Ujenzi wa kibanda siyo nyumba

Asante mkuu nishampata Fundi mkuu
Asante Sana kwa kuonyesha Nia ya kutaka kunisaidia
 
Wazo lako nizuri ila hela haitoshi mwanzoni nilikuwa na wazo Kama Hilo Ila mahesabu yalikataa baada ya kuona itabidi niongeze idadi ya kila kitu
 
Ndiyo mkuu upo
Udongo tifutifu eneo tambarare
Hapo unapata chumba mbili master plus solo na sebule yake kwa ramani ya kisasa kabisa , pamoja na kuezeka , Ila utapata tabu ya kuhamia bila floor Wala plasta na milango,
Ujitoe lakini , sio Lele mama! na usisikilize mtu zaidi ya kuzikumbuka kero na nyodo za father house uliyopanga.

Sent
 
Vyumba viwili na sebule? Inawezekanaje hapo inaweza kuwa
Tofali 900 bati 40 cement mifuko 30
Million 3 haitoshi
 
Kama unaweza kuafford kulipa Kodi ya laki moja kwa mwezi upo kwenye position nzuri Sana ya kujenga
Anza na boma tupu bila madoido , na ikiwezekana hamia hivo hivo , finnishing utaifanya ukiwa ndani , Ni njia rahisi kabisa ya kuondokana na kero ya kupanga
Lakini ukitaka uhamie nyumba ikiwa imekamilika kila kitu , ujenzi utaouona ngumu Sana ,


Sent
 
Thanks mkuu pamoja sana
 
Hata mie nimeona ajenge kwa staili unayomshauri , vyumba viwili na sebule , atapumzika kidogo wakati anajipanga na nyumba kubwa
Lakini chumba kimoja simshauri kwa kipato chake

Sent
 
Mkuu anza mengine yatajulikana mbele, hiyo hela inatosha
 
Ushauri Mzuri aanze mengine yatakuja njiani maana hiyo laki ya kilawezi atakuwa anaifanyia marekebisho taratibu
 
Vyumba viwili na sebule? Inawezekanaje hapo inaweza kuwa
Tofali 900 bati 40 cement mifuko 30
Million 3 haitoshi
Sijajua unatumia ramani ipi,unaweza usitumie hiyo idadi ya tofali,tafuta ramani nzuri

Sent
 
Inategemea na choo! Unaweza zika pipa mbili zikawa ndio chamber ya kutuliza mizigo huku ukijikongoja na mengine pipa 1 ni 20 mpk 25 elf wengne wana zika tire yote hayo upande wa choo kunakua na sink kama kawaida na pipe ya pvc inch4 ndio inapeleka kwny chamber
 
Sijajua unatumia ramani ipi,unaweza usitumie hiyo idadi ya tofali,tafuta ramani nzuri

Sent
Vyumba viwili havihitaji ramani
Sebule 350
Chumba 300 na choo chake Cha 100x160
Kajiko la 150 kwa 160
 
Choo Haina shida Nina eneo la kutosha na udongo ni tifutifu hivyo na Jenga Cha shimo na kufunika na mbao kwanza au mabanzi na kuta zake pia zitakuwa za mabanzi
 
Pi
Choo Haina shida Nina eneo la kutosha na udongo ni tifutifu hivyo na Jenga Cha shimo na kufunika na mbao kwanza au mabanzi na kuta zake pia zitakuwa za mabanzi
Choo una jenga kawaida sink kama kawaida ila kule mizigo inapo elekea badala ya kutumia gharama kubwa unakua umezika pipa lililotobolewa au matairi unajengea juu 2 pvc pipe ndio itaunga choo kwenda kwny chamber kuliko cha shimo kiafya chember au choo kikae mita kadhaa
 
Kila la heri mkuu utupe mrejesho.
Sie wa kuunga unga kulipa kodi roho inamaga basi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…