Ujenzi: Nimefanya uchunguzi kwanini watu wengi wanashindwa au kuchelewa kuwa na kwao

Hii ni kujisahau. Unapata hela unaweza kulipa Kodi popote unaona huna umuhimu wa kujenga 'nje' ya mji. Siku unashtukia mrija wa pesa umeziba ndio unaanza kujuta.
Mfano yuke mama wa zenji imenisikitisha na inatia huruma, mume wake alikua na kazi serikalini wakawa wanakaa kwenye nyuma ya serikali mume wake kafa akalazimishwa kutoka kwenye nyumba kinguvu, sasa wakati wanamuhoji anasema hajui pakwenda waende wapi inasikitisha sana
 
Vizuri sana.
 
Shida hiyo boss, inasikitisha halafu watu wa hivyo huwa hawashauriki, ndiyo tunakuja kwenye point kuwa kujenga ni mipango, mtu mwenye akili anaanza mdogo mdogo unashangaa umemaliza,
 
Hao ni wengi sana.
 

3M finishing? Unatumia mbao gani kuezeka na bati za ubora upi mkuu? Hapo haujaongelea madirisha wala lipu. Unaweza kubana unavyoweza ila hiyo pesa ni ndogo. Vinginevyo iwe ni vyumba viwili.
 
Okey kwahiyo una maana ulianza vyumba vichache kupandisha boma, au kwenye finishingi ulichagua vyumba vichache
 
Shida hiyo boss, inasikitisha halafu watu wa hivyo huwa hawashauriki, ndiyo tunakuja kwenye point kuwa kujenga ni mipango, mtu mwenye akili anaanza mdogo mdogo unashangaa umemaliza,
Mkuu kama ulikuwepo hashauriki maana ilifika wakati mpaka tunagomba nikabidi kumuacha maana yeye anataka mambo makubwa anadhani pesa huwa zinashukaga na malaika mbinguni ,
Namwambia ujenzi sio rahisi watakiwa ujinyime upunguze matumizi ,yaan ujibane bane kwa hali zetu ndipo ujenge kinyume chake kila siku utaishia nyumba za kupanga ,
Binafsi nilikaza roho nikaanza kujenga taratibu tena nyumba ile nayotaka lkn nilianza mdogo mdogo mpaka hapa nilipofikia sihaba
 
Okey kwahiyo una maana ulianza vyumba vichache kupandisha boma, au kwenye finishingi ulichagua vyumba vichache
Kiongozi nilianza chumba kimoja master msingi nikja onganisha msingi wa chumba cha pili master nikaja msingi wa chumba cha tatu master ,kisha nikaja kunyanya vyumba viwili boma nikapiga linta na kuezaka nikaeka milango nikahamia nikaendeleza hicho kingine na kunganisha ukumbi na jiko na store ,ila ilikuwa mwendo wa kobe ,tena nilikuwa mchumi hatari naandika kila nachotumia hapo mpaka nyumba inasimama na nashinda site na mafundi mwanzo mwisho sametime nakuwa kibarua mwenyewe
 
We muache ipo siku atakukumbuka, na majuto kibao ndiyo dawa ya watu wabishi majuto kwao ndiyo mafundisho,

Huwezi kumaliza kila kitu unahamia na vingine vinaendelea wakati upo kwako, mdogo mdogo, aiseehh mbona unamaliza, tena ni kwako kwanza unakua na shauku na raha kupamaliza yani ukipata hela tu huyo unakimbilia site[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], nyumba za kupanga kuna kero sana, sisajua huyo dada anazifurahiaje,

Yani ujenzi uneletaga raha sana ukiwa unajenga kwako asikuambie mtu, kama mtu unajinyima unajenga kwako ni jambo la heri, jioni nilikua natoka na mafundi site nakaa nao mahali nawapa vinywaji nawambia nataka kumaliza kitu fulani ila hela imekata, wananipa moyo napata ushauri aiseeeh najikuata nimemaliza, so ushirikiano na mafundi pia umenisaidia sana sana
 
Ila mkuu mimi siwezi kumcheka mbongo anayejenga nyumba nitamcheka ambaye amehonga pesa na kunywea pombe.
Haya mambo yanaendana na tamaduni mkuu huwa hatuigani kwenye maisha.

Wahindi kitu kingine wana elimu na connection kubwa ya mambo ya biashara.

Kwa mfano utakuta muhindi yupo Bongo lakini kuna ndugu zake wapo Zambia,South Africa,Dubai,Canada,China wanafanya biashara kubwa kubwa.

Kwa hyo mtu kama huyu akifungua biashara hawezi kuyumba,coz anapoanzisha tayari anakuwa na plans zake kichwani kwamba bidhaa fulani nitachukua zambia,zingine nitachukua South Africa kwa bei fulani,zingine nitachukua Dubai kwa bei fulani na nikishafikisha bongo nitauza kwa bei fulani tena kwa haraka.

Lakini mwenzangu na mimi hujawahi kufanya biashara na wala Dubai/SA/China hujawahi kufika unapasikia tu siku ukienda kwa mara ya kwanza unaanza kushangaa shangaa mwishowe unaishia kutapeliwa tu pesa.

Na kingine pia wana ushirikiano sana ikitokea mmoja wapo amefirisika watamchangia hadi ainuke tena.

Lakini huku bongo ukifirisika ndio basi tena unabaki kuchekwa na kuzomewa tu.

Kwa hiyo ukiona mtu anajenga mijumba ule ni uoga anajihami asije kuja kuchekwa baadae akifulia.
 
Mkuu umenikatisha tamaa kabisa. Nilijua unataka unipe mkakati kwamba tuweke nguvu pamoja tuijenge halafu nikupangishe miaka mitano au kumi kulingana na gharama tutakayoitumia katika ujenzi.
Noooo [emoji38][emoji38][emoji38] nitakupa ushauri ni jokes tu hizo boss, ila mzee vyumba 6 ni mjumba sio nyumba, ila kuna plan za kufanya kaa na mafundi boss weka nao mikakati, mafundi wanatakiwa wajue una hela kidogo hata kama una milion 100 ili uoate ushauri halisi, unakaa nao na kuwauliza nataka kumalizia hapa nafanyaje na hela inakata!!? Watakupa ushauri na utatoboa boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…