Ujenzi wa Miundombinu ya mabasi ya Mwendokasi Awamu ya Nne - Dar unaendelea

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
photo_2024-07-24_16-45-23.jpg

photo_2024-07-24_16-45-18 (2).jpg
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5.

Pia, ujenzi wa miundombinu ya Mabasi hayo unaendelea kuanzia Mwenge - Tegeta (DAWASA) yenye urefu wa kilometa 15.63 ambapo ujenzi huo unatekelezwa na Wakandarasi wawili M/s China Geo Engineering na M/s Shandog Group Co. Ltd.
photo_2024-07-24_16-45-21.jpg
Bashungwa ameeleza hayo Mkoani Dar es Salaam wakati akizungumza na wakazi wa Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali imejipanga vyema kuufungua Mkoa huo kwa miundonbinu ya uhakika ili kutatua kero za foleni za magari.

“Tunao Wakandarasi wanaojenga barabara ya Mwendokasi kuanzia Serena Hoteli kuelekea Mwenge na kutoka Mwenge kuelekea Ubungo (Daraja ya Kijazi), Wakandarasi wako kazini na fedha ipo”, amesema Bashungwa.

Bashungwa amemtaka Mkandarasi Sinohydro Corporation anayetekeleza ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tatu (BRT 3) katika barabara ya Tanganyika Motors – DIT, Uhuru (Buguruni – Msimbazi) Bibi Titi na Shaurimoyo (Karume – Bohari), kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati kulingana na mkataba.

Aidha, Waziri Bashungwa amefafanua kuwa TANROADS wapo katika hatua ya manunuzi ya kumpata Mkandarasi atakayejenga Daraja la Mzinga na kufanya upanuzi wa barabara kuanzia Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu ili kupunguza foleni ya magari na kuondoa adha ya watumiaji wa barabara hiyo kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
photo_2024-07-24_16-40-05.jpg

photo_2024-07-24_16-40-06.jpg
Amefafanua kuwa katika Bajeti ya 2024/25, Serikali imejipanga kufanya upanuzi wa njia nne barabara ya Mwaikibaki (Morocco - Africana) yenye urefu wa kilometa 11.7, itakayoanzia Morocco kuelekea Africana kupitia Kawe ya Chini, Kawe - Lugalo pamoja na kipande cha Mwalimu Nyerere cha kwenda Rose Garden.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kuingia Ubia na Sekta Binafsi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja ya kulipia tozo kama ilivyokuwa katika Daraja la Nyerere Mkoani Dar es Salaam ili fedha hizo zinazopatikana ziweze kutumika katika ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara na madaraja iliyoharibika.
 
Uhaba wa hizo gari ndio changamoto kubwa.
Zinasaidia kusave muda ukishaliotea ila muda wa kuisubiri unaweza kujuta kabisa.
Laiti kama gari zingekua za kutosha hata foleni ingepungua sana maana hata wa gari ndogo akitaka kuwahi na kusave wese angetumia mwendokasi chap kwa haraka.
 
Sawa sawa kabisa
Kuna Saccoss zina hazina ya mpunga mrefu Sana kwanini zisi ingie ubia na serikali kwa kuanzisha huduma za miundombinu za malipo kama hilo daraja la Nyerere. Mfano Ngome Saccoss, Crdb workers, nk nk ziko nyingi Sana. Zina mabilion
 
Hii mipango Yao kama watatekeleza Hadi mwakani nitaipigia Kura CCM Kwa mara ya Kwanza.
Kama watajenga kweli barabara daraja la mzinga na kutanua barabara kutoka rangi3 Hadi vikindu Mimi na ukoo wangu tutawapa Kura CCM
 
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5.

Pia, ujenzi wa miundombinu ya Mabasi hayo unaendelea kuanzia Mwenge - Tegeta (DAWASA) yenye urefu wa kilometa 15.63 ambapo ujenzi huo unatekelezwa na Wakandarasi wawili M/s China Geo Engineering na M/s Shandog Group Co. Ltd.

Bashungwa ameeleza hayo Mkoani Dar es Salaam wakati akizungumza na wakazi wa Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali imejipanga vyema kuufungua Mkoa huo kwa miundonbinu ya uhakika ili kutatua kero za foleni za magari.

“Tunao Wakandarasi wanaojenga barabara ya Mwendokasi kuanzia Serena Hoteli kuelekea Mwenge na kutoka Mwenge kuelekea Ubungo (Daraja ya Kijazi), Wakandarasi wako kazini na fedha ipo”, amesema Bashungwa.

Bashungwa amemtaka Mkandarasi Sinohydro Corporation anayetekeleza ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tatu (BRT 3) katika barabara ya Tanganyika Motors – DIT, Uhuru (Buguruni – Msimbazi) Bibi Titi na Shaurimoyo (Karume – Bohari), kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati kulingana na mkataba.

Aidha, Waziri Bashungwa amefafanua kuwa TANROADS wapo katika hatua ya manunuzi ya kumpata Mkandarasi atakayejenga Daraja la Mzinga na kufanya upanuzi wa barabara kuanzia Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu ili kupunguza foleni ya magari na kuondoa adha ya watumiaji wa barabara hiyo kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Amefafanua kuwa katika Bajeti ya 2024/25, Serikali imejipanga kufanya upanuzi wa njia nne barabara ya Mwaikibaki (Morocco - Africana) yenye urefu wa kilometa 11.7, itakayoanzia Morocco kuelekea Africana kupitia Kawe ya Chini, Kawe - Lugalo pamoja na kipande cha Mwalimu Nyerere cha kwenda Rose Garden.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kuingia Ubia na Sekta Binafsi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja ya kulipia tozo kama ilivyokuwa katika Daraja la Nyerere Mkoani Dar es Salaam ili fedha hizo zinazopatikana ziweze kutumika katika ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara na madaraja iliyoharibika.

WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.01.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.01(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.01(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.02.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.03.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.04.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.05.jpeg
 
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya Nne (BRT 4) kuanzia Daraja la Kijazi (Sam Nujoma) - Mwenge - Maktaba ya Taifa (Posta) yenye urefu wa kilometa 13.5.

Pia, ujenzi wa miundombinu ya Mabasi hayo unaendelea kuanzia Mwenge - Tegeta (DAWASA) yenye urefu wa kilometa 15.63 ambapo ujenzi huo unatekelezwa na Wakandarasi wawili M/s China Geo Engineering na M/s Shandog Group Co. Ltd.

Bashungwa ameeleza hayo Mkoani Dar es Salaam wakati akizungumza na wakazi wa Mkoa huo ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali imejipanga vyema kuufungua Mkoa huo kwa miundonbinu ya uhakika ili kutatua kero za foleni za magari.

“Tunao Wakandarasi wanaojenga barabara ya Mwendokasi kuanzia Serena Hoteli kuelekea Mwenge na kutoka Mwenge kuelekea Ubungo (Daraja ya Kijazi), Wakandarasi wako kazini na fedha ipo”, amesema Bashungwa.

Bashungwa amemtaka Mkandarasi Sinohydro Corporation anayetekeleza ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tatu (BRT 3) katika barabara ya Tanganyika Motors – DIT, Uhuru (Buguruni – Msimbazi) Bibi Titi na Shaurimoyo (Karume – Bohari), kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati kulingana na mkataba.

Aidha, Waziri Bashungwa amefafanua kuwa TANROADS wapo katika hatua ya manunuzi ya kumpata Mkandarasi atakayejenga Daraja la Mzinga na kufanya upanuzi wa barabara kuanzia Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu ili kupunguza foleni ya magari na kuondoa adha ya watumiaji wa barabara hiyo kwa wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Amefafanua kuwa katika Bajeti ya 2024/25, Serikali imejipanga kufanya upanuzi wa njia nne barabara ya Mwaikibaki (Morocco - Africana) yenye urefu wa kilometa 11.7, itakayoanzia Morocco kuelekea Africana kupitia Kawe ya Chini, Kawe - Lugalo pamoja na kipande cha Mwalimu Nyerere cha kwenda Rose Garden.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi kuingia Ubia na Sekta Binafsi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja ya kulipia tozo kama ilivyokuwa katika Daraja la Nyerere Mkoani Dar es Salaam ili fedha hizo zinazopatikana ziweze kutumika katika ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara na madaraja iliyoharibika.

View attachment 3051028View attachment 3051029View attachment 3051030View attachment 3051031View attachment 3051033View attachment 3051034View attachment 3051035View attachment 3051037
Mkuu hivi ile miradi yetu ya DMDP iliishia wapi? Mbona serikali haiiongelei tena miradi hii?
 
WhatsApp Image 2024-07-24 at 15.03.02.jpeg

Tanzania kama nchi tuna watu wana akili ndogo sana. Yaani uelewa wao ni mdogo kias hata unajiuliza kama ndio Baba kwenye familia anawezaje kuiongoza Kwa kiwango kidogo cha akili aliyo nayo.

Tukio lilikua ni ni kuhusu Barabara ambazo ni za watumiaji wa itikadi zote. Lakini anatokea mkosa akili mmoja huko alikotoka anakuja amevaa sare za chama.

Yaani kwa kiwango hiki cha akili ndio maana Tanzania ni nchi ambayo ni rahisi sana kuiongoza. Sababu watu wake wengi wana upeo duni sana wa kichanganua na kuelewa mambo.
 
Back
Top Bottom