nyboma
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 2,308
- 7,366
Bila shaka wakati Mh. Raisi Samiah Suluhu Hassan akipokea ripoti ya TAKUKURU na CAG na ulipofika wakati wa yeye kuzichambua ripoti zile nimemsikia kwa masikio yangu mawili ya kwamba “Mradi wa ufuaji umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere” utakamilika mnamo mwaka 2024 ama zaidi ya hapo.
Nikirudi nyuma nakumbuka waziri wa Nishati kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo mbunge wa chato Dk Medard Kalemani alisema ” Bwawa la kufua umeme wa megawati 2,115 wa Julius Nyerere (JNHPP) litaanza kujazwa maji kuanzia Novemba 15, mwaka huu na hadi kufikia Aprili 15, 2022 litakuwa limejazwa ili mwezi mmoja baadaye umeme uanze kufuliwa kutoka kwenye bwawa hilo.”
Kwa ufupi tungetegemea kupata umeme kutoka katika bwawa hilo mwezi wa tano mwaka huu.
Wajuzi wa mambo mnaweza niambia ni kitu gani hasa kilipelekea bwawa lile kutokujazwa maji ndani ya muda uliopangwa? Na kwanini hadi 2024?
Pili kati ya serikali ya Mama yetu Samiah Suluhu Hassani na Ile ya Mpendwa wetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ni ipi inasema ukweli? Maana naona zinapingana waziwazi ilihali Mama yetu huyu ambaye kwa sasa ndio Raisi wetu alikuwa msaidizi wa Magufuli na alikuwa akifahamu kila kitu kinachojiri katika ujenzi wa bwawa lile.
Ama tuseme ndio Mama keshawekwa kati na mtoto wa mjini (mzee wa smile) na genge lake ili kuupotezea mradi ule na kurudi kulekule kwenye kukodi mitambo ya kufua umeme ili wajilipe mabilioni ya fedha za wananchi kwa kutuuzia umeme?
Nawasilisha.