Ujauzito wa mke wangu unanitesa

kila jr

Member
Joined
Mar 28, 2014
Posts
28
Reaction score
3
Habarini za asubuhi wana jf,

Mwenzenu nimekuwa katika hali ya mateso ya uchovu usioisha na mara nyingine kutapika kila asubuhi kwa muda mrefu sasa yapata miezi mitano sasa na mke wangu mjamzito naugua lakini ninachougua hakijulikani.

Nimefanya vipimo karibia vyote vya kitabibu lakini hakuna ugonjwa wowote ambao unaonekana mwilini.

Nimeenda mpaka kwa wataalamu wa tiba mbadala hadi kwenye maombi imeshindikana bado hiyo hali niko nayo mpaka inanifanya kutoweza kufanya kazi.

Sasa naomba kuuliza hivi kuna uhusiano wowote ujauzito kumtesa mwanaume?

Naomba mnisaidie.
 
Hiyo kitu hutokeaga kwa mwanaume tena wakati wa kujifungua kwake utapata uchungu wewe
 
Yeah. Ni mimba ya mke wako inaku affect. Kaka una morning sickness.
 
Dawa yake ni kuwa karibu naye kwa siku mbili mfululizo huku mkila kwa sahani moja na kunywa kwa kikombe kimoja.Ukipata nafuu sema
 
Hiyo kitu hutokeaga kwa mwanaume tena wakati wa kujifungua kwake utapata uchungu wewe

Yan aisee nateseka sana jaman hapa natuma hii thread nko kwa mganga wa tiba mbadala karibia wiki ya pili sasa wanasema nina majin nisaidien jaman
 
Yeah. Ni mimba ya mke wako inaku affect. Kaka una morning sickness.

Sasa kuna uhusiano gan jaman au nikamtoe maanake nashindwa kufanya hata kazi kwa raha jamani alafu yeye yuko poa tu hata haimsumbui aisee
 
Dawa yake ni kuwa karibu naye kwa siku mbili mfululizo huku mkila kwa sahani moja na kunywa kwa kikombe kimoja.Ukipata nafuu sema

Yan mdau hatuwezi kukaa sehem moja muda mrefu either tutazinguana au atanibore tu yan cjui hii hali itaisha lini jaman starehe zote kwisha yan ni unyonge usioisha aisee
 
Yan mdau hatuwezi kukaa sehem moja muda mrefu either tutazinguana au atanibore tu yan cjui hii hali itaisha lini jaman starehe zote kwisha yan ni unyonge usioisha aisee

Acha ujinga,sasa mbona kila ushauri unakataa? Au unataka comments nyingi tu!? Fanya hivyo nilivyokuambia umalize tatizo. Na utoke wala usirudi kwa huyo mganga wako
 
Acha ujinga,sasa mbona kila ushauri unakataa? Au unataka comments nyingi tu!? Fanya hivyo nilivyokuambia umalize tatizo. Na utoke wala usirudi kwa huyo mganga wako

Asante mdau ila nilikua naomba kufahamu huo uhusiano unakuwaje
 
Yan aisee nateseka sana jaman hapa natuma hii thread nko kwa mganga wa tiba mbadala karibia wiki ya pili sasa wanasema nina majin nisaidien jaman

Hata usijali hiyo hali itaisha hata kwa sangoma usingeenda mbona wanawake wanavumiliaga
 
Hiyo hali ni ya kiasili na haina maelezo yoyote. Fanya hivyo upone

Asante sana mdau kwa ushauri wako manake nakuwa sijielewi kabisa yani kwa hyo mpaka ajifungue ndio nitakuwa poa? Manake anatarajia mwezi wa 9
 
Labda ametunga tatizo.kama kawaida ya Jf

Hapana mdau mimi niko serious na hyo hali nilio nayo kila ninaemweleza anashindwa kunielewa coz siumwi sehem yeyote ya mwili ni uchovu tu usioisha na mara nyingine kuishiwa nguvu sababu ya kutapika na ku loose apetite
 
Vumilia tu unywe hicho kikombe mpaka mwisho...... ili ujue wanawake ni kias gan na wenyewe huchoka haswa ktk kpnd hicho...... ila yatakwisha
 
Yan aisee nateseka sana jaman hapa natuma hii thread nko kwa mganga wa tiba mbadala karibia wiki ya pili sasa wanasema nina majin nisaidien jaman

Basi tena....zishakuwa fix hizi
 
Yan aisee nateseka sana jaman hapa natuma hii thread nko kwa mganga wa tiba mbadala karibia wiki ya pili sasa wanasema nina majin nisaidien jaman

waongo hao hauna majini wala nin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…