Wanaojenga wamefunga barabara yote bila kuwa na njia mbadala ili shughuli za kijamii ziendelee, baadhi ni athari zilizosababishwa na ujenzi huo;
1. Gari za taka kushindwa kuingia kubeba taka na hivyo kusababisha Watu kukaa na taka muda mrefu
2. Ambulance kushindwa kupita endapo itatokea emergency na tayari ishatokea.
3. Gari za emergency kama fire na tanesco kushindwa kupita
4. Magari zaidi ya 800 kukosa parking na wanapoelekezwa kupaki wanatozwa parking ya Tsh. 2,000 kwa siku
5. Tunalipishwa hela za parking lakini hakuna risiti, hiyo inamaanisha kuna ukwepaji Kodi ya Serikali pia kuna upigaji hizo hela zinaelekezwa kwa nani?
Wakazi walimshauri Diwani wa Upanga Magharibi, Adnan Kondo kwamba afunge barabara nusu ili kuepuka usumbufu mkubwa lakini hakuwasikiliza na kutaka watoe magari yao yote na walivyotoa ameanza kuwatoza parking, wakati kule walipokuea wanapaki walikuwa hawalipi.
Hata wengine kuwatoza pesa za parking za mwezi mzima na baada ya siku mbili kuwatoa. Na kutowarudishia pesa zao.
Kwa hesabu ya haraka kuna gari zaidi ya 800 kila gari anatoza 2000 kwa siku kwa hiyo ni mtaji wa takriban milioni moja na laki sita kwa siku.