Waambie wamshukuru Mungu na awaombe awaongezee baraka maishani, wala sio aibu kabisa huwa inatokea kwa wengi, watoto watapishana kama zaidi ya mwaka.
waambie wasijaribu kutoa huyo anaweza akawa wa mwisho kwao.
nasema tena aina tabu kabisa hata hapa nchini wengi wana watoto hivyo, watakaowasema wawaambie ni baraka za Mungu na wanashukuru.
sielewi kwanini waone aibu, je wangekuwa hawawezi kuzaa kabisa wangeona aibu pia au ndio wangechekwa, mtu akiwashauri watoe eti karibu sana basi huyo hana mema nao.
I hope na wewe hujawashauri wamuue mtoto huyo tumboni, ni dhambi kaa kimya waambie washukuru Mungu wasubirie mtoto.