Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Hii ni kujisahau. Unapata hela unaweza kulipa Kodi popote unaona huna umuhimu wa kujenga 'nje' ya mji. Siku unashtukia mrija wa pesa umeziba ndio unaanza kujuta.
Mfano yuke mama wa zenji imenisikitisha na inatia huruma, mume wake alikua na kazi serikalini wakawa wanakaa kwenye nyuma ya serikali mume wake kafa akalazimishwa kutoka kwenye nyumba kinguvu, sasa wakati wanamuhoji anasema hajui pakwenda waende wapi inasikitisha sana
 
Nilikuwa nawaza sana suala la ujenzi. Nikishaenda kwa architecture akanichorea ramani moja tamu sana ila nilipopiga hesabu nikagundua ile nyumba ili niikamilisha basi itanipasa kupambana na kuitesekea sio chini ya miaka 10.

Basi nikaona isiwe kesi nikamchukua fundi tukaenda site last week tukapima nikamwambia aniwekee kijumba changu cha room 2 na sebule tu.

Leo hii nafunga lenta na wala haijaniumiza sana kiasi hata cha kuathiri biashara zangu. Na finishing pia sioni hata dalili ya kuja kunitesa na nina uhakika Mungu akipenda basi nitaikamilisha hata ndani ya mwaka huu

Sent using Jamii Forums mobile app
Vizuri sana.
 
pana dada mmoja ukiangalia kodi anayolipa hapo anapokaa kama angeamuwa kupanga nyumba ya uswahilini bei nafuu basi angekuwa ameshaanza ujenzi
na pili anataka kujenga nyumba kubwa wakati uwezo hana namwambia jenga kwanza ya wastani ili kujihifadhi ,hasikii
Shida hiyo boss, inasikitisha halafu watu wa hivyo huwa hawashauriki, ndiyo tunakuja kwenye point kuwa kujenga ni mipango, mtu mwenye akili anaanza mdogo mdogo unashangaa umemaliza,
 
Mfano yuke mama wa zenji imenisikitisha na inatia huruma, mume wake alikua na kazi serikalini wakawa wanakaa kwenye nyuma ya serikali mume wake kafa akalazimishwa kutoka kwenye nyumba kinguvu, sasa wakati wanamuhoji anasema hajui pakwenda waende wapi inasikitisha sana
Hao ni wengi sana.
 
Ni kweli lakini inategemea kwa mfano kuna nyumba unaweza kuijenga na kwenyw finishing ikawa haikutesi sana.

Kuna nyumba nyingine ukishafika lenta ukiwa na 3M unamalizia ila nyingine inahitaji 30M hawa watu hawawezi kuwa sawa

Sent using Jamii Forums mobile app

3M finishing? Unatumia mbao gani kuezeka na bati za ubora upi mkuu? Hapo haujaongelea madirisha wala lipu. Unaweza kubana unavyoweza ila hiyo pesa ni ndogo. Vinginevyo iwe ni vyumba viwili.
 
Haya unayosema kiongozi ni sahihi ,mimi nimejenga nyumba ya ndoto yangu ila kidogo kidogo ,..

nilichofanya nikuwa na ramani ya anina nyumba nayoitaka ,kisha nikaanza kuinyanyuwa vyumba viwili ambavyo master na nashukuru haikuchukuwa muda sana ,japo nayo imenigharimu kulingana na aina ya ujenzi niliotaka ,
maana nilitaka nijenge nyumba ambayo zitakujutia baadae au kuja kujenga tena ,kwahiyo nilijitahidi kujenga kila kitu katika kiwango bora ,ila kama ningetaka nimalize ramani yote nahisi mpaka yesu angerudi angenikuta nipo kwenye msingi ama linta na sijapauwa sijui napauwa lini
Okey kwahiyo una maana ulianza vyumba vichache kupandisha boma, au kwenye finishingi ulichagua vyumba vichache
 
Shida hiyo boss, inasikitisha halafu watu wa hivyo huwa hawashauriki, ndiyo tunakuja kwenye point kuwa kujenga ni mipango, mtu mwenye akili anaanza mdogo mdogo unashangaa umemaliza,
Mkuu kama ulikuwepo hashauriki maana ilifika wakati mpaka tunagomba nikabidi kumuacha maana yeye anataka mambo makubwa anadhani pesa huwa zinashukaga na malaika mbinguni ,
Namwambia ujenzi sio rahisi watakiwa ujinyime upunguze matumizi ,yaan ujibane bane kwa hali zetu ndipo ujenge kinyume chake kila siku utaishia nyumba za kupanga ,
Binafsi nilikaza roho nikaanza kujenga taratibu tena nyumba ile nayotaka lkn nilianza mdogo mdogo mpaka hapa nilipofikia sihaba
 
Okey kwahiyo una maana ulianza vyumba vichache kupandisha boma, au kwenye finishingi ulichagua vyumba vichache
Kiongozi nilianza chumba kimoja master msingi nikja onganisha msingi wa chumba cha pili master nikaja msingi wa chumba cha tatu master ,kisha nikaja kunyanya vyumba viwili boma nikapiga linta na kuezaka nikaeka milango nikahamia nikaendeleza hicho kingine na kunganisha ukumbi na jiko na store ,ila ilikuwa mwendo wa kobe ,tena nilikuwa mchumi hatari naandika kila nachotumia hapo mpaka nyumba inasimama na nashinda site na mafundi mwanzo mwisho sametime nakuwa kibarua mwenyewe
 
Mkuu kama ulikuwepo hashauriki maana ilifika wakati mpaka tunagomba nikabidi kumuacha maana yeye anataka mambo makubwa anadhani pesa huwa zinashukaga na malaika mbinguni ,
Namwambia ujenzi sio rahisi watakiwa ujinyime upunguze matumizi ,yaan ujibane bane kwa hali zetu ndipo ujenge kinyume chake kila siku utaishia nyumba za kupanga ,
Binafsi nilikaza roho nikaanza kujenga taratibu tena nyumba ile nayotaka lkn nilianza mdogo mdogo mpaka hapa nilipofikia sihaba
We muache ipo siku atakukumbuka, na majuto kibao ndiyo dawa ya watu wabishi majuto kwao ndiyo mafundisho,

Huwezi kumaliza kila kitu unahamia na vingine vinaendelea wakati upo kwako, mdogo mdogo, aiseehh mbona unamaliza, tena ni kwako kwanza unakua na shauku na raha kupamaliza yani ukipata hela tu huyo unakimbilia site[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], nyumba za kupanga kuna kero sana, sisajua huyo dada anazifurahiaje,

Yani ujenzi uneletaga raha sana ukiwa unajenga kwako asikuambie mtu, kama mtu unajinyima unajenga kwako ni jambo la heri, jioni nilikua natoka na mafundi site nakaa nao mahali nawapa vinywaji nawambia nataka kumaliza kitu fulani ila hela imekata, wananipa moyo napata ushauri aiseeeh najikuata nimemaliza, so ushirikiano na mafundi pia umenisaidia sana sana
 
Mpe mbongo bilioni 10 atajenga mijumba akitegemea kurejesha mapesa yake baada ya miaka 10 hadi 20.

Mpe msomali bilioni 10 atafungua maduka makubwa, ata import na kukuza biashara zake kwa eneo husika.

Mpe Muhindi bilioni 10 ataanzisha kiwanda kitakua kikubwa na atapiga pesa kwa muda mrefu.

Ujumbe tusifikirie kujenga sana tuache dhana ya uoga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila mkuu mimi siwezi kumcheka mbongo anayejenga nyumba nitamcheka ambaye amehonga pesa na kunywea pombe.
Haya mambo yanaendana na tamaduni mkuu huwa hatuigani kwenye maisha.

Wahindi kitu kingine wana elimu na connection kubwa ya mambo ya biashara.

Kwa mfano utakuta muhindi yupo Bongo lakini kuna ndugu zake wapo Zambia,South Africa,Dubai,Canada,China wanafanya biashara kubwa kubwa.

Kwa hyo mtu kama huyu akifungua biashara hawezi kuyumba,coz anapoanzisha tayari anakuwa na plans zake kichwani kwamba bidhaa fulani nitachukua zambia,zingine nitachukua South Africa kwa bei fulani,zingine nitachukua Dubai kwa bei fulani na nikishafikisha bongo nitauza kwa bei fulani tena kwa haraka.

Lakini mwenzangu na mimi hujawahi kufanya biashara na wala Dubai/SA/China hujawahi kufika unapasikia tu siku ukienda kwa mara ya kwanza unaanza kushangaa shangaa mwishowe unaishia kutapeliwa tu pesa.

Na kingine pia wana ushirikiano sana ikitokea mmoja wapo amefirisika watamchangia hadi ainuke tena.

Lakini huku bongo ukifirisika ndio basi tena unabaki kuchekwa na kuzomewa tu.

Kwa hiyo ukiona mtu anajenga mijumba ule ni uoga anajihami asije kuja kuchekwa baadae akifulia.
 
Mkuu umenikatisha tamaa kabisa. Nilijua unataka unipe mkakati kwamba tuweke nguvu pamoja tuijenge halafu nikupangishe miaka mitano au kumi kulingana na gharama tutakayoitumia katika ujenzi.
Noooo [emoji38][emoji38][emoji38] nitakupa ushauri ni jokes tu hizo boss, ila mzee vyumba 6 ni mjumba sio nyumba, ila kuna plan za kufanya kaa na mafundi boss weka nao mikakati, mafundi wanatakiwa wajue una hela kidogo hata kama una milion 100 ili uoate ushauri halisi, unakaa nao na kuwauliza nataka kumalizia hapa nafanyaje na hela inakata!!? Watakupa ushauri na utatoboa boss
 
Back
Top Bottom