Ujenzi wa flyover kuondoa foleni Zanzibar

Ujenzi wa flyover kuondoa foleni Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ujenzi wa barabara za juu (Flyover) Mwanakwerekwe na Amani kuondoa tatizo la foleni Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara ya kutoka uwanja wa ndege hadi Kiembe Samaki hadi Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 08 Januari 2024 katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya nane imetekeleza kwa vitendo maagizo ya ilani ya CCM na kuivuka.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amesema Serikali imejenga kilomita 200 za barabara ikiwemo ujenzi wa barabara za mjini kilomita 100 na vijijini kilomita 275.

Vilevile ujenzi wa barabara mpya zitazoanza hivi karibuni Tunguu hadi Makunduchi, Kisauni hadi Fumba, Chake hadi Mkoani zenye jumla ya kilomita 500.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza kampuni ya CECC ya China kwa ujenzi wa viwango vizuri vya barabara zikiwa na mitaro ya kupitisha maji, njia za watembea kwa miguu.
IMG-20240108-WA0140.jpg
IMG-20240108-WA0135.jpg
IMG-20240108-WA0137.jpg
IMG-20240108-WA0138.jpg
IMG-20240108-WA0139.jpg
IMG-20240108-WA0136.jpg
IMG-20240108-WA0133.jpg
IMG-20240108-WA0142.jpg
IMG-20240108-WA0134.jpg
IMG-20240108-WA0141.jpg
IMG-20240108-WA0132.jpg
IMG-20240108-WA0130.jpg
IMG-20240108-WA0128.jpg
IMG-20240108-WA0131.jpg
IMG-20240108-WA0129.jpg
IMG-20240108-WA0127.jpg
IMG-20240108-WA0126.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240108-WA0128.jpg
    IMG-20240108-WA0128.jpg
    60.5 KB · Views: 19
Back
Top Bottom