Ujasusi wa Kiuchumi unavyombeba Bakhersa Group

Ujasusi wa Kiuchumi unavyombeba Bakhersa Group

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Vyombo vingi vya Afrika mwaka 2015 viliripoti mgogoro wa kibiashara nchini Rwanda, na pengine vyombo vya Tanzania havikuipa uzito habari hiyo kutokana na mazingira na wakati, ikizingatiwa mwaka na mwezi huo tulikuwa kwenye mchakato wa Uchaguzi mkuu, na aina ya mgogoro uliogubikwa ujasusi zaidi.

Makaka ya Gazeti la The New Times la Rwanda tazama hapa> Tanzanian investor to challenge court ruling in trademark dispute iliyoandikwa na kuchapishwa February 23, 2015 na mwandishi wa habari za kiuchunguzi Bwana Kenneth Agutamba, inaeleza mkasa mkali wa kibiashara kati ya makapuni makubwa ya uwekezaji nchini Rwanda ambayo ni Bakhresa Group na Mikoani Traders Ltd ambao ulitokea nchini Rwanda kuanzia mwaka 2009 hadi 2015

Kampuni ya Bakhresa Group na Mikoani Traders Limited ni kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati ambazo hujishughulisha na uzalishaji wa bidhaa za vyakula kama unga wa Ngano na Mahindi na kila mmoja anafanya namna kushika soko zaidi.

Kwa hiyo bila wao kupenda tayari wanakuwa washindani kutokana na bidhaa wanazo zalisha, Bakhresa wao wanafanya biashara chini ya brand ya Azam na wana bidhaa nyingi zinazoendana na jina hilo huku kampuni mama ikiwa inaitwa Bakhresa, Azania pia wana bidhaa nyingi zinazoenda kwa jina hilo huku kampuni tanzu ikiitwa Mikoani traders Ltd (company and business names)

January 2009 Bakhresa grain milling Ltd ilisajiliwa Rwanda ikiwa na lengo za kuzalisha unga na kusambaza katika nchi za Congo, Burundi na Rwanda ambapo walipata eneo kwenye special economic zone pale Kigali na kuanza uzalishaji May 2011 huku wakizalisha tani 12k ujanja kuwahi bwana, pengine wanaongozwa na majasusi waliobobea.

Mikoani Traders nao hawakubaki nyuma Aug 2011 Mikoani Traders walifanikiwa kusajili biashara yao Rwanda chini ya jina tanzu la Mikoani traders ltd ili baadae wafanye biashara kwakutumia Brand ya Azania na baada ya usajili walipata eneo kwenye special economic zone na wakaipa kampuni ya Questafrica kazi ya kujenga factory yenye kuzalisha tani 750/day

Wakati Mikoani wanaendelea na usajili waligundua kuwa jina la Azania lilikuwa limeshasajiliwa na kuchukuliwa na mtu mwingine nchini Rwanda na walipofuatilia waligundua kuwa aliesajili na kupata hakimiliki ya jina la Azania nchini Rwanda ni Bakhresa tangia 2009.

Kwahiyo mojakwamoja wao wakizalisha bidhaa zao hawataweza kutumia jina la Azania nchini Rwanda na endapo watatengeneza brand nyingine basi ingekuwa ni gharama sana kulitangaza. Basi wakaamua kwenda mahakamani kudai fidia, kutokana na figisu hiyo baada ya mazungumzo ya kawaida nje ya mahakama kushindikana.

Wanasheria maarufu nchini Rwanda wakaidaka hii kesi ya matajiri hawa, Mikoani traders walimchukua Godfrey Mwina na Bakhresa alimchukua Safari Kizito na kesi Ilianza Kunguruma pale Kigali Nyarugenge Commercial Court January 8, 2015 ambapo Mikoani wawanadai dola laki tatu na sitini elfu ($360k) sawa na TZS 830mil kama hasara ya kuchafuliwa jina ama "consequential demage"

Mwanasheria wa Bakhresa akasema kuwa Mteja wake ana haki na hajavunja sheria kwani alijilinda protect na kusajili jina ambalo Kwa Rwanda lilikuwa halina mtu na siku jina hilo linapata usajili Rwanda jina la Azania

Kwa Tanzania lilikuwa imeisha muda wake na lilihitaji kuhuishwa, Mahakama ikasema Afrika Mashariki hakuna mikataba kuhusu ulinzi wa majina/ nembo za kibiashara kwa nchi wanachama na hivyo Bakhresa alikuwa na haki ya kusajili jina analolitaka kwakuthibitisha kama lilikuwa halina mtu au laa nchini Rwanda. Hivyo Mikoani hawakuwa na ulinzi wa jina hilo kwa Rwanda ama kwingineko duniani baada ya kuisha muda wa umiliki wa jina hilo Tanzania.

Kwa hiyo Bakhresa akashinda kesi huku Azania akiugulia kwa machozi ya kupoteza biashara na uwekezaji mkubwa. Ukisoma Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi sura ya tano ukurasa wa 609 kisa hiki kinafafa na kisa cha mgogoro wa kampuni ya Samsung kule Korea Kusini.

Na mwaka huo huo tayari kampuni hizo mbili zilikuwa zinafukuzia Mkopo wa $24mil kutoka IFC. Ambapo Azania alikuwa na nafasi kubwa ya kuupata lakini alishindwa na mkopo ukaenda kwa Bakhresa kwa sababu alikuwa ameshasajiliwa na kuanza operation zake Rwanda hivyo Bakhresa aliliteka soko vizuri sana Congo, Burundi, Rwanda na Afrika ya Kati.

Bakhresa alitumia uzembe kidogo wa kampuni ya Mikoani kwani ilisajili jina la "Azania" nchini Tanzania January 2001 na kupewa usajili wa miaka 7 tu, na expire yake ilikuwa January 2008 na kwa uzembe hawakuhuisha mpaka July 2014 na pia Bakhresa walicheza na sheria ya Tanzania trade/service marks act of 1986 na wakafanikiwa, Kama huelewi kasome kitabu cha Ujasusi wa kidola na Kiuchumi kujua zaidi maana ya Ujasusi wa Kiuchumi.

Habari hii ya Bwana Keneth Agutamba ilichapishwa pia katika mtandao maarufu Afrika wa All Africa tazama > https://allafrica.com/stories/201501140725.html pia nimefurahi kuona baadhi ya vijana wa kitanzania wanaufahamu vizuri mgogoro huu hasa bwana Octavian Lasway amekuwa akitoa dondoo za hapa na pale hali inayoleta matumaini kwamba vijana hatuko nyuma sana kufuatilia yanayojiri Duniani.

Kisa hiki kinafanana sana na namna ujasusi uliotumiwa na Kenya wakati wa uwekezaji wa TBL na Serengeti Breweries Limited, na namna chenga za visigino na sambusa zilivyokuwa zikikatwa hadi Nairobi ikawin games.

Jambo muhimu ni kuwa unapotaka kuwa mwekezaji na hata unapokaribisha mwekezaji unahitaji kuwa makini sana na huu ndio msingi hasa wa mimi kuandika Kitabu cha Ujasusi wa Kidola nikikusudia kuweka msukumo wa uhitaji wa mageuzi ya lazima ya Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), Kuna mambo ya msingi manne au matatu ndio hutazamwa na mwekezaji kabla hajaweka pesa yake,

Mosi huwa ni Political risk: hapa wanaangalia sera za nchi unayotaka kuwekeza, muundo wa utawala, demokrasia, na mambo kadhaa wa kadhaa yanatokana na madaraka ya kisiasa. Zingatia matamko yoyote katika nchi sio sera, sera huwa katika maandishi na hazibadiliki hovyo.

Pili ni Inflation: Mfumko wa bei ni moja ya kigezo kikuu cha mwekezaji yoyote, Hapa hutazamwa kwa umakini hasa katika ununuzi wa malighafi, gharama za ubadilishanaji na usafirishaji wa pesa (Transaction) nk.

Tatu ni Usalama; Baada ya mambo ya hapo juu ndio hili hutazamwa kwa umakini mkubwa, lakini hili maranyingi huwa kigezo kikuu kwa mtu anayetaka kuwekeza katika nchi zilizostarabika. Kwa Afrika usalama ni ishu ndogo, Somalia, Congo, Sudani nk biashara za uwekezaji zinaendelea vizuri tu.

Nne ni Miundombinu: Barabara, Viwanja vya ndege, Bandari na Reli ni mojawapo wa mahitaji ya mwekezaji.

Tano ni Uwezo wa Soko la Ndani. Hili huwa la mwisho pia kulingana na aina ya uwekezaji unaoufanya, mfano kama ni biashara ya madini, basi hutategemea soko la ndani zaidi.

Sita: Nyongeza ni kutazama madhaifu ya sheria ili uweze kuwashinda washindani wako wa ndani na nje , jua sera na sheria zinazoendesha biashara yako, compliance ni muhimu sana Kwa biashara, Behavior ya idara/taasisi za ujasusi za nchi husika ni muhimu saba kujua na kuziishi.

Mwekezaji mkubwa nchini Tanzania Kijana machachali Joseph Mbilinyi maafuru kama Sugu anazujua vema rules hizi na amefanikiwa kusimamia kampuni kubwa kabisa kusini mwa Afrika kwa sasa ya Desdery Group ikisimamia Hoteli ya nyota tano ya Desdery Hotel. Sugu anabaki kuwa mfano bora kwa sisi vijana tunaoota kufikia mafanikio ya uwekezaji aliyofikia yeye na zaidi.

IMG_20200210_123611_632.jpg
 
Losers wakubwa sio Mikoani Traders, bali ni Rwanda kwa kubariki anti competition practice. Kwanza wanazuia price wars kati ya hao washindani ambapo faida ingeenda kwa walaji, wanabariki kukosesha vijana ajira kwa kuzuia kampuni mpya kuingia na kujinyima mapato ya kodi.

Simply ni bad decision from Rwanda government, mtu awezi kusajili brand ya mwenzake kwa lengo kumzuia kuingia sokoni na wewe ukabariki that’s just a bad business policy.
 
Losers wakubwa sio Mikoani Traders, bali ni Rwanda kwa kubariki anti competition practice. Kwanza wanazuia price wars kati ya hao washindani ambapo faida ingeenda kwa walaji, wanabariki kukosesha vijana ajira kwa kuzuia kampuni mpya kuingia na kujinyima mapato ya kodi.

Simply ni bad decision from Rwanda government, mtu awezi kusajili brand ya mwenzake kwa lengo kumzuia kuingia sokoni na wewe ukabariki that’s just a bad business policy.
Mikoani traders inabidi wasajili jina lingine na kuanza kuijenga brand hiyo.
Tambu la uwepo wa sheria
 
Du! hapa hukusema kuwa unga wa Azania unauzwa Rwanda toka kiwanda kiko Mwenge late 1990's. Hii ni sawa na case ya Acacia na Inayoitwa Twiga tofauti later walikuwa wanazungumzia Kahama Gold Mine Ltd na North Mara Gold Mine (Hii Migodi iko vile vile tu) sarakasi zilikuwa mbwembwe tu za watawala.

Azania unga unauzwa Kigali, majasusi wapya nendeni na field kupunguza bookish katika story. na kama huu ni ujasusi basi mara 800 ule wa Willy Gamba.
 
Mikoani traders inabidi wasajili jina lingine na kuanza kuijenga brand hiyo.
Tambu la uwepo wa sheria
Sijabishia uwepo wa sheria, isipokuwa ni sheria mbovu inayo promote monopoly and anti competition practices.

Lengo la patents ni kulinda intellectual property au creativity which introduces new ways (the latter is very hard to protect today) lakini sio kutumiwa kuzuia rival competition kuingia kwenye soko kwa kuwatengenezea mazingira magumu ya makusudi na serikari husika ikulinde kwa sheria.

If anything alichofanya Bakhresa is bad for Rwanda competition market if you look at the whole thing from economic point of view; serikari makini aiwezi bariki vitu kama ivyo.
 
Iyo technic wameitumia Google na wameweza kushinda kununua domain zote za nchi husika,kwaio hhakuna mtu anaweza kununua kwa jina lao tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom