Ujenzi bora wa mabanda ya kufugia kuku wa kisasa na kienyeji

Kwa kuku wa kienyeji.....ufugaji mzuri ni wa nusu huria kwa maana ya usiku wanalala bandani mchana nje.
Kwa kuanzia vyumba vitatu: 1: mita 3 (kuku wanaoanzia miezi 2 na kuendelea) 2: mita 2 (kwa mitetea wanaoatamia) 3: mita 2 (kwa ajili ya vifaranga ambao watahifadhiwa kwa kutumia joto, liwe la umeme, maji ya moto kwenye dumu n.k).

Linatakiwa kuwa na madirisha mbele yenye ukubwa kama wa futi 2 kwa kila chumba na mlango unaokuwezesha kuingia bila vikwazo..............Urefu wa banda kama mita 3 tu zinatosha kwa maana kwamba unaweza kuingia na kufanya usafi bila tatizo.

Kumbuka kuku ni ndege kwa hiyo unaweza kupitisha fito pembeni ili wanaotaka kulala wamening'inia wasipate shida. Chini weka pumba za mpunga au maranda ya mbao kuabsorb kinyesi ili kupunguza bakteria.

Kwa sababu ni wa kienyeji nje ya banda unazungushia uwa wa waya ili wasitoke lakini wapate nafasi ya kufanya mazoezi, na kula. Banda la aina hii lina uwezowa kuchukua kuku 300.
 

Ndivyo nilivyoshauriwa pia......asante
 
Nshukuruni nyote kwa michango yenu....very useful

www.oric.co.tz, skype: alfred.kohi, 0784800989
 

Platozoom unatisha mkuu, ngoja niku PM....thx

www.oric.co.tz, skype: alfred.kohi, 0784800989
 
Nimetumia mabazi ya mbao na hapo kwenye nyavu wanashinda mchana. HAINGII PANYA WALA KICHECHE

Mzee Safari naona umenipa changamoto nyingine maana sasa naweza ku design lAngu kwa muundoo huo huo ...ntaleta picha likikamilika....thx

www.oric.co.tz, skype: alfred.kohi, 0784800989
 
mliohaidi mtaleta picha mabanda yakikamilka, bado hamjamaliza kujenga?????
 
Usijari mkuu, mi ndo nimeanza ujenzi, by end of next week naleta picha hapa.


founder and CEO of www.oric.co.tz and www.aio.co.tz skype: alfred.kohi, 0784800989, 0715800989
 
Nimependa ushauri wako Mama Joe, kweli mambo haya wayajua mpaka natamani ungekuwa jirani yangu nikufate unipe ushauri zaidi kabla sijaanza mradi huu ambao watu wengi wananitisha kuwa una risk nyingi ila nina tabia ya kutokuogopa hasara kama jambo nilifanyalo nalijua vizuri.
 
Je gharama ya kujenga banda la kuku 200 ni kama ngapi?
 
akohi, wadau tunaomba kufahamu umefikia wapi nasi tujaribu???
Pia tunapenda kufahamu changamoto ulizopitia.
 
Last edited by a moderator:

Jaribu kutembelea site za majengo makubwa......huwa wanauza used materials kama mabati ya fence, mirunda na mbao za kumwagia zege.....utapunguza sana gharama

what a nice idea for cost minimazation
 
mkuu Chasha wewe huna banda? tuwekee bana!

Ninayo ila sijayapiga Picha, Mambanda kwa ujmla hayana Formula maalumu ya Kujenga, ni Ilimuradi yakidhi vigezo vya kutunzia kuku kama maswala ya usafu, panya wasingie, hewa ya kutosha, mwanga, na yasiwe kwenye sehemu za mikondo ya maji,
Ila kwenye ramani wapo wanao jenga ya Mviringo kama nyumba za Msonge, wapo wanao jenga ya Full suti Bati chini na juu, wapo wanajenga na kuezeka kwa makuti, wapo wanotumia Udongo kujengea, nahayo yote hufaa kulingana na maeneo ulipo,
 
Chasha ukipata chance tuwekee bana we can learn something kutoka kwako mkuu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…