Ujenzi wa Gabion, nyumba kwa milioni 2 tu!

Ujenzi wa Gabion, nyumba kwa milioni 2 tu!

nimependa mawazo yenu...

Iko appealing..

Ila mie nikilala humo nitakufa kwa pressure...

Nitakuwa nawaza kudondokewa na kufa ndani ya kifusi saa yoyote ..😀😀😀😳
 
MKuu vpi kuhusu..wadudu..kakama nge, tandu, mende, na ata nyoKa ..utapona kweli kwa hayo mawe
 
Ujenzi huo ni mzuri mbali na pwani kwenye hewa yenye unyevunyevu wa chumvi inayosababisha kutu.

Ujenzi huo sio mzuri kwa nyumba ya kuishi sababu utasumbuliwa sana na wadudu wadogo wadogo ndani wanaopita ktk upenyo ulio katikati ya mawe. Pia yatakuwa makazi ya kuishi wadudu.

Unafaa kujenga kuta za uzio tu si nyumba ya kuishi labda ndani upige plasta lakini bado wadudu watatoka kutani na kuingia ndani kupitia mioangoni.
 
Aahh labda ukae IRINGA
Hayo mawe unaokota nje ya nyumba yako

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ndugu Watanzania,najua na kwa pamoja tunajua kuwa UJINGA ndio asili yetu..

Naomba kuwatahadharisha kuwa huwezi kujenga Nyumba kwa mfumo huo,kama utaangalia vizuri hiyo video utaona kuwa huo Ujenzi unaoitwa "Gabion" hutumika kwa mapambo au kwa kujengea uzio "Fence" sio kwa kujengea Nyumba..

Kule Ulaya ujenzi huo hutumika sana pembezoni mwa Barabara ili kuzuia maporomoko ya Udongo au kasi ya maji yasiharibu Barabara....

Msimsikilize mleta hii Mada atakuuweni,mtafukiwa na mawe mkijenga nyumba zenu kwa kutumia huo ujenzi😁😁
 
Mkuu vipi umeshapaua? Leta picha halisi sasa sio za youtube tuone....heheheee
 
Unataka kuniambia m mbili unajenga nyumba ya hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi kujenga hiyo nyumba kwa 2m, uliza gharama za wire mesh au hizo Gabion uambiwe, pia gharama ya mawe na usafiri ni kubwa pia,
Kupanga mawe unahitaji skilled labour maana hiyo siyo zege kusema kwamba utamwaga tuu , kikawaida mawe yanataka mpangilio mzuri maana shape yake ni irregular

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Tuchekeche akili zaidi nadhani interlocking bricks zenye hole katikati ni cheap na bora zaidi maana akili ni kutumia gharama nafuu zaidi na kupata kitu bora nampongeza sana sana
 
Ingependeza kama ungesema mpango wako ni kuwa na kampani ya wadudu labda waogopa upweke ndio maana
 
Back
Top Bottom