Ukinipa M 143 nakuletea nyumba kama hiyo mbili na vimilioni vichache vinabaki.
Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Na hapa kuna washauri/consultants lukuki
Mfano.. Quantity surveyors
...architects
....structural Eng
Na kadhalika na hawa wote wanalipwa ghali, hapa bado hujajua finishing ya ndani na SAMANI zake.
Msiwe mnakurupuka bila kuwa na ufahamu sahihi
Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani