJASUSI; USIWAAMBIE WATU NDOTO/MALENGO YAKO. FUTURE NI SIRI NA NDOTO INAPASWA KUWA SIRI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Hakuna anayeijua Kesho. Hiyo ndio Kanuni namba Moja ya UJASUSI. Kama hakuna ajuaye Kesho basi nawe unatakiwa kuhakikisha hakuna ajuaye ndoto au Hatua yako inayofuata ni nini.

Kuijua Kesho ya Mtu mwingine ni kumtawala, kumdhibiti na unaweza kumchekecha vile unavyotaka.

Leo Taikon Master, Naam ndiye Mtibeli Kutoka Nyota ya Tibeli. Sitakuwa na Maneno Mengi. Nitakueleza umuhimu wa kuficha ndoto/malengo na mipango, mikakati na Hatua zako zinazofuata mbele ya kadamnasi.

Sio kila unayemuona mbele yako ni mwema kwako. Sio kila aliyekaribu yako anakupenda. Niliwa kukuandikia kuwa Rafiki ni adui aliyekaribu yako.

Zipo sababu maalumu kwa nini unachokiwaza ubongoni mwako hakuna mtu mwingine anaweza kukijua zaidi yako mwenyewe. Na ili mtu ajue unachowaza lazima umshirikishe kwa kumwambia kile unachofikiria akilini mwako. Hiyo tosha ingetosha kukupa picha kuwa dunia ya Kesho IPO mikononi mwa wale wanaojua kuficha Mawazo Yao na kuyatekeleza wakati sahihi utakapofika.

Kama Jambo utalifanya Mwakani au Miaka kumi au ishirini ijayo kuna ulazima gani wa kulisema mbele za watu Leo hii. Embu jiulize!

Hutakiwi kumwambia yeyote Yule malengo au mipango yako ijayo.
Kama kungekuwa na ulazima wa kuwaambia watu wako wa karibu Basi naturally mawazo ya watu yangekuwa connected automatically na wale watu wanaowapenda ikiwemo Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.

Mtu anampango wa kuanzisha biashara Mwakani. Unakuta anaanza Kuropoka ropoka vitu visivyoeleweka.
Ndoto yako ya kuanzisha biashara kuiweka hadharani ni kujaribu kuihujumu, kuichelewesha na wakati mwingine kuiangamiza wewe mwenyewe.

Unampango wa Kuolewa au kuoa hivi karibuni. Kaa Kimya.
Weka mipango yako vizuri
Ifanye ikae vizuri.
Ikishafika Muda WA Jambo kutokea ambapo inahitaji ushiriki WA watu kama kuchanga michango ya harusi ndio upeleke Ombi Lako mbele za watu.

Unampango wa kuwa Rais au kiongozi katika ngazi Fulani. Tulia! Weka mipango na mikakati yako kimyakimya. Ikishahakikisha umeiseti vizuri na sasa unahitaji kuwa mbele za Umma jitokeze mdogomdogo. Anza polepole kama utaweza andaa drama na propaganda kupima Kina cha Maji. Usijitokeze mwenyewe mapema. Jitokeze ukishajihakikishia kuwa upo Mbele kwa zaidi ya asilimia 70%.

Kwa nini hutakiwi kuisema kwa Watu ndoto au malengo yako;

1. Wewe bado ni mchanga
Fikiria hauna mtaji alafu unatangaza mbele za watu unataka kuwa mfanyabiashara Mkubwa.
Fikiria hauna Kazi lakini unatangaza unandoto ya kuwa Mkurugenzi Mkubwa sijui manager.
Fikiria hauna lolote, uko na mpenzi wako unatangaza bila Akili ndiye utakayemuoa kwa kumuanika mitandaoni.

Unajua nini kinatokea?
Kusema ndoto yako mbele za watu ukiwa mchanga ni kuiuza hiyo ndoto kwa wenye nguvu na wakomavu.
Wapiga ramli, Washirikina, Wachawi, wenye husda wataingia mzigoni kukuzonga. Na kwa vile wewe bado mchanga watakutoa kwenye Reli. Wataiangamiza ndoto yako au kukuangamiza wewe mwenyewe.

2. Kuleta upinzani wakati usiosahihi.
Ni kweli ili ndoto yako itimie lazima upate upinzani.
Lakini lazima uelewe kuwa sio kila wakati ni wakati wa Kupata upinzani.
Ni wewe unayeamua wakati upi sahihi wa Kupata upinzani.
Katika kuchagua wakati wa Kupata upinzani ni hekima kuchagua wakati ambao utakuwa umejiandaa vya kutosha, umekomaa vya kutosha, na sasa unauwezo wa kukabiliana na nguvu yoyote ya upinzani.

Kuleta upinzani wakati ukiwa haujajiandaa ni kujiangamiza mwenyewe. Ni kuzima ndoto na malengo yako kimakusudi. Na wakati mwingine inaweza kukugharimu maisha yako.

Taikon Master ninakuambia mpiganaji hodari anajua ni wakati gani sahihi wa kuruhusu maadui washambulie.
Hii inamaanisha vita hiyo inakuwa chini ya uratibu wako. IPO kwenye Warmap yako(Ramani yako ya kivita).

3. unavunja Kanuni za Kijasusi.
Kanuni za Kijasusi Mojawapo ni kukusanya taarifa, kuzichambua, kuzidadavua, kuziwekea mipango na matumizi yake, kujua rasilimali zinazohitajika ndipo kuingia mzigoni au kwenye pambano.
Na sio utangaze na kuingia kwenye pambano ndipo uanze kukusanya taarifa za vita.
Vita hazipo hivyo. Kitendo cha kuingia vitani au kutangaza vita alafu ndio unaanza Kutafuta taarifa za kiintelejensia ujue umepigwa kwenye hiyo Vita na lazima utapoteza.
Na kama utashinda basi utatumia Muda mrefu Sana hata adui angekuwa mdogo kiasi gani.
Yaani kutimiza ndoto hata kama ni ndogo kiasi gani utachukua Muda mrefu ikiwa utaitangaza ndoto hiyo kabla ya kuwa umejiandaa kikamilifu.

Sababu za watu wengi kutangaza au kusema mbele za watu Ndoto au malengo Yao;

1. Utoto.
Akili za kitoto yaani ambazo ni changa ambazo hazijapevuka, hazijui Dunia ikoje hujikuta kwenye hatari ya kuzisema ndoto au malengo yao mbele za watu.

Nabii Yusufu yupo katika Kundi la watu hawa.
Yeye aliota Ndoto ambayo alijulishwa na miungu yake kuwa atakuwa mtu Mkubwa na ndugu na Wazazi wake watamuinamia. Lakini kwa utoto wa Yusufu, alienda kuwahadithia ndugu na Wazazi wake ndoto hiyo yeye akiona labda ni Jambo la kawaida. Kumbe sivyo.
Kilichotokea wote tunajua.
Ni kupitia ndoto hiyo Yusufu alitaka kuuawa lakini Kwa bahati Njema akauzwa na ndugu zake na kupitia madhila makubwa kwa Miaka mingi Sana.

Wasikilize ndugu za Yusufu; zingatia Maneno niliyokoleza kwa wino mweusi;
Mwanzo 37
19Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. 20Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.
Unaona mambo hayo; yaani kuna watu watakuzonga na kukukwamisha ikiwezekana kukuua ili tuu ndoto na malengo yako yasitimie.
Nataka kukuambia Yusufu alisota sio pungufu ya Miaka 40 kwa kosa dogo la kuisema na kutangaza ndoto yake.
2. Kutokuwa na uelewa WA mambo.
Kuna wengine sio watoto lakini wanauelewa finyu kwenye ishu kama hizo.
Kwa hiyo wao kila kitu husema sema.
Kila mipango Yao huisemasema.
Jamani sio kila Mtu wa kumwambia mipango yako. Tumia AKILI.
Ni vizuri kama umeoa mipango yenu wewe na Mkeo/Mumeo muijue ninyi tuu.
Na kama unajua mwenza wako ni roporopo basi hata yeye unaweza ukamficha kwa Muda. Mpaka ndoto yako itakapokuwa imefikia asilimia angalau 70% ya kufanikiwa.
Kuna watu Miaka nenda Rudi wameoa na Kuolewa. Kila mwaka ni Mipango. Mara kununua kiwanja, mara kuanza Ujenzi. Lakini kutwa kuchwa midomo IPO wazi wanaisema mipango Yao kwa Watu wasiohusika.
Unamwambia shoga yako kuwa mwaka huu unampango wewe na Mumeo mjenge. Shoga yako anahusika na nini kwenye nyumba yenu?
Mamaako/ Babaako, ndugu zako wanahusikaje kwenye mipango yenu ninyi kama Familia.
Kuwashirikisha ni Jambo zuri lakini kuna wakati sahihi wa kuwashirikisha. Hasahasa wakati Jambo limeshakamilika. Mmeshajenga nyumba, unataka kusherehekea iteni watu mfurahie.
Kisa cha Yusufu kinaelezea Jambo nyeti Sana kuhusu umuhimu wa kuficha baadhi ya ndoto nyeti hata kwa Wazazi.
Yusufu alipoota ndoto ya Kwanza, iliyowahusu ndugu zake kumuinamia Baba yake Mzee Yakobo hakuona tatizo na Wala hakumnyamazisha. Lakini, kwenye ndoto ya Pili ambayo sasa haikuwahusu tuu ndugu zake Yusufu Bali iliwahusu Wote yaani ndugu za Yusufu na Wazazi wake(Baba, Yakobo na Mama zake, wakeze Yakobo). Hapo ndoto hiyo ikamuudhi na kumkasirisha Mpaka Yakobo kiasi cha Yakobo Kumkemea Yusufu, Mwanaye.
Kula chuma hicho zingatia Maneno yaliyokolezwa;
Mwanzo 37:
9 Akaota tena ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake, akasema, Angalieni, nimeota ndoto nyingine; na tazama, jua na mwezi na nyota kumi na moja zikaniinamia.
10. Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie hata nchi?
11 Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.

Hii inatuambia na kutupa funzo kuwa sio ndoto au malengo yako unatakiwa umwambie Baba au mama yako. Kuna mambo ya kawaida unaweza mshirikisha lakini kuna mambo mengine hupaswi kumshirikisha hata mzazi wako.

NIlisema Leo sitakuwa na Mengi ya kuandika. Kufikia hapa Sina la Ziada.

Acha nipumzike sasa

Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hao wanaojiita watabiri itakuaje Sasa? Ngoja waje niwa zoom maana nipo benchi la mbele hapa
 
It is true!
 
Sasa hivi nawahi kazini kuliko mfanyakazi yeyote na pia Kuna muda mpaka nawasaidia wadada wa usafi kufanya usafi ,Siri ni kuwa nataka nipate tuzo ya mkoa ya mfanyakazi bora .
Alafu hata sijamwambia mtu Ila nimeona nguvu ya kuficha Siri naona mpaka mfawidhi kachanganyikiwa kuhusu haya Mambo yangu ,Sasa hivi Kuna muda anapiga jioni eti kuniuliza kazi za siku nzima zimeendaje na Mimi namwambia kila kitu hata Kama Kuna waliowaomba wagonjwa rushwa sifichi ng'o mpaka niwe mtumishi bora wa mwaka nipate Cha kuwaringishia wanangu huko uzeeni .

Haya maajabu yamekuwa kwa wafanyakazi wenzangu maana walishanizoea kuchelewa kazini na pia kuja nikiwa nimelewa Ila kwasasa nimekuwa tofauti hakika nawachanganya Sana .

Itoshe kusema Mtibeli uko sahihi Sana ,siku nikipata tuzo ya mtumishi bora nitakusimulia itakavyokuwa
 
Ha ha ha ha kweli umedhamiria....unawasaidia usafi hadi "cleaners" !
 
SIJAJUA SANA MNACHOMAANISHA AU LABDA INATEGEMEA NA MIPANGO YENYEWE...

BINAFSI MIMI WAKATI 2025 INAANZA NILITAMANI KUFUGA KUKU NA HATA WATU WANGU NILIWAJULISHA NA KAMA UTANI NIKAANZA NA KUKU WATATU HATIMAYE LEO TU NINA KUKU ZAIDI YA 27..NA STILL NAWASIMULIA WATU MAENDELEO HAYO NATOA TESTIMONY LENGO NI KUTOKUA MCHOYO NATAKA WENGI WAFANYE UFUGAJI PIA..

KAMA KUNA MTU ANA CHUKI NA HUSUDA NA HAPENDI NIWE NA KUKU BASI AFANYE ANACHOTAKA KAMA NI KUWAIBA AU KUWAPA SUMU..ILA MIMI NITAENDELA KUSIMAMA NA KUKU NAPENDA WAFIKE HATA 100 HIVI..SINA MENGI AKILI YANGU NIMEINGIA KWENYE KUKU TU
 
Eeee Kaka na sio sehemu zilizojificha napenda ninapoonekana na wengi yaani karibu na geti la kuingilia maboss wote na wafanyakazi wote yaani nawachanganya Ila Siri ni tuzo Kaka .
Maana nilikaa nikawa naangalia sebuleni Sina picha za heshima na pia kwenye vyeti vyangu ninavyo vya shule tu sikuona hata cheti Cha appreciation Wala kutambuliwa nikaogopa siku watoto watauliza baba wewe kazini hakuwa na bidii yoyote ikabidi nipambane kaka
 
SIJAJUA SANA MNACHOMAANISHA AU LABDA INATEGEMEA NA MIPANGO YENYEWE...

BINAFSI MIMI WAKATI 2025 INAANZA NILITAMANI KUFUGA KUKU NA HATA WATU WANGU NILIWAJULISHA NA KAMA UTANI NIKAANZA NA KUKU WATATU HATIMAYE LEO TU NINA KUKU ZAIDI YA 27..NA STILL NAWASIMULIA WATU MAENDELEO HAYO NATOA TESTIMONY LENGO NI KUTOKUA MCHOYO NATAKA WENGI WAFANYE UFUGAJI PIA..

KAMA KUNA MTU ANA CHUKI NA HUSUDA NA HAPENDI NIWE NA KUKU BASI AFANYE ANACHOTAKA KAMA NI KUWAIBA AU KUWAPA SUMU..ILA MIMI NITAENDELA KUSIMAMA NA KUKU NAPENDA WAFIKE HATA 100 HIVI..SINA MENGI AKILI YANGU NIMEINGIA KWENYE KUKU TU
Naomba mbinu na njia unazotumia Kaka kutoka kuku 3 mpaka 27 kwasasa
 
SIJAJUA SANA MNACHOMAANISHA AU LABDA INATEGEMEA NA MIPANGO YENYEWE...

BINAFSI MIMI WAKATI 2025 INAANZA NILITAMANI KUFUGA KUKU NA HATA WATU WANGU NILIWAJULISHA NA KAMA UTANI NIKAANZA NA KUKU WATATU HATIMAYE LEO TU NINA KUKU ZAIDI YA 27..NA STILL NAWASIMULIA WATU MAENDELEO HAYO NATOA TESTIMONY LENGO NI KUTOKUA MCHOYO NATAKA WENGI WAFANYE UFUGAJI PIA..

KAMA KUNA MTU ANA CHUKI NA HUSUDA NA HAPENDI NIWE NA KUKU BASI AFANYE ANACHOTAKA KAMA NI KUWAIBA AU KUWAPA SUMU..ILA MIMI NITAENDELA KUSIMAMA NA KUKU NAPENDA WAFIKE HATA 100 HIVI..SINA MENGI AKILI YANGU NIMEINGIA KWENYE KUKU TU
Hapo ndio watu wataanza kutofautisha ndoto na mipango
 
Back
Top Bottom