Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Hiyo nyumba tuseme kupaua ni milioni 10
Msingi na jamvi milion 10.
Kupandisha tofali juu milion 10
Finishing milion 15
Ziada milini 10.

Jumla milioni 55!

Magu yupo sahihi hapo pana upigaji!

Kwa hiyo hela milioni 143 ilitakiwa zitoke nyumba kama hizo 3
 
Ila kumbuka huwez jenga nyumba ya taasisi ukasupervise kama yako, hii inaenda na wataalam, tofali hadi upeleke maabara, zege pia, i bet kwa construction process halisi zikifuatwa hii nyumba inafika 110mil.
Kumbuka kila kitu kinatakiwa kiwe standard
Hawajui kuwa hata nondo, mchanga, kokoto hupelekwa maabara na vipimo vyake ni ghali sana
 
Ila kumbuka huwez jenga nyumba ya taasisi ukasupervise kama yako, hii inaenda na wataalam, tofali hadi upeleke maabara, zege pia, i bet kwa construction process halisi zikifuatwa hii nyumba inafika 110mil.
Kumbuka kila kitu kinatakiwa kiwe standard
You are right.
Kwa ujenzi wa mitaani hiyo nyumba inacheza kwenye milioni 80.
Ila kiserikali kuna milolongo mingi inaweza kufika milioni 110
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Mi naomba kuuliza kwanini majengo yote ya serikali yasiwe yanafanana? Kama ni ofisi ya TAKUKURU yafanane nchi nzima. Kama ni la hamlashauri hivyi hivyo. Kwa nini kila wilaya/mji majengi ya ofisi ya taasisi moja hayafanani?
 
Hiyo nyumba finishing yale ni kali sana.. inaweza fika hata mil.150.

Pia bati naona kama geji 28 ambazo ni gharama sana. View attachment 1514090[/QUOTE]
FB_IMG_1595429360203.jpeg
FB_IMG_1595429357230.jpeg
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Hii imezidi sana bila ya bei ya kiwanja ni milioni sabini
 
Hujui lolote mkuu na ukubali hilo.
Hiyo ni nuumba ya serikali huwezi kujenga kwa gharama hiyo.
Dodoma baadhi ya vifaa vya msjenzi ni ghali sana tofauti na dar.
Pili hivi unajua hiyo gharama ni pamoja na thamani zake za ndani?
Unajua kuna vyumba vingapi?
Unajua wamerumia tofali za gade gani?
Unajua tofali zimelazwa au kusimamishwa?
Unajua marumaru zimetolewa wapi...Spanish au India?
Tujifunze kuhukumu kwa haki wakuu
mm siwezi tetea uizi, dodoma naielewa vizuri sana, zungukaaa maneno mia ila hiyo nyumba haiko na viwango tajwa. na mm pia nimejenga nyumba nzuri sana yenye hadhi kwa thamani ndogo tu..ndani ipo full, huwezi linganisha na hiyo kwa thamani yenu
 
Hiyo nyumba tuseme kupaua ni milioni 10
Msingi na jamvi milion 10.
Kupandisha tofali juu milion 10
Finishing milion 15
Ziada milini 10.

Jumla milioni 55!

Magu yupo sahihi hapo pana upigaji!

Kwa hiyo hela milioni 143 ilitakiwa zitoke nyumba kama hizo 3
Mkuu ujenzi wa serikali huendagi hivyo.
Kuna consultant...architect
Kuna consultant....structure
Kuna consultant.....BOQ
hawa wote wanalipwa na huenda wao pekee wamekula 30ml kabla hujalipa mjenzi.
Hiyo 40ml yenu huenda ni gharama za ujenzi pekee
 
Unapozungumzia mali za serikali sio kama zetu mtaani,kwanza serikalini awaruhusu kujengea kitu kisicho kipya,watu wa manunuzi wanaelewa.

Pili,kuna bei elekezi za ununuaji vitu hasa kama wametumia mfumo wa tender,Mfano kalamu unayonunua wewe 300 bei ya kimanunuzi kwa serikalini unaweza kuta ni 500,hata ikishuka au ikipanda kama tayari upo kwenye mkataba wao watanunua kwa bei hiyo hiyo.

Note:sidhani kama nimeelezea vizuri ila nadhani utapata nilichokuwa nafikiria.
 
Ila kumbuka huwez jenga nyumba ya taasisi ukasupervise kama yako, hii inaenda na wataalam, tofali hadi upeleke maabara, zege pia, i bet kwa construction process halisi zikifuatwa hii nyumba inafika 110mil.
Kumbuka kila kitu kinatakiwa kiwe standard
Mkuu unajitetea sana .Huku mtaani hata kama hatukusoma lakini majengo ya serikali hasa yaliyojengwa miaka ya hivi karibu ni majengo yenye ubora duni sana. Kwenye hilo la Takukuru kuna shida hapo.
 
Hiyo Nyumba kwa thamani ya ml.90 inaweza kufika. Maana msingi pamoja na jamvi si chini ya ml 10.
Sasa kama msingi na jamvi tufanye mil 10,kwenda na tofali mpaka lenta mil 10,lenta na tofali za juu mil5,roofing mil 10,gypsum na rangi mil 10,tiles na umeme mil 10,mfumo wa majitaka mil10,finishing nje mil 10.unapata mil 75,hapo nimekadilia tu kwa kiwango cha pesa ambacho ni juu sana,sasa hizo mil 143 kwa nyumba ya kawaida sana kama hiyo unanunua material gani ya ajabu?,wizi tu hapo.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
hii inaitwa mbuzi kafia kwa muuza supu
 
Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano. View attachment 1514090
Du, Takukuru wanajua kutafuna kuku!
 
Back
Top Bottom