KERO Ujenzi wa barabara ya Safina Olasiti hadi Morombo-Arusha

KERO Ujenzi wa barabara ya Safina Olasiti hadi Morombo-Arusha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naipongeza Serikali kwa ujenzi wa barabara hii. Changamoto iliyopo ni kuwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Safina Olasiti hadi Morombo hajaweka alama ambazo zinawataka/kuelekeza watumiaji wa barabara kutumia njia mbadala.

Hili linasabisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara/njia hizo.

Pia barabara/njia ambazo watumiaji wanalazimika kutumia zimeharibika hasa kipindi hiki cha mvua.

Tunaomba Mkandarasi aelekezwe kuweka vibao elekezi na kurekebishwa barabara/njia mbadala ili kuepuka usumbufu kwa wananchi.

Mkazi wa Olasiti Arusha.
 
Back
Top Bottom