KERO Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni Binti Matola (V-WAYS) nini kinaendelea? imetelekezwa?

KERO Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni Binti Matola (V-WAYS) nini kinaendelea? imetelekezwa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Topintz

Senior Member
Joined
Aug 2, 2013
Posts
170
Reaction score
663
Mnamo mwaka jana 2025 mwanzoni, serikali ilitangaza kuboresha barabara ya Kinondoni kuanzia Wakulima Road (usalama) mpaka Mtaa wa Binti Matola (mtaa opposite na mwembe jini, unaoenda mpaka V Ways) kwa kiwango cha lami.

Viongozi pamoja na mkandarasi walikaa kikao na sisi wakazi wa eneo husika kuelezea zoezi zima na tukafurahi kuona maboresho husika. Ndani ya muda mfupi mkandarasi alifika site akatifua na kuchimba barabara nzima kuanzia Binti Matola mpaka Wakulima road, ajabu ni kwamba ile barabara ya wakulima road ikapigwa zege na lami chap chap ndani ya mwezi ikakamilka.

Changamoto imebaki huu upande wa Binti Matola (Kutoka Mwembe jini kwenda V Ways) , barabara ilichimbwa ila imetelekezwa pasipo kujali changamoto tunazopitia wakazi wa eneo hili kwani maeneo ya parking yamevurugwa kwa vifusi, mvua ikinyesha barabara inajaa matope, wenye biashara zimeathirika kwani magari hayafiki kiurahisi kutokana na barabara kuchimbwa na hivyo eneo la pembeni kuwa juu zaidi.

Tumefanya jitihada za kuwasiliana na uongozi wa mtaa na wilaya kupata suluhisho lakini hakuna majibu ya kuridhisha yenye kutoa timeline, tunapigwa danadana inaenda mwaka sasa.

Je, kulikuwa na ulazima gani wa kuchimba barabara na kukwamisha shughuli za mtaa mzima kama hamkua na bajeti ya kumalizia ujenzi wa barabara husika? Mmewafikiria walipa kodi wenu kama wenye viosk, garage, wauza vyakula, ma bar kama V Ways na wafanyabiashara wengine hapo mtaani mnaowadai kodi na ushuru kila siku na wakati mme disrupt mzunguko wao wa pesa inaenda mwaka sasa?
Project ilikuwa moja ila kwanini Wakulima Road itengenezwe haraka halafu sisi wengine ndo tutelekezwe?.
6.jpeg
2.jpeg

5 (1).jpeg
1.jpeg
 

Attachments

  • 5.jpeg
    5.jpeg
    142.2 KB · Views: 20
  • 4.jpeg
    4.jpeg
    143.5 KB · Views: 18
  • 3.jpeg
    3.jpeg
    202 KB · Views: 19
  • 1.jpeg
    1.jpeg
    109 KB · Views: 22
Mtoa mada atuelekezo vizur ni maeneo gani hayo mm ni mtoto wa mitaa hiyo ya kinondoni lakini kwenye picha sijaelewa my be kinondoni ya upande wa pili kule care
 
Mkuu, hizo barabara za daslam kumbe ni kama za huku lalago, maswa ndanindani simiyu huku eehhh....🤔
 
Mtoa mada atuelekezo vizur ni maeneo gani hayo mm ni mtoto wa mitaa hiyo ya kinondoni lakini kwenye picha sijaelewa my be kinondoni ya upande wa pili kule care
Mwembe jini(makaburini)
Hapo

Ova
 
Mnamo mwaka jana 2025 mwanzoni, serikali ilitangaza kuboresha barabara ya kinondoni kuanzia Wakulima road (usalama) mpaka Mtaa wa Binti Matola (mtaa opposite na mwembe jini, unaoenda mpaka V Ways) kwa kiwango cha lami.
Hivi mzee mwambalaswa bado yupo huko
Aise kweli naona wamechimba wameacha mahandaki
Hata mikocheni regent mitaa fulani hali iko hivyo hivyo

Ova
 
Mtoa mada atuelekezo vizur ni maeneo gani hayo mm ni mtoto wa mitaa hiyo ya kinondoni lakini kwenye picha sijaelewa my be kinondoni ya upande wa pili k

Mkuu, hizo barabara za daslam kumbe ni kama za huku lalago, maswa ndanindani simiyu huku eehhh....🤔
Haha! Tunashindwa kuelewa, ni kheri wangeiacha kama hawana bajeti au uhakika wa kuitengeneza kuliko kuchimba na kuharibu mtaa mzima alafu unautelekeza. Shughuli za mtaa mzima zimekua affected, mvua ikinyesha ni balaa mtaa mzima.
 
Mkuu, hizo barabara za daslam kumbe ni kama za huku lalago, maswa ndanindani simiyu huku eehhh....🤔
Tofauti ya dar na mikoani ni maghorofa,ambayo kimsingi ni ofisi/biashara, nyumba za makazi mikoani ni Bora zaidi kwa asilimia kubwa
 
Mkuu, hizo barabara za daslam kumbe ni kama za huku lalago, maswa ndanindani simiyu huku eehhh....🤔
Tofauti ya dar na mikoani ni maghorofa,ambayo kimsingi ni ofisi/biashara, nyumba za makazi mikoani ni Bora zaidi kwa asilimia kub
 
Sio 4 ways ni V way.. umechanganya
Hio barabara inatoka Mwembeni inapita V ways na 4 ways pia inatokea Leaders Ada Estate. V ways na 4 ways pote pamechimbwa.
 
Mtoa mada atuelekezo vizur ni maeneo gani hayo mm ni mtoto wa mitaa hiyo ya kinondoni lakini kwenye picha sijaelewa my be kinondoni ya upande wa pili kule care
Unapajua makaburini? Barabara inatoka hapo mwembeni inaingia ndani kuelekea Kino shamba,Ada estate. Upande wa pili wa mwembeni inapita katikati makaburini kuelekea Usalama wa taifa na Hananqsif.
 
Back
Top Bottom