UJASUSI; Usiwaambie watu Ndoto/malengo yako. Future ni Siri na ndoto inapaswa kuwa Siri

UJASUSI; Usiwaambie watu Ndoto/malengo yako. Future ni Siri na ndoto inapaswa kuwa Siri

SIJAJUA SANA MNACHOMAANISHA AU LABDA INATEGEMEA NA MIPANGO YENYEWE...

BINAFSI MIMI WAKATI 2025 INAANZA NILITAMANI KUFUGA KUKU NA HATA WATU WANGU NILIWAJULISHA NA KAMA UTANI NIKAANZA NA KUKU WATATU HATIMAYE LEO TU NINA KUKU ZAIDI YA 27..NA STILL NAWASIMULIA WATU MAENDELEO HAYO NATOA TESTIMONY LENGO NI KUTOKUA MCHOYO NATAKA WENGI WAFANYE UFUGAJI PIA..

KAMA KUNA MTU ANA CHUKI NA HUSUDA NA HAPENDI NIWE NA KUKU BASI AFANYE ANACHOTAKA KAMA NI KUWAIBA AU KUWAPA SUMU..ILA MIMI NITAENDELA KUSIMAMA NA KUKU NAPENDA WAFIKE HATA 100 HIVI..SINA MENGI AKILI YANGU NIMEINGIA KWENYE KUKU TU
...malengo madogo ya ufugaji vikuku 27 yamtie husda fatani MWENYE AKILI ?!! Ha ha ha ha
Fatani MWENYE AKILI angeogopeshwa na kufuga kuku elfu huku ukimtangazia kuwa umepata tenda ya kila siku kupeleka kuku 50 kwenye hoteli kubwa .....
 
Naomba mbinu na njia unazotumia Kaka kutoka kuku 3 mpaka 27 kwasasa
Nilianza na kuku 3 nilinunua 7000,7000, na mmoja 8000

Kisha nikaja kuongeza majogoo watano Kuna dogo tulibadilishana nilimpa simu smart na wote walikuwa machotara...
Baadae nikaongeza makoo wawili kienyeji wakubwa niliwanunua wote kwa 30000....baadae wawili wakatamia vifaranga 18..na wamekuwa wakubwa sijawahi KUWAPA hata chanjo moja..nahisi napokaa magonjwa hakuna maana ni porini kdg kwenye kagetto changu mwenyewe..sasa hizo ndo malengo makuu kwa mwaka huu nifikishe kuku 100..mixer wa kienyeji na chotara...sioni ubaya kusimulia watu WOWOTE wanaopenda hii sekta..
 
...malengo madogo ya ufugaji vikuku 27 yamtie husda fatani MWENYE AKILI ?!! Ha ha ha ha
Fatani MWENYE AKILI angeogopeshwa na kufuga kuku elfu huku ukimtangazia kuwa umepata tenda ya kila siku kupeleka kuku 50 kwenye hoteli kubwa .....
Ndo maana nasema kwamba INATEGEMEA na malengo Mimi binafsi kuzungumzia mipango ya kuku sioni kama Kuna ubaya kwani kupitia stori na watu napata pia maarifa mengine ya kuzalisha
 
Dah kweli
Nilianza na kuku 3 nilinunua 7000,7000, na mmoja 8000

Kisha nikaja kuongeza majogoo watano Kuna dogo tulibadilishana nilimpa simu smart na wote walikuwa machotara...
Baadae nikaongeza makoo wawili kienyeji wakubwa niliwanunua wote kwa 30000....baadae wawili wakatamia vifaranga 18..na wamekuwa wakubwa sijawahi KUWAPA hata chanjo moja..nahisi napokaa magonjwa hakuna maana ni porini kdg kwenye kagetto changu mwenyewe..sasa hizo ndo malengo makuu kwa mwaka huu nifikishe kuku 100..mixer wa kienyeji na chotara...sioni ubaya kusimulia watu WOWOTE wanaopenda hii sekta..
Dah kweli wewe hucheki na wowote umetisha Sana kaka
 
Eeee Kaka na sio sehemu zilizojificha napenda ninapoonekana na wengi yaani karibu na geti la kuingilia maboss wote na wafanyakazi wote yaani nawachanganya Ila Siri ni tuzo Kaka .
Maana nilikaa nikawa naangalia sebuleni Sina picha za heshima na pia kwenye vyeti vyangu ninavyo vya shule tu sikuona hata cheti Cha appreciation Wala kutambuliwa nikaogopa siku watoto watauliza baba wewe kazini hakuwa na bidii yoyote ikabidi nipambane kaka
....wataanza kuhisi UNAFANYA KAZI NYINGINE hapo...na kama sivyo jiandae kurogwa na MFAWIDHI kwa kuhisi utampindua ufawidhini ....yakikushinda nitafute nikupeleke kwa babu yangu CHOKOCHO....ha ha ha ha
 
Hapo ndio watu wataanza kutofautisha ndoto na mipango
Ok nimekusoma mkuu..so Mimi LENGO langu niwe na kuku around 100 ila plan zangu ni kuongeza walahu kila mwezi kuku hata wanne wakubwa hasa napoenda vijijini huko..so sijaona sababu ya kutowasimulia watu kwani katika stori wengine inatokea wanakupa ujuzi hata kama watakuwa ni watu wabaya sidhani kama watakuwa kukuathiri kwamba wakuloge kuku au wawaibe..wataiahia labda kuwa na chuki tu
 
Kwa hiyo unawasimulia watu wa kijijini kuhusu kuku 27 ili utekelezaji uje kuufanya hapo mjini ?!!
 
Ni kitu kinachoeleweka kwa kila mtu hakukuwa na sababu ya kuandika uzi tena mrefu kama nini?😀😀😀
Haujajua jinsi ambavyo kwa weeengi hili somo ni jambo ambalo halijawahi kukatiza akilini na kila siku inaharibika (au kufigiswa) mipango, acha aelimishe.
 
Nilitangaza hovyo hovyo kwa kila mtu nimeagiza gari oooh nimeagiza gari! Mbona nilishindwa kulikomboa na pesa nilikuwa nayo iliisha mdogo mdogo zingine ndugu walikopa siku ya kulipa kodi imefika wanarudisha elf 50 kwa mtu uliyempa laki tatu! We acha kabisa. Ningenunua gari langu kimya kimya likija si wangeliona tu! I was very stupid though umri ushasogea
 
Kwa hiyo unawasimulia watu wa kijijini kuhusu kuku 27 ili utekelezaji uje kuufanya hapo mjini ?!!
Sijui kama umenielewa ila anyway nachokiona ni kuishi na watu vizuri na kutowafanyia ubaya..basi ila riziki yako kama ipo itakuja tu usimulie ama ukae kimya kama hela ya kupata gari 2025 ili kuwa ikufikie basi lazima itakufikia tu.

Nataka nijue kwenu kwa mfano umesimulia watu una tamani 2025 upate gari na baadae HATIMAYE ukalipata je wakikuona una endesha kwamba watakuja kukuhujumu kwa sababu tu uliwasimulia
 
Nilitangaza hovyo hovyo kwa kila mtu nimeagiza gari oooh nimeagiza gari! Mbona nilishindwa kulikomboa na pesa nilikuwa nayo iliisha mdogo mdogo zingine ndugu walikopa siku ya kulipa kodi imefika wanarudisha elf 50 kwa mtu uliyempa laki tatu! We acha kabisa. Ningenunua gari langu kimya kimya likija si wangeliona tu! I was very stupid though umri ushasogea

Pole Sana Mkuu
 
Sasa hivi nawahi kazini kuliko mfanyakazi yeyote na pia Kuna muda mpaka nawasaidia wadada wa usafi kufanya usafi ,Siri ni kuwa nataka nipate tuzo ya mkoa ya mfanyakazi bora .
Alafu hata sijamwambia mtu Ila nimeona nguvu ya kuficha Siri naona mpaka mfawidhi kachanganyikiwa kuhusu haya Mambo yangu ,Sasa hivi Kuna muda anapiga jioni eti kuniuliza kazi za siku nzima zimeendaje na Mimi namwambia kila kitu hata Kama Kuna waliowaomba wagonjwa rushwa sifichi ng'o mpaka niwe mtumishi bora wa mwaka nipate Cha kuwaringishia wanangu huko uzeeni .

Haya maajabu yamekuwa kwa wafanyakazi wenzangu maana walishanizoea kuchelewa kazini na pia kuja nikiwa nimelewa Ila kwasasa nimekuwa tofauti hakika nawachanganya Sana .

Itoshe kusema Mtibeli uko sahihi Sana ,siku nikipata tuzo ya mtumishi bora nitakusimulia itakavyokuwa

Ukipata UTUMISHI Bora lazima tule nyama choma Mkuu
 
Back
Top Bottom