Ujasusi wa kiuchumi na Yeriko Nyerere is real!

Ujasusi wa kiuchumi na Yeriko Nyerere is real!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Angalia mfano huu than connect dots, kwa kuangalia kitu kinachoitwa ujasusi wa kiuchumi.

1. Mimi ni Dubai ninataka kucontrol usafirishaji majini kwa Africa,

2. meli nyingi zinazotoka china kuja africa huwa zinapitia bandari yangu,

3. kuna uwezekano meli nyingi toka china zikapita bila kutoa kwangu moja kwa moja hadi Oman then Africa, hivyo nitakosa soko la bandari,

4. nimesikia wachina kwa kushirikiana na Oman wanataka kujenga bandari bagamoyo ya takriban USD 10billion ambapo wachina watafanya bagamoyo kuwa dubai ya Africa,

5. Oman pia itafaidika kwasababu meli zikitoka China zitatua kwanza Oman then zinakuja Bagamoyo kama lango kuu la Africa hivyo Oman watamreplace Dubai kam alango la Africa,

6. Dubai anaona kumbe Oman na Bagamoyo watanireplace...., anaamua kuvuruga na kutia sumu dili la wachina kwa ujasusi wake then linafeli,

7. Wachina na Oman hawakusema wanataka kucontrol bandari zote nchini kwetu tusiendeleze ila Bagamoyo tu, ila Dubai yeye anataka tusifanye kingine chochote ili yeye awe ndio ameshika mpini wa usafirishaji wote nchini kwa njia ya maji.(ananyang'anya sovereignity yetu kabisa)

8. baada ya kufeli kwa dili la China & Oman, anaingia mkataba na wabongo kuendesha bandari ya DSM ambayo tulishaijenga na ilikopewa trilioni moja na ushee kwa maboresho deni tutakalolipa wabongo yeye akilifanyia biashara,

9. anatupiga stop hakuna kujenga au kuendeleza bandari zingine zozote za maziwa makuu au bahari bila ruhusa yake, manake pale pale dsm port palivyo padogo ndio patumike.

10. hakuna kujenga bagamoyo wala kokote, after all amekabidhiwa kama zawadi bandari zooote za maziwa, mito na bahari.

11. wabongo wanakubali kugawa mkopo pamoja na bandari zote, na dubai anaibuka mshindi kwa kucontrol bandari zote za africa na kutuendesha apendavyo, na mkijaribu kuvunja mkataba atawanyoosha.

12. ili kutufanya tuamini kwamba hakuja Tanzania pekee au kwamba tukimkataa Tanzania ataenda kwengine, anarusha yale mapicha kwenye mnara, ya Kenya na Uganda ili tuone gere tuseme kenya wasije wakachukua hilo dili, kumbe kaweka ndoana anayewahitaji ni sisi wala sio kenya wala uganda.

Yeriko Nyerere msimchukulie poa, vile vitabu vyake vinaongea mambo ya uhalisia kabisa.
 
Kumbe Oman kule kwa wajomba, walikuwa wanakuja kuwa ndio vinara wa bandari kama lango la kuingilia Africa ukitoka china, meli zingetoka moja kwa moja China, zinapita Oman then Bagamoyo ambako Wachina na Oman walishaingia makubaliano ya kuijenga hivyo bandari ya Bagamoyo.
 
Unafikiria kazi ya Ujasusi ni kulinda chama tu kiendelee kutawala na kusikiliza umbea kwenye mabaa na kutishia raia mitaani?

Ujasusi ni pamoja na kulinda mipaka ya nchi kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni nk, Matumizi mazuri ya ujasusi na majasusi huboresha pia maisha ya watu na ustawi wa jamii ya nchi husika.
 
Umaskini unachangia umaskini na ubinafsi kuongezeka.
 
tumepigwa jiwe zito
20230615_104559.jpg
 
Unafikiria kazi ya Ujasusi ni kulinda chama tu kiendelee kutawala na kusikiliza umbea kwenye mabaa na kutishia raia mitaani?

Ujasusi ni pamoja na kulinda mipaka ya nchi kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni nk, Matumizi mazuri ya ujasusi na majasusi huboresha pia maisha ya watu na ustawi wa jamii ya nchi husika.
sasa hapo upo upande gani? manake ndicho walichofanya dubai, kulinda uchumi wao wa bandali ilikuwa lazima waje washike masikio maeneo shindani yote, maeneo shindani kwa meli zinazokuja Africa ni Tanzania na Oman ambao wlaikuwa wameingia mkataba na china kujenga bagamoyo port. au ulikuwa umemaanisha nini ili ueleweke?
 
Umaskini unachangia umaskini na ubinafsi kuongezeka.
wabinafsi ni wale wanaouza nchi kwa maslahi ya mfukoni. ipo wazi dubai wanaogopa meli zisije kuhamia Oman na Tanzania moja kwa moja bila kupitia kwao, yaani hadi waarabu wametuzidi ujasusi? mwarabu?
 
Back
Top Bottom