Ujenzi wa hidden roof na paa la kawaida

Ujenzi wa hidden roof na paa la kawaida

Jenga la kawaida mkuu, nakumbuka jamaa yangu alijenga hiyo ,nilipomuuliza kuhusu ubora wa paa na kutokuvuja akasema ana warranty na fundi basi kitu kikaja kushuka mweee ni mwembe fundi kupigiwa simu blah blah nyingi mara kapotea mazima
Ukijenga Ile Kitu Ujue Ni Kihonda Morogoro Yaani Mafuriko Na Hasara Tele
 
Mimi nimepaua hidden roof ... Haivuji .... But kama unachagua namna ya upauaji kwa ajili ya kupunguza gharama wewe bora upaue paa la kawaida tu. Ukijichanganya kwenye hidden roof eti unapunguza gharama utaimba haleluya [emoji23]
Kila siku nawaambia watu hizo contemporary sio nyumba za maskini maana ukilazikisha kimaskini utakimbia nyumba..
 
Mimi nilichofanya nilipaua mwezi wa kumi then nikasubiri mvua sikuwa na haraka ya kufunga board ndani, mvua ilipokuja ikawa inavuja sehemu chache tu za misumari na hiyo kutokana na pilikapilika za fundi kupiga plasta ili ni kosa kwa maana kila kitu unatakiwa umalize kabla ya kuweka bati, mvua za sasa hivi nacheka kwa dharau tu hakuna cha kuvuja wala nini, NB usikimbilie kufunga board subiri mvua ije ikupe majibu sahihi alafu acha pilikapilika baada ya kupiga bati, kwaupande wangu upauaji huu umeokoa sana kibunda changu
 
Kama unapenda sana huo mtindo kote funika kasoro nyuma ila inahitaji plani nzuri kusudi hata aliepo pembeni asione bati
 
Paua kwa paa la kawaida, maji si kitu cha kufanya nacho mzaha, utakuja nishukuru baadae
 
Mimi nimepaua Hidden roof na haivuji ... Lakini i will stick to my last statement. "USIPAUE HIDDEN ROOF KUOKOA GHARAMA ... UTAIMBA HALELUYA"
IMG_20220530_082032.jpg
 
Mimi nilichofanya nilipaua mwezi wa kumi then nikasubiri mvua sikuwa na haraka ya kufunga board ndani, mvua ilipokuja ikawa inavuja sehemu chache tu za misumari na hiyo kutokana na pilikapilika za fundi kupiga plasta ili ni kosa kwa maana kila kitu unatakiwa umalize kabla ya kuweka bati, mvua za sasa hivi nacheka kwa dharau tu hakuna cha kuvuja wala nini, NB usikimbilie kufunga board subiri mvua ije ikupe majibu sahihi alafu acha pilikapilika baada ya kupiga bati, kwaupande wangu upauaji huu umeokoa sana kibunda changu
Asante kwa taarifa.
 
Hidden roof huvuja sababu kwa sababu kuu tatu;
1. Wakati wa kutengeneza gutter haikuzibwa vizuri na kupigwa plasta kwenye kona za ukuta hivyo kusababisha maji kutuama na kuingia kwenye ukuta.

2. Mabomba ya kutolea maji ni finyu au yameziba au gutter hazina slope ya kutosha

3. Fundi bati alizingua aidha hakuziba vizuri sehemu ambazo bati inaingia kwenye ukuta wakati wa kuezeka au alikuwa na pilika nyingi zilizopelekea kukanyanga bati maranyingi. Hii hutokea pale ambapo ushapaua ndio unapandisha tofali za kumalizia juu au kupiga plasta.
Sehemu ambazo geta hugusana na kuta sharti pabandikwe tile, slope nzuri na usafi wa mara kwa mara wa njia za maji, aidha hakikisha nyumba haiwi chini ya miti. Hupati tatizo lolote kamwe.
 
Mkuu karibu tukufanyie offer kwenye finishing kuanzia board had skiming.ndan nje tunakufanyia free ,na pia tukufanyie water proof treatments kwenye bat na ukuta juu isivuje daima call/WhatsApp 0757735884 au Instagram highland_decor_solution
Mimi nimepaua Hidden roof na haivuji ... Lakini i will stick to my last statement. "USIPAUE HIDDEN ROOF KUOKOA GHARAMA ... UTAIMBA HALELUYA"View attachment 2482713
 
Hidden roof huvuja sababu kwa sababu kuu tatu;
1. Wakati wa kutengeneza gutter haikuzibwa vizuri na kupigwa plasta kwenye kona za ukuta hivyo kusababisha maji kutuama na kuingia kwenye ukuta.

2. Mabomba ya kutolea maji ni finyu au yameziba au gutter hazina slope ya kutosha

3. Fundi bati alizingua aidha hakuziba vizuri sehemu ambazo bati inaingia kwenye ukuta wakati wa kuezeka au alikuwa na pilika nyingi zilizopelekea kukanyanga bati maranyingi. Hii hutokea pale ambapo ushapaua ndio unapandisha tofali za kumalizia juu au kupiga plasta.
Hampend kujifunza.ya nin upate shida mwaga slope usiweke gutter
 
Back
Top Bottom