Ujenzi kutumia Interlocking blocks

Kuhusu gharama za tofali hizi naona kama hazina bei ambayo ni constant, kuna wengine jimeona wanaziuza 500 kwa tofali moja lenye ukubwa wa 300mm x 150mm x 100m, gharama za udongo na cement ikiwa juu yao wewe unafyetuliwa tofali zako hapohapo site
Je hii 300 x 150 x 100 inayouzwa TZS 500/= ni sehemu gani ya tofali la kawaida la Block linalouzwa TZS 800/=??
 
Nashukuru sana nimeanza kupata mwanga, kama bei ni 500 it's reasonable ukizingatia unaokoa gharama za exterior finishing na hata ukipenda interior bado inapendeza sana.

Nakaribisha maoni na ushauri zaidi
 
Ni Dar? Ni sehemu gani? Naomba kujua
 
Je hii 300 x 150 x 100 inayouzwa TZS 500/= ni sehemu gani ya tofali la kawaida la Block linalouzwa TZS 800/=??
Mkuu sijajua, ila tofali zile nyepesi kwa mahali nilipo zinauzwa around 850.
 
Interlock kwa mujibu wa mtaalamu fulani aliniambia wanatumia udongo wenye asili ya ufinyanzi kwa kuchanganya na cement udongo huo hupimwa maabara kwanza kabla ya kufanyiwa kazi.

Ni tofali ngumu na hukaa/hudumu kwa muda mrefu kuliko block

Zinahimili hali ya hewa na majanga ya tetemeko lakini pia ikitokea unahama unaweza kuhama nazo kwa kufumua nyumba bila shida na kuzijenga upya sehemu nyingine.

Mwisho wenyewe wanasema zina gharama ndogo kwa sababu hazihitaji plasta so cement hutotumia ila kuangalia kiundani hazipishani sanaaaa.... Gharama ya cement inafidiwa kwenye tofali, zitahitaji polish yake pia kila muda fulani.

Ni hayo tu
Mkuu kama unawafahamu share nasi ulichojifunza. Ugumu upo kwenye kumpata mtu anayefahamu huu ujenzi kiundani
 
So kwa ndani ya nyumba hakuna haja ya kupiga plaster?
 
Ni tofali nzuri sana hizi, nyumba inavutia na inakuwa unique. Kenya wanaifanya sana hii kazi sijui tufuate mafundi huko? halafu tukiwaleta tz makandarasi wanaanza kulalamika, hili ni jukwaa la ujenzi na kila siku zinakuja post za kuuza ramani nk ila swala hili wengi tuna interest lakini hakuna msaada wowote kutoka kwa wataalam
 
Vipi likitokea kwa mfano tetemeko la ardhi zina ustahimilivu ukoje?
 
Nimesubiri majibu kitambo sana kuhusu gharama za tofali na ujenzi. Ninataka kujenga eneo ambalo lina udongo mzuri wa kufyatulia. Kama kuna wafyatuaji, Je bei ni kiasi gani kwa tofali, kama tatizo ni mashine naweza kugharamia kukodi au kununua.
Ndg watafute Ujenzi Empire kwa no. 0716 023 456, pia ingia instagram "interlocking_bricks" utapata maelezo yote,
 
Hyo bei ya wapi? Namaanisha dar au mkoa kwingine?.
Usije ukafananisha bei na Yale matofali ya kuchoma
Ukitoka Mlimani city kwenda Mwenge baada ya petrol station ya Oil com kuna kiwanda cha Serikali/Wizara ya ujenzi hizo tofari zimejaa tele unabeba tu bei ni TZS. 500 kwa moja au wapigie Ujenzi empire 0716 023 456 karibu
 
Ukitoka Mlimani city kwenda Mwenge baada ya petrol station ya Oil com kuna kiwanda cha Serikali/Wizara ya ujenzi hizo tofari zimejaa tele unabeba tu bei ni TZS. 500 kwa moja au wapigie Ujenzi empire 0716 023 456 karibu
Hiyo ni kwa hapa Dar es Salaam mikoani sifahamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…