Ujenzi bora wa mabanda ya kufugia kuku wa kisasa na kienyeji

akohi

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Posts
787
Reaction score
526
Naombeni munisaidie ukubwa na namna ya kujenga banda zuri la kisasa ambalo linaweza kkufuga aina yoyote ya kuku (kisasa au kienyeji).

Nataraji kuanza na kuku wa kienyeji. Je, nianze na kuku wakubwa au vifaranga? Wangapi?

Ntashukuru kwa ushauri wenu maana naona kweli JF ni mkonbozi na nimeamua kuanza ufugaji mara baada ya kupitia nyuzi mbali mbali zenye kuhamasisha, hongereni kwa nyote mulioanzisha mada na maelezo jinsi faida inavyopatikana.


Majibu kutoka kwa wanaJF


==========

 
Kabanda kangu kako hivi, ninafuga kuku 50





 
Jamani hako kabanda kazuri sana kwa kuku wa kienyeji wa zero grazing yaani wanalala usiku asubuhi unawafungulia si ndio?
Kuku wanaofugwa ndani banda inabidi liwe na madirisha makubwa na yanayotizamana ili kuwezesha hewa kutembea, pia upande wa jua kali yaani magharibi uwe mdogo kuliko upande usiopigwa jua ili wasiadhiriwe na jua kali kiasi kikubwa
mtu kama anataka mfano wa banda google kuna mitandao inayoonyesha mfano wa mabanda ya kuku.
 
Nashukuru wakubwa, walau sasa napicha ya nini kifanyike, nadisign na kujenga then ntalipiga picha mu comment...Asanteni
 
Asante kwa kuomba msaada wa banda la kuku. Majibu yatasaidia wengi maana ufugaji wa kuku uwe hob kwa familia maana nyama nyekundu kwa gauti na upotevu wa madini ya zink so cancer nyingi kwa vibofu. Tuhamasike tufuge kuku wa afya zetu.
 
literature nyingi nilizopitia wana-recommend kuku 18 per square meter (kwa kuku wadogo wa hadi wiki 4) na wakubwa (wiki 4-8) kuku 9 per square meter.umri zaidi ya wiki 8 ni kuku 4 kwa square meter. ila wafugaji wanaweza kutupa experience zao, kama safari -ni safari anaweza kutupa dimensions za hilo banda lake zuri lenye kuku 500
 

layers or broiler au wa kienyeji
 
Nakuwekea mfano wa banda kwa kuku wa kisasa na kuku wa kienyeji au hybrid wanaofugwa ndani


na pia hili kwa kuku wanaolala au kushinda lakini wanatolewa nje



hii ni mifano waweza fanya modification na kutumia vifaa ulivyonavyo mabanzi, matofali, mabati nk
 

Mama Joe hili ndio banda lako? Maan nahisi we ni mfugaji...
 
No no Riwa ni mfano tu tena yapo kwenye mtandao mie nami nimfugaji mfanyakazi si unajua tena, Mungu akipenda nitaweka la kwangu hapa nikipata muda wa kupiga picha
 
Wekeni mtusaidie nasi tunataka kuingia kwa hiyo biashara ya ufugaji, usihofu competition....Tz we are very far from satisfying the chicken demand/market..
 
Muhimu ni kujua kama kuku 500 kwa mfano watakaa kwenye square metres ngapi?
 
Nawashukuru wote walitoa mchango na kuonyesha mfano wa mabanda pia aliye uliza swali.Nami nimepata picha ya kabanda kangu.
 
Mnaouliza ukubwa wa banda ninavyojua kuku wakubwa wa mayai 7-9 kwa square metre moja na wa nyama 9-10 kwa square metre moja
ina maana kuku mia tano ni banda (500kuku/10)= 50m2 approx 5mx10m au kipimo chochote upate 50m2 hii kwa broiler
layers kwa sababu ya viota na pia sababu wataishi muda mrefu wanahitaji space zaidi kuweza kufanya mazoezi (hawahitaji uzito mkubwa)
kuku 500/9 = 55.5m2 approx 5mx11m
ila ngoja wengine waje watoe ushauri zaidi
space pia inategemea mzunguko wa hewa, kama huna space au umebanwa usijaze kuku ili kuepuka vifo kwa magonjwa yanayoambukizwa kwa hewa. All the best
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…