Ujenzi soko dogo Karikaoo wajengwa chini ya ulinzi

Ujenzi soko dogo Karikaoo wajengwa chini ya ulinzi

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Dar es Salaam. Ujenzi wa uzio wa soko dogo Kariakoo na ukarabati wa soko kubwa lililoungua moto Julai mwaka huu unafanyika chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Hali hii imeonekana leo baada ya kupita siku nne tangu mkandarasi Estim Contraction Ltd anayetakiwa kufanya shughuli hiyo kukabidhiwa mkataba na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Kumekuwepo na mvutano kati ya wafanyabiashara wa soko dogo na uongozi wa mkoa ambao walionyesha msimamo wa kutohama sokoni hapo wakitaka suala hilo lifanyike kimaandishi.

Mwananchi leo Jumanne Desemba 28,2021 imefika sokoni hapo na kukuta mafundi wakiendelea na kazi ya kuzungushia uzio huku kukiwa na gari mbili za polisi zilizokuwa na askari wasiopungua 15.

Askari hao walibeba silaha zikiwemo bunduki na mabomu ya machozi huku wakiwa wanapokezana kuangalia hali ya usalama katika soko hilo.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Mnyau Hamis, amesema wanashangaa kwa nini Serikali inatumia nguvu kubwa hivyo kupambana na watu wasio na silaha wakati ombi lao ni dogo tu na linalotekelezeka katika kuhakikisha wanaweka kumbukumbu.

Mfanyabiashara mwingine Mariam Mziwara, amesema ili biashara zao zisiathirike, walishatoa ombi kuwa ni vema kuanza kukarabati soko kubwa ili wake huko kwa muda kupisha ujenzi wa soko lao dogo.

Alidai utaratibu huo umewahi kutumika katika ujenzi wa masoko mengine likiwemo la Kisutu na Buguruni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Hussein Magaeli, amesema kikao cha mazungumzo kati yao na uongozi wa wilaya jana kilishindwa kufanyika baada ya kuwaomba wawapatie barua rasmi ya kikao.

Wakati wafanyabiashara wakieleza hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija amesema wameamua kuweka ulinzi ili mkandarasi afanye kazi yake kwa usalama kutokana na kuibuka kwa sintofahamu ya wafanyabiashara kugoma kuondoka

Chanzo:- Mwananchi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wanabembelezwa sana, yaani soko ni kwa manufaa yawatanzania wote halafu wanataka kuleta huu ujinga. Piga mabomu ya kutosha kabisa
 
Back
Top Bottom