Ujenzi Unaofanywa na Wachina

Ujenzi Unaofanywa na Wachina

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nikiwa na mamlaka ya kutoa tenda, sitatoa tenda ya ujenzi kwa niaba ya taifa kwa kampuni yoyote ya Kichina. Hata kama pesa zinatoka kwao, nitawaambia warudi nazo kwao.

Katika thread hii nitatoa mifano mingi sana ya ujenzi unaofanywa na Wachina ambao unahatarisha maisha ya watu; kwa bahati nzuri YouTube inatoa ushaidi mwingi sana.

Leo nitaanza na tukio hili lililotokea Pakistan mwanzoni mwezi huu

Subiri wafuasi flani waje kuwatetea hawa matapeli
Watakuambia hizo ni propaganda za nchi za magharibi, mara wachina hawajawahi kutawala ni rafiki zetu wa kweli, mara utasikia mikopo yao haina masharti ya kuruhusu haki za ushoga...😂😂

Nasikia kuna kampuni fulani ya SinoHydro imepewa tenda ya kujenga barabara ya mwendokasi, kabla hata haijawakabidhiwa tayari ishaanza kubomoka..na ndio hao hao wanajenga bwawa la Nyerere
 
Siyo kweli. Ujenzi wao hata uko kwao uko hivyo hivyo, ni wa kubabaisha na wenyewe wanajua hivyo. Ni mara kadhaa kwa serikali ya china imekuwa inatafuta Conslutants kuroa kwa Mabeberu ili kukwepesha hilo.

Angalia mifano hii ambayo ni ndani ya china yenyewe

Kinachoogofya ni kuwa nyingi zinaanguka ndani ya miaka kumi tu. Madaraja mengi hujengwa kuhimili mizigo kwa zaidi ya miak hamsini, lakini kwa china ni tofauti kabisa

Duh kwahio baada ya miaka kumi tunaweza kujikuta tunazama na Nyerere bridge?!! Inatisha.
 
Duh kwahio baada ya miaka kumi tunaweza kujikuta tunazama na Nyerere bridge?!! Inatisha.
Hilo daraja hata mimi siliamini sana, ila hatari zaidi iko Kenya kwenye ile SGR yao. Tukiwa hai, baada ya miaka kumi ijayo iwapo JF itaendelea kuwa active tutakumbushana; kuna sehemu walijengea chokaa baada ya kuishiwa sementi wakidai huo ni ugunduzi mpya.

Angalia matukio zaidi hapa

Siyo kweli. Ujenzi wao hata uko kwao uko hivyo hivyo, ni wa kubabaisha na wenyewe wanajua hivyo. Ni mara kadhaa kwa serikali ya china imekuwa inatafuta Consultants kutoka kwa "Mabeberu" ili kukwepesha hilo.

Angalia mifano hii ambayo ni ndani ya china yenyewe

Kinachoogofya ni kuwa nyingi zinaanguka ndani ya miaka kumi tu. Madaraja mengi hujengwa kuhimili mizigo kwa zaidi ya miak hamsini, lakini kwa china ni tofauti kabisa
Ungekuwa unaangalia documentary za huko kwa mabeberu, ungebaini kuwa hata kwao kuna engineering blunders nyingi tu.
 
Ungekuwa unaangalia documentary za huko kwa mabeberu, ungebaini kuwa hata kwao kuna engineering blunders nyingi tu.
Mimi ninaishi kwa mabeberu. Wanalalamika kuwa barabara na madaraja yo mengi yana umri wa takriban miaka mia wanataka yabadilishwe; baadhi ndiyo yameanza kuanguka moja moja kwa uzee siyo kwa engineering mbovu. Siyo unajenga daraja leo kwa mabilioni ya pesa halafu miaka kumi tu limeanguka na kuua watu. Civil Engineering haifanyi kazi hivyo.

Nikiwa na mamlaka ya kutoa tenda, sitatoa tenda ya ujenzi kwa niaba ya taifa kwa kampuni yoyote ya Kichina. Hata kama pesa zinatoka kwao, nitawaambia warudi nazo kwao.

Katika thread hii nitatoa mifano mingi sana ya ujenzi unaofanywa na Wachina ambao unahatarisha maisha ya watu; kwa bahati nzuri YouTube inatoa ushaidi mwingi sana.

Leo nitaanza na tukio hili lililotokea Pakistan mwanzoni mwezi huu

Isijekua ni vita vya kibiashara
Kumbuka kua reli ya TAZARA ilijengwa na wachina mwanzo mwisho.
 
Isijekua ni vita vya kibiashara
Kumbuka kua reli ya TAZARA ilijengwa na wachina mwanzo mwisho.
wakati wachina wanajenga reli ya TAZARA walikuwa hawajawa na tamaa ya utajiri. In fact walijenga reli ile kwa kutumia materials kutoka Ujerumani, siyo ya kutoka China. Kuna aibu tuliyojipatia kuwa treni moja iliharibika, China wakasema ilitoka Ujerumani watatuma mtaalumu kutoka Ujerumani atusaidie, na wajerumani wao wakasema kuwa treni hiyo ilitokea Afrika ya Kusini ambao wakati huo hatukuwa na uhusiano nao kwa sababu ya ubaguzi. Lakini ikabidi tumruhusu kaburu aje kututengenezea treni yetu hiyo tuliyokuwa tunaamini ni ya mchina.
 
Mimi ninaishi kwa mabeberu. Wanalalamika kuwa barabara na madaraja yo mengi yana umri wa takriban miaka mia wanataka yabadilishwe; baadhi ndiyo yameanza kuanguka moja moja kwa uzee siyo kwa engineering mbovu. Siyo unajenga daraja leo kwa mabilioni ya pesa halafu miaka kumi tu limeanguka na kuua watu. Civil Engineering haifanyi kazi hivyo.

Mimi nakubaliana na wewe kuwa wachina wanafanya kazi chini ya viwango kwa condition moja kubwa, waliowapa kazi hawapo serious katika usimamizi.

Kuna kipindi huwa naangalia kinaitwa "engineering blunders and fixes". Huko ughaibuni wanatoa documentary nyingi tu kuonyesha makosa makubwa wanayofanya wakandarasi wa ujenzi, iwe maharaja au skyscrapers.
 
Mtoa mada mimi ninaona tatizo lipo kwa politicians wetu na wenye maamuzi kama wewe, ninakupa mfano, pale mpakani na Zambia, wachina wanajenga Ile barabara kuu, hasa kutoka Isoka hadi Chinsali, ni top class road, pana na nzuri mno,tatizo wapo very slow, pia Wachina wamejenga Ile barabara ya kutoka kafue hadi Kazungula border ipo safi, wachina wamejenga Kazungula Bridge pamoja na zile one stop border post zipo safi, inategemeana na political will ya nchi
 
Wachina product zao ni cheap na quality ni mbovu. Hili ni wazi. Na usipokuwa makini nao wanakuangamiza. Vitu kama hizi toys za kuchezea watoto kuna baadhi zina kemikali mbaya zinapoingia mdomoni. Product yoyote ya mchina inatakiwa kuangaliwa kwa macho mawili. Hawajali na hawana utu kama wazungu.
 
Subiri wafuasi flani waje kuwatetea hawa matapeli
Watakuambia hizo ni propaganda za nchi za magharibi, mara wachina hawajawahi kutawala ni rafiki zetu wa kweli, mara utasikia mikopo yao haina masharti ya kuruhusu haki za ushoga...😂😂

Nasikia kuna kampuni fulani ya SinoHydro imepewa tenda ya kujenga barabara ya mwendokasi, kabla hata haijawakabidhiwa tayari ishaanza kubomoka..na ndio hao hao wanajenga bwawa la Nyerere
Mtu anaewapigia promo wa china muangalie mara 2*2 wengi wao uwa na matatizo fulani fulan hivi.
 
Subiri wafuasi flani waje kuwatetea hawa matapeli
Watakuambia hizo ni propaganda za nchi za magharibi, mara wachina hawajawahi kutawala ni rafiki zetu wa kweli, mara utasikia mikopo yao haina masharti ya kuruhusu haki za ushoga...[emoji23][emoji23]

Nasikia kuna kampuni fulani ya SinoHydro imepewa tenda ya kujenga barabara ya mwendokasi, kabla hata haijawakabidhiwa tayari ishaanza kubomoka..na ndio hao hao wanajenga bwawa la Nyerere
Acha uongoo.bwawa linajengwa na wamisri
 
Back
Top Bottom