Ujenzi wa kibanda siyo nyumba

Ujenzi wa kibanda siyo nyumba

Tatizo gharama za Choo zipo constant, iwe unajenga nyumba ya vyumba 4 au kimoja, mfumo wa Choo unamaliza sana hela

Lakini ukijipanga chumba kimoja kizuri kinajengeka

Pia mimi huwa siwaamini mafundi kwa asilimia zote, anaweza kukwambia hiyo hela inatosha kumbe lengo lake apate kazi, mjengo utakapoishia hapo hapo yeye hana hasara

Yaani upo sahihi mafundi wanazingua sana
Mie nilileta fundi tubadilishe bati...tumefumua bati sii akaniambia unajua bro na kenchi nazo zitoke...nilichokaje
 
Kwa nini??
ukiwa na kiwanja tayari huwezi shindwa kuanza kama una kianzio kidogo lets say 3millions inafanya uhamie ndani kabisa
Hatua ya kwanza Jenga msingi.

pili pandisha tofali.

tatu funga lenta na nondo alafu pandisha tofali za mwisho course 2 au 3.

nne tafuta mbao za 2×4 na 2×3 funika kenchi na mbao za 2x2

tano nunua bati za bei nafuu na imara zenye muonekano mfano bati za corrugated za rangi.

sita weka milango na madirisha mazuri yenye hewa ya futi labda 5x6

ANGALIZO:
siyo lazima kumaliza ujenzi mfano milango ya ndani, malizia sebule, choo cha public, dinning, vibraza vya nje na chumba chako cha kulala kama kupiga plaster, rangi na tiles inatosha kuamia kama hutaki kuendelea kupanga.
 
Kama unalipa laki moja kodi kwa mwezi inaonesha kipato chako ni kizuri. Kwanini usijibane uongeze kidogo mkuu? gharama ya kujenga nyumba ndogo au chumba ni kubwa kuliko ya kujenga vyumba viwili au nyumba kubwa. sijui kama utaelewa
Ufafanuzi mkuu
 
Kwatope ukiwa na maana gani?
View attachment 1504651
Kama hivi[emoji116]
IMG_20200713_182112_9.jpg
 
Hapo unapata chumba mbili master plus solo na sebule yake kwa ramani ya kisasa kabisa , pamoja na kuezeka , Ila utapata tabu ya kuhamia bila floor Wala plasta na milango,
Ujitoe lakini , sio Lele mama! na usisikilize mtu zaidi ya kuzikumbuka kero na nyodo za father house uliyopanga.

Sent
hapo umeongea sana
 
Tatizo gharama za Choo zipo constant, iwe unajenga nyumba ya vyumba 4 au kimoja, mfumo wa Choo unamaliza sana hela

Lakini ukijipanga chumba kimoja kizuri kinajengeka

Pia mimi huwa siwaamini mafundi kwa asilimia zote, anaweza kukwambia hiyo hela inatosha kumbe lengo lake apate kazi, mjengo utakapoishia hapo hapo yeye hana hasara
Kabisa, Fundi hawana makadirio ya ukweli.
 
Fundi ameniambia tofali 650
Mchanga 2 cement 15 bati 16-18
Mawe Lori moja, maji nilipo ni bure, kibarua ni Mimi mwenyewe, Ela ya Fundi Hadi paa 200k siku tatu tunapiga Hadi lenter, madirish mawili na mlango mmoja vyote used, kibanda tayari.View attachment 1504411
nimeipenda hii plan haina Mambo mengi
 
Anaweza akaanza na cha pipa mkuu huku akivuta nguvu.

Sink ni Tsh 18,000 , Bomba Type C ni 25,000/= Tofali 8 ni 8,000/= ,Cement mfuko mmoja 13,500/= Mchanga atanunua viroba hata vitatu kwa buku na fundi akampa 20,000/= tu kumfanyia settings....Pipa anaweza kupata kati ya elfu 30 hadi 50.
Kinadumu kwa muda gani?.
 
Sijaona mahali mmeongelea kibali cha ujenzi.....auinategemea sehemu na sehemu?.
 
ndiyo iliyokuwa nia yangu mkuu mimi kama nina milioni 2 tu siwezi kupanga wala kulalamika ujenzi ni mgumu maana watu wanadanganyana sana kuhusu ujenzi, niambie kwani nini nitakujibu.
Kwanini?
 
Anaweza akaanza na cha pipa mkuu huku akivuta nguvu.

Sink ni Tsh 18,000 , Bomba Type C ni 25,000/= Tofali 8 ni 8,000/= ,Cement mfuko mmoja 13,500/= Mchanga atanunua viroba hata vitatu kwa buku na fundi akampa 20,000/= tu kumfanyia settings....Pipa anaweza kupata kati ya elfu 30 hadi 50.
Kwenye pipa sijaelewa unanyea humo?
 
Kama unalipa laki moja kodi kwa mwezi inaonesha kipato chako ni kizuri. Kwanini usijibane uongeze kidogo mkuu? gharama ya kujenga nyumba ndogo au chumba ni kubwa kuliko ya kujenga vyumba viwili au nyumba kubwa. sijui kama utaelewa
Mwenye uwezo wa kulipa laki kwa mwezi yuko vizuri huyo anatuzuga tu
 
Habari wakuu,

Je, milioni tatu naweza kupata kibanda cha kuishi nimechoka kupanga, huwa nalipa 100k kwa mwezi naona kama nikipata kibanda cha kuishi nitapunguza matumizi?
Kama unacho kiwanja waweza jenga kama hii sehemu yoyote Tanzania
255712050947_status_4a6d9387745d425bb91c200fa75b1351.jpg
 
  • Thanks
Reactions: apk
Back
Top Bottom