Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo-Busisi) wafikia 85%

View attachment 2935272

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye Kilometa 3.2 pamoja na Barabara unganishi ya Kilometa 1.66, linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria umefika asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 15, 2024 Mkoani Mwanza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso (Mb) ilipoambatana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kukagua maendeleo ya mradi huo.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb) ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo na imempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili mradi huo ukamilike kwa muda uliopangwa.

Kakoso ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi wa daraja hilo kutoa fedha zitakazokwenda kuisaidia jamii inayozunguka mradi huo ambazo zitakuwa kielelezo kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema na Misungwi.

Aidha, Kakoso ameitaka Wizara ya Ujenzi kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika daraja hilo ambalo linatokana na kodi za wanachi ili liweze kudumu kwa muda wa miaka 100.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ambapo mpaka sasa jumla ya Shilingi Bilioni 441.3 zimetolewa kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anautazama sana mradi huu kipekee, amekuwa akitoa fedha kwa kila hati za Mkandarasi zinapowasilishwa na zimekuwa zikilipwa kwa wakati ili Mkandarasi asikwame kutokana na kukosekana kwa fedha", amesema Bashugwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Doroth Mtenga ameeleza kuwa mradi huo unatumika kama darasa la mafunzo kwa wanafunzi na wataalamu wetu wa ndani kupata uzoefu wa kusimamia na kujenga madaraja mengine kama hayo hapa nchini.

Hoja ya Mdau kuhusu Daraja - Matengenezo ya Daraja la Kigongo Feri mpaka Busisi kulikoni?
Hongera zake Magufuli

Japo bodaboda watahitaji elimu sana maana watapukutuika wengi kwa huo mkeka
 
Hivi hili daraja lina umuhimu gani? Yaani ni magari/mizigo ya kutoka wapi kwenda wapi yatalitumia? Kabla ya hapo hali ilikuwaje? NB: nauliza kwa nia nzuri kwani hayo maeneo siyajui.
Hili ni daraja muhimu Sana kwasababu linaunganisha mwanza kwenda sengerema,chato,bukoba na nchi za jirani..zamani kabla ya daraja magari yalivushwa kwa pantoni ambapo zaodi ya nusu saa unatembea ndani ya maji, daraja likiisha watatumia dk 5 tu
 
View attachment 2935272

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi) lenye Kilometa 3.2 pamoja na Barabara unganishi ya Kilometa 1.66, linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema - Geita katika Ziwa Victoria umefika asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 15, 2024 Mkoani Mwanza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso (Mb) ilipoambatana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kukagua maendeleo ya mradi huo.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb) ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo na imempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili mradi huo ukamilike kwa muda uliopangwa.

Kakoso ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi wa daraja hilo kutoa fedha zitakazokwenda kuisaidia jamii inayozunguka mradi huo ambazo zitakuwa kielelezo kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema na Misungwi.

Aidha, Kakoso ameitaka Wizara ya Ujenzi kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika daraja hilo ambalo linatokana na kodi za wanachi ili liweze kudumu kwa muda wa miaka 100.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ambapo mpaka sasa jumla ya Shilingi Bilioni 441.3 zimetolewa kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anautazama sana mradi huu kipekee, amekuwa akitoa fedha kwa kila hati za Mkandarasi zinapowasilishwa na zimekuwa zikilipwa kwa wakati ili Mkandarasi asikwame kutokana na kukosekana kwa fedha", amesema Bashugwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Doroth Mtenga ameeleza kuwa mradi huo unatumika kama darasa la mafunzo kwa wanafunzi na wataalamu wetu wa ndani kupata uzoefu wa kusimamia na kujenga madaraja mengine kama hayo hapa nchini.

Hoja ya Mdau kuhusu Daraja - Matengenezo ya Daraja la Kigongo Feri mpaka Busisi kulikoni?
Je Airport ya Chato inaendeleaje?
 
Magufuli oyeee
Magufuli amekufa likiwa kwenye materials mobilisation stage. Mpeni tu sifa Rais Samia kwa kuhakikisha anamaliza miradi yote ya mtangulizi wake.

Kumbuka Dikteta alivyponda na kutoendeleza miradi aliyoanza Kikwete kama bomba la gesi Mtwara na Bagamoyo port..

Magufuli alibuni miradi lakini hakuna mradi ulfika 40% kuanzia 2017 hadi anakufa mwaka 2021.

Samia ameruhusu ukosoaji na pamoja anavyobezwa lakini kazi amepiga kusawasawa.

Hongera Rais Samia kwa miaka 3 ya kazi iliyotukuka
 
Hili daraja halianzi kutumika mwaka huu.

Kila siku muda kukamilisha daraja unao gezwa
IMG_20240315_220644.jpg
 
Magufuli amekufa likiwa kwenye materials mobilisation stage. Mpeni tu sifa Rais Samia kwa kuhakikisha anamaliza miradi yote ya mtangulizi wake.

Kumbuka Dikteta alivyponda na kutoendeleza miradi aliyoanza Kikwete kama bomba la gesi Mtwara na Bagamoyo port..

Magufuli alibuni miradi lakini hakuna mradi ulfika 40% kuanzia 2017 hadi anakufa mwaka 2021.

Samia ameruhusu ukosoaji na pamoja anavyobezwa lakini kazi amepiga kusawasawa.

Hongera Rais Samia kwa miaka 3 ya kazi iliyotukuka
ST.MAGUFULI OYEE,,,mtajuana wenyewe vibaraka wa waarabu
 
Magufuli amekufa likiwa kwenye materials mobilisation stage. Mpeni tu sifa Rais Samia kwa kuhakikisha anamaliza miradi yote ya mtangulizi wake.

Kumbuka Dikteta alivyponda na kutoendeleza miradi aliyoanza Kikwete kama bomba la gesi Mtwara na Bagamoyo port..

Magufuli alibuni miradi lakini hakuna mradi ulfika 40% kuanzia 2017 hadi anakufa mwaka 2021.

Samia ameruhusu ukosoaji na pamoja anavyobezwa lakini kazi amepiga kusawasawa.

Hongera Rais Samia kwa miaka 3 ya kazi iliyotukuka
Ukimpa credit wewe cheti feki inatosha tusipangiane
 
R. I. P Magufuli hata nyumbu erythrocyte watapita hilo daraja huku wakitukana matusi yao
Mfuate we bwege, hiyo ni kazi ya mama labda km wafu wanafanya kazi duniani. Daraja lenyewe halina umuhimu, ni ule upendeleo wake ulioivunja nchi. Hatutaki kumsikia huyo shetani wenu
 
Hivi hili daraja lina umuhimu gani? Yaani ni magari/mizigo ya kutoka wapi kwenda wapi yatalitumia? Kabla ya hapo hali ilikuwaje? NB: nauliza kwa nia nzuri kwani hayo maeneo siyajui.
Hilo daraja Magufuli alijenga kwa ajili yake sawasawa na ule uwanja wa Chato. Yule alikuwa shetani hii nchi sijui leo ingekuwa wapi, tumshukuru Mungu kumwondoa yule shetani. Tuombe uzima uone km kutakuwa na magari itakuwa km daraja la umoja
 
Hivi hayo magugu maji yaliyotapakaa eneo la ujenzi na bandari karibu zote hapo Mwanza, hakuna kabisa akili zinazoona hayo magugu kuwa ni uchafu unaopaswa kusafishwa? Daraja jipya linaloitwa la kisasa na uchafu wapi na wapi? Nunueni mashine za kusafisha magugu, zinauzwa tu mbona? 😎
Halafu nilisikia kuwa hayo majani ni malighafi ya kutengenezea kitu kama mbolea hivi.
Ama ndiyo ule usemi kwamba, 'kwenye miti hakuna wajenzi'?
 
Back
Top Bottom