Ujenzi wa frame ya duka uzingatie mahitaji ya mtumiaji

Ujenzi wa frame ya duka uzingatie mahitaji ya mtumiaji

umenikumbusha, kuna siku nilienda benki, ghafla tumbo likasumbua nikaongea na jamaa huduma kwa wateja anionyeshe sehemu ya kujisitiri, jamaa akanijibu kuwa benki ni sehemu ya kutoa na kuweka pesa si sehemu ya kujisaidia, nikaona isiwe taabu, akili ikafanya kazi kwa haraka pale pale nikajaza fomu ya kutoa fedha zote kwenye akaunti yangu na , jamaa wa benki yule yule akacheki akaunti yangu akaniambia anaomba anisaidie kunionyesha chooni, nikamjibu kuwa benki ni sehemu ya kuweka na kutoa pesa kwa hiyo nimeamua kutoa pesa zangu, akaona aibu huku akijichekesha chekesha tu!!
😂 Vyoo vya bank ni kwa staff tu duniani kote.
 
Wamiliki wa frame inabidi wabadilike.

Ukijenga frame lazima uweke choo pembeni hata kwa nje kwa ajili ya mhudumu na wateja.

Unaweza kukifanya cha kulipia. Unakuta mjini frame kibao lakini choo cha kulipia kipo mita kadhaa, hivyo inakuwa usumbufu kwa mhudumu wa frame akibanwa haja!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
1.Suala lako la jiko
- halifai kabisa kwa maduka bize Kama ya kariakoo.

-pia kukaa na jiko ndani ya duka kiusalama kwa majanga ya Moto itakusumbua sana.

-kuruhusu muuzaji apike ndani ya duka unakaribisha kuondoa umakini wa muuzaji wako .

Mf: Ishu za kuonja onja mapishi kwa muuzaji
Haziwez kubisa kuweka umakini ktk kuandika Oda za wateja, kusikiliza na kubageini Bei, kufunga mzigo na kurudishana chenji kwa ufasaha kwa wateja.

2. Suala la choo Cha ndani ya duka kwa ajili ya wageni.

-Hili halifai maana utakaribisha wezi na vibaka wakuchoree ramani ndani ya duka lako kwa kisingizio Cha kukojoa uje upigawe matukio mpk ushangae.

-Mhudumu kwenda haja ndogo ndani ya duka itakaribisha watu kutoka nje waweze kupora au kupata access ya duka kwa timing maana Mhudumu wako atajifungia kwa ndani ila nje ya duka pako wazi.

3.suala la stoo ya ndani
-hili nakuunga mkono, ila Ni muhimu iwepo stoo ndogo tu kwa ajili ya mzigo usiozidi siku 3 au wiki maximum.

NB: Kamwe Usijenge stoo kubwa/GODOWN na ukaiunganisha na duka lako la kuuzia.

Hapa likitokea la kutokea ndipo utajua Nini namaanisha. Yaani Unafilisika kabisa ndani ya usiku mmoja.

4. Suala la mlinzi wa ndani, Achana nalo kabisa, litakuja kukipata shida mwenyewe.
-kwanza kiserikali hairuhusiwi.

-Pili unahatarisha maisha ya mlinzi husika.
Nb: kamwe Mlinzi hatakiwi kujulikana kajificha exactly wapi ili asiwe target number one pale uvamizi unapotokea.

-tatu unatengeneza mazingira ya mlinzi kujua in&out ya biashara yako. Which is very risky.

Yaan ile
leo umeingiza mzigo, anajua apo Boss huna CASH,
Leo umemaliza mzigo, anajua apo boss UNAYO CASH.

Sefu na droo zote ndani ya duka lako, mlinzi wako unampa nafasi ya kuzijua.

Milango na mageti yote mlinzi anapata access ya kujua yamesukwa sukwa vipi, udhaifu uko wapi, uimara uko wapi.

5. Suala la Kitanda Cha mlinzi,
-Huu Ni Upuuzi achana nao kabisa, unajilisha tu upepo kwa wema wa kijinga.

Alokwambia mlinzi anaendaga lindo kulala ni Nani?

Mlinzi kazi yake Ni patrol full time, unapomletea Kitanda unamaanisha ananafas ya kulala.

Na siku akiibiwa,
akakwambia "nilipitiwa usingizi boss",
Upaswi kulalamika maana kulala KAZIni umeifanya Ni Haki yake na Wewe mwnyw ndo umedhamini kabisa huo usingizi kwa kugharamia Kitanda na godoro.[emoji4]

NAWASILISHA[emoji120][emoji4]
Good!! Very smart napendaga sana mabandiko yako

After all unajuaga kupangilia hoja zako
 
Kweli hizi ni mentality za watu wa abroad, yaani unachoongea hapa kipo huko kwa wenzetu, eti mwenye frame akujengee jiko kwa ajili ya kupasha kiporo chako cha wali maharage...hapa hapa Dar! Haha
sawa unaeza kuta hata kama likiwepo bei itakuwaje
 
View attachment 2144304
Wengi tunapofikiria kufungua frame ya duka, unawaza mahali Pa kuweka bidhaa na dirisha la wateja kuona na kununua bidhaa. Mambo ya muhimu tusiyo yazingatia ni mahitaji ya binadamu anaehudumia duka.

Mhudumu anahitaji kula, anahitaji kwenda haja. Haya ni mambo ya muhimu kwa kila binadamu. Unapoweka frame weka na jiko, choo na sehemu ya kuhifadhia bidhaa. Jikoni unaweza kuweka jiko la kupikia chakula, microwave na fridge. Mhudumu akipata mapumziko ya chakula anaweza kupasha kiporo chake cha wali maharage alichotoka nacho nyumbani au akaja na mchuzi wa kuku au mchicha wa nazi na akaweza kupika ugali wake pale na siku ikaendelea

Choo kitamsaidia mhudumu au hata wateja wako wachache. Fikiria mtu anafanya manunuzi ya milioni nne ana kutaarifu traffic ilikua kubwa barabarani amekaa njiani masaa matatu na anawahi kurudi. Kama anahitaji huduma ya choo unaweza kumpisha.

Ukiweka store ya ziada unawsza kuhifadhi bidhaa za ziada na pia kitanda cha mtu wa kulinda duka kwa ndani.

Unajenga frame choo kiko nje cha shimo, unamuona mhudumu anakwenda uwani na kopo la maji na akitoka huko aje akupimie sukari.!!
Utaambiwa iga ufe na unaendekeza anasa. Ni kama jiwe alivyokuwa waziri wa ujenzi na miundo mbinu alikataa kujengwa sidewalks barabarani eti ni anasa na kuchezea hela wakati yeye alikuwa anakunja 10%.

Mmatumbi binadamu wa ajabu sana.
 
Back
Top Bottom