Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE AGENS MARWA ACHANGIA UJENZI NYUMBA YA KATIBU UWT MKOA WA MARA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Marwa amekabidhi mifuko 10 ya Saruji katika ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Mkoa wa Mara ikiwa ni sehemu ya matofali 1000 pamoja na laki tano (500,000) zilizotumika kununua Saruji Mifuko 25 hivyo kufikisha Mifuko 35 ya Saruji na Lori moja la mchanga ikiwa ni mchango wake hadi sasa katika ujenzi huo.
"Nilitoa laki tano ilikuwa nimifuko ya Saruji 25 na matofari 1000 pamoja na Trip 1 ya Mchanga na Leo nimechangia mifuko 10 hii nimchango ambayo binafsi nimetoa katika kuunga Mkono katika ujenzi wa Nyumba ya katibu wetu wa UWT mkoa wa Mara" - Mhe. Agness Marwa Mbunge wa Viti Maalum Mara.
Aidha, Wananchama 33 kutoka CHADEMA, CUF na NCCR wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mkutano wa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara Agness Marwa uliofanyika Manispaa ya Musoma katika Kata ya Mwigobero huku wakidai kufanya hivyo nikumuunga mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utendaji kazi wake.